COVID-19: Watumishi wa Afya ni kama tumetolewa kafara?

COVID-19: Watumishi wa Afya ni kama tumetolewa kafara?

Wahudumu wa afya wote wapewe chanjo ya covid19

Japo pia huwa siwaelewi hao wazungu wanachanjwa lakini bado wanaendelea kuvaa barakoa wanaogopa nini sasa

Kwa hapa wazungu wamefanikiwa kutuchanganya
 
Asilimia kubwa ya watumishi wa uma wa Tz ni wajinga na wapumbavu waliotawaliwa na uoga, mfano wa afya nyinyi ndio mnaojua hali halisi ya corona cha ajabu mmekaa kimya as if hamna chochote, askari huna silaha alafu eti uko front line kupambana na adui? Vifaa vya kujikinga mahospitalini hakuna sasa mnajikinga vipi kama sio kuhatarisha maisha yenu na vizaz vyenu, kwann msiwe na sauti moja ikiwezekana kuishinikiza serikali hata kwa mgomo? Nawakubali sana wakenya hawana huu ujinga ujinga wa kupelekeshwa ovyo.
Kwa hiyo ungekuwa na wewe ni mtumishi wa umma basi ungekuwa jasiri, mwerevu, unaye simama mbele za vyombo vya habari kuikemea Serikali ya Magufuli, ungekuwa ni mtumishi wa umma asiye ogopa chochote!!

Unaongelea tuwe na sauti moja kama Wakenya! Unafahamu kitambo vyama vyote vya Wafanyakazi vinaongozwa na Makada wa Ccm? Utasema kwa nini tumewaruhusu waongoze bila shaka! Jibu ni kwamba, mbona na wewe hukufanya chochote Ccm ilipo amua kwa makusudi kuuvuruga uchaguzi mkuu wa 2020?

Unafanya shughuli gani mwenzetu inayokufanya uwe jasiri na mwerevu awamu hii ya pili ya Rais aliyejimilikisha kila kitu? Unadhani hao Watumishi wa umma hawana familia zinazo wategemea?
 
mmeshindwa kutengeneza PPE zenu wenyewe, kila kitu mnataka mpewe tu. Inabidi baadhi ya hospitali mbadili mitazamo mwaanzishe viwanda vyenu vya kutengeneza PPE zenu wenyewe si kila kitu kulalama tu
Akili za kuku zimejaa CCM.
 
Naomba kukumbushwa au kukosolewa... ?, Hivi TZ haikupata misaada ya kupigana na Corona ?, hizo pesa zilienda kufanya nini, nilidhani zingefanya kazi kama hizi..., vilevile wale watu wa muhimbili hawakusema kwamba wameweza kutengeneza vifaa vya kujikinga cheaply viliishia wapi ? Hata kama huku hatuna Ugonjwa si tuwape ndugu zetu wa Kenya wenye uhitaji ......
 
Back
Top Bottom