Covid19 ni virus?
Kama ndivyo
Virus : Non living organism outside of the host cell (si kiumbe Hai nje ya seli ya kiumbe hai)
Mate hayana seli za kumuhifadhi(to host) kirusi.
Je! Ni kwa namna gani Korona inaweza ambukizwa kwa njia ya hewa, (drop lets)?
Kawaida ya magonjwa ya virusi mtu akibahatika kupona yanamjengea Kinga mwili dhidi ya ugonjwa husika,
Ajabu ni kwa Korona haifanyi Hivi.
Ukipona, ikikupata Tena inakuenyesha kama Kawaida.
MASWALI KWA WATAALAMU WETU WA AFYA
#1 Korona ni ugonjwa wa virusi kweli(viral disease)??
Kama ndivyo ama sivyo;
#2 Korona inaambukizwa kwa njia gani haswa?
#3 Ulaya na Asia wanajikinga vizuri Sana ikiwemo kwa kuvaa Barakoa, ni kwa nini Korona inazidi kusambaa zaidi na zaidi?
**IFAHAMIKE KWAMBA
Sijabisha kuhusu uwepo wa Korona,
Mfano (pia siwezi Kuwa na mawazo finyu kama ya kupima HIV au COVID19 kwenye embe.
Kwa sababu :
@1 HIV virus tunapima Kinga mwili (Antibodies), na embe halina antibodies tuzipimazo
@2 Kipimo husika kinahitaji sampuli sahihi na kwa kiwango sahihi.)
1: Kwa mujibu wa tafiti na vitendanishi vilivyofanyika kiumbe hiki kimebeba sifa za kirusi.
2: Korona inaambukizwa kwa:
- njia ya hewa (droplets)
-mgusano/contact (eneo ambalo droplet zilidondoka kama meza, kiti, simu na wakati huo muda wa kirusi kufa haujafika nk.)
-fumes/hewa (pale ambapo mtu aliyeambukizwa virusi anapojisaidia na kufrash choo, ile hewa inayopanda juu kama ukiingia kabla ya muda wa kirusi kufa). Hapa pia kunaweza kuwa na uhusiano wa fecal - oral kama hautanawa mikono vizuri baada ya haja kubwa na kutawaza.
3: Maambukizi kuendelea kuwa juu pamoja na matumizi ya mask. Njia ya kuambukiza si ya hewa/droplets tu kama ilivyoelezwa hapo juu. Pia, vitu vingine kama vitu tunavyonunua na kuleta majumbani, simu na mfumo wa macho pia yametajwa. Hii inaweza kuwa sababu kwamba njia ya kujikinga si matumizi ya mask tu bali kujikinga na mzunguko mzima kama ilivyoelezwa kule juu.
Suala la kinga: hii inatokana na mnyumbuliko wa kirusi toka uzao mmoja kwenda mwingine na ikiwa inaonyesha kuongezeka kwa ukali wa kizazi kinachofuata.
Upimaji wa Embe: kipimo cha Korona kilichokuwa kinatumika ni cha PCR ambacho kinatafuta DNA na si antibody. Hivyo, kulingana na contamination unaweza kupata kwenye vitu vingine.
Kuhusu kuishi kwenye mate: ndiyo maana kuna muda unaambiwa baada ya muda kirusi kinakufa kinapokuwa kwenye droplets, lakini hakifi ghafla kuna muda maalumu mtu unapogusa kabla ya huo muda ndo unakirudisha kwenye mzunguko wa uhai.
Wale virusi wa HIV ni selective wanaishi kwenye CD4 cells, hapo pia kuna utofauti wa maisha. Lakini unaweza kuona kuna muda toka maambukizi mpaka akavamie CD4 cells na anakuwa bado hai. Ila akikuta mtu hana specific receptor kwenye CD4 cell zake, maisha huwa magumu kwake pia.
Pia, Korona ina athari kubwa karibu kwa kila eneo la mwili. Viungo vingi vinaweza kuathiriwa hata bila kirusi kufika eneo husika mfano: kuongezeka kwa specific gravity ya damu/thickness inatosha kuumiza viungo vingi sana. Uwezo wa kusambaza chakula na oksijeni unakuwa umetatizwa. Uwezekano wa damu kuganda, stroke, figo kufeli, pulmonary embolism nk.
Hivyo mtu anaweza kufa kwa madhara haya hata kama mwili ulikuwa na uwezo wa kupambana na kirusi husika yaani wakati unapambana na kirusi huku damu inakuwa nzito na unakufa kwa pulmonary embolism.
Pia kuna watu wanakufa kutokana na kinga za mwili kuwa na nguvu sana mfano: kuna watu wanakufa kwa cytokines storm/ ambayo ni pale mwili unapo-overeact dhidi ya kirusi husika.
Lakini pia, mhimu kukili kwamba mambo mengi ni mapya juu ya tatizo husika ndiyo maana mambo mengi yanaendelea kubadilika katika tiba na kujikinga kulingana na muda unavyoendelea.