Ngatele
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 808
- 704
Sampuli ngapi? Tunasikia wenzetu kati ya 600 au 800 wagonjwa kadhaa wamepatikana. Hiyo ingetuonesha walau jitihada katika upimaji wa wale contacts na pia kuelewa kama kuna changamoto ya vipimo. Jana nilisikia majirani zetu wakisema wanasambaza vipimo vya corona zaidi ya 1000 lakini sisi tunazidi kusikia sampuli kupelekwa sijui kwa Mkemia Mkuu(kama niko sahihi).
Tunaiona jitihada ya serikali lakini uwazi zaidi unahitajika na kama ni takwa la kimataifa (WHO), ni vizuri tukalitekeleza. Yawezekana hali ya ugonjwa kwa maana ya idadi ya wagonjwa nk ikawa ni kigezo cha kupewa misaada au kusamehewa madeni au kusogezwa muda mbele wa kulipa madeni ili pesa kidogo tuliyonayo itumike kushushughulikia janga hili.
Kama pengine tulianza vibaya si vibaya kurekebisha yale ambayo tunaona hayajatusaidia kwani hali yaweza kuwa mbaya hapo baadaye kama hatukuweka sawa mipango yetu.
Tuchape kazi lakini tukumbuke kuwa ugonjwa huu huonekana baada ya siku 14 na hivyo aliyeambukizwa anaweza akawa anaambukiza wengine kabla ya dalili hazijajitoleza. Leo nilikwenda Kariakoo nikiwa nimevaa Barakowa, katika watu zaidi ya 200 kwa wastani utakutana na mtu mmoja mwingine kavaa Barakowa na watu wanakuwa kama wanakushangaa kama wanaona mzungu katoka nje. Mungu atusaidie lakini inabidi tujisaidie pia.