Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara wafanya magendo Tarime, Wauaji na wakwepa kodi au wanasiasa wanaotumika kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya Serikali na pia kudhurumu Haki za watu wasio na nguvu au utetezi.Mnamo Tarehe 30 Desember 2022, Majira ya saa 6 usiku, maofisa wa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa walifika katika Hotel ya PKM Tarime Mjini na kumkamata Ndugu Lameck Cowiti. Operation ambayo ilionekana ya siri maana walimdaka nje ya uzio kabla hajaingia hotelini.
Alikuwa akitokea katika Hotel ya Lakairo kwa ajili ya Chakula na vinywaji.
Huenda ponapona yake ni kwa sababu kuna kijana anamfahamu na aliona ule mchezo hivyo kuwataarifu ndugu zake. Ambao mapema tarehe 31 Desember walianza kufuatilia Polisi licha ya kufukuzwa na kukataliwa kumuona.
Duru zinasema kilichomgharimu Bwana Cowiti ni uzalendo wake wa kupambana na maovu katika jamii yake ambayo kwa kiasi kikubwa inaonekana viongozi wengi kama si wote wa Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa wanaungana na magenge ya Majambazi, wauaji na wakwepa kodi ili kunufaika kwa mapato haramu.
Kilichomgharimu ni kama IFUATAVYO.
COWITI: WAFANYABIASHARA WADHURUMAJI NA WAUAJI TARIME WAUNGANA NA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI NA USALAMA WA TAIFA TARIME KUMUUMIZA KWA YEYE KUTETEA HAKI ZA WANAOUWAWA NA KUZURUMIWA.
1. ALISIMAMIA KUKAMATWA KWA SIMON KILESI (MFANYABIASHARA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI TARIME VIJIJINI) BAADA YA KUMUUA JOHNSON MSIRANGA
2. ALISIMAMIA HAKI YA MDHURUMIWA WA NYUMBA AMBAYO MFANYABIASHARA JURA ALIMUUZIA MFANYABIASHARA MWENZIE DHURUMATI PETER ZAKARIA
1. Mnamo May 2021, Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, Simon Kilesi alimuua Johnson Msiranga.
Baada ya mauaji hayo alifanya mpango na OCCID aliyekuwepo wakati huo waseme kuwa Kijana Johnson ameuwawa na wananchi wenye hasira kali.
Baada ya kujulishwa juu ya mauaji na njama za kuficha mauaji hayo, Afisa Usalama wa Wilaya alisema hao watu (OCCID) ni watu anaofanya nao kazi hivyo kuliingilia jambo hilo hawezi.
Ndipo Ndugu Lameck Cowiti alipata taarifa na kuwajulisha viongozi wa juu wa serikali juu ya mauaji hayo, Ndipo Mh. Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama Tarime ikae na kupitia ushahidi ndipo kweli ikathibitika Simon Kilesi ana kesi ya mauaji Ndipo akakamatwa na kufunguliwa kesi ya mauaji.
Lakini baada ya miezi miwili Bwana Kilesi kwa kutumia rushwa alibadilishiwa kesi na kuwa ya kuua bila kukusudia hivyo yeye na watuhumiwa wenzake wakapata dhamana.
Kesi ikaendelea na imemalizika October 2022 kwa kumuchia huru Simon Kilesi na wenzie kuwa hawana hatia japo postmortem ripoti na hati ya kifo inaonyesha kuwa Johnson Msiranga aliuwawa.
Ndipo Simon Kilesi akasema lazima afanye kisasi ili Lameck Cowiti akamatwe kwa namna yeyote ili aweze kulipa kisasi kwani kwa sababu yake ametumia zaidi ya milioni 700 ili kumaliza kesi hiyo hadi kuonekana hana hatia, hivyo kamrudisha nyuma kibiashara.
2. Dhurmati ya nyumba maarufu kama Girango Hotel Tarime Mjini.
Mwaka 2019 aliyekuwa mpangaji wa nyumba mali ya Jonathan Waluse, ambaye anajulikana kwa jina la Girango aliuza nyumba hiyo isiyo mali yake kwa thamani ya milioni 200.
Nyumba hiyo imepangwa na Girango kwa muda mrefu ambapo alikuwa anaendesha biashara ya Hotel na ndio maana inajulikana hadi leo kama Girango Hotel.
Nyumba hiyo ilionekana inauzwa kwa Mfanyabisahara Jura lakini kwenye mkataba wa mauziano likaandikwa jina la mke mdogo wa mfanyabiashara Peter Zakaria ambaye ni Hakimu katika wilaya ya Serengeti ajulikanaye kwa jina la Mh. Mzarifu.
Baada ya kumuuzia walimuahidi kuwa watamletea Hati Halisi za nyumba hiyo. Ndipo Girango akamfuata Mzee Jonathan Waluse anapoishi katika Wilaya ya Butiama akampatia milioni 20 na kumtaka ampatie Hati ya nyumba.
Mzee Waluse akakataa kutoa Hati akisema kama wanalipa hiyo milioni 20 kama kodi ni sawa ila sio kuwapa Hati.
Ndipo wakala njama na Polisi Tarime wakamkamata kuwa ameghushi nyaraja za Nyumba na akafunguliwa mashitaka, akafungwa na kupelekwa gereza la Serengeti.
Mzee Jonathan Waluse akiwa gerezani Serengeti alifuatwa na Jura na Hakimu Mzarifu wakimtaka awape Hati Halisi ya nyumba na Mzee huyo alipiga mayowe kwa sauti kubwa akilia akiwa mle ndani ya gereza.
Ndipo Lameck Cowiti akaanza kufuatilia kesi hiyo kwani Mzee Jonathan Waluse ni mjomba wake. Akamkatia rufaa, kesi ikafutwa na ikadhihirika kuwa nyumba ni mali halali ya Mzee Waluse.
Ndipo Lameck Cowiti akamsaidia mjomba wake kufungua kesi kudai nyumba yake kwani tayari inamilikiwa na Hakimu Mzarifu kinyume na sheria.
Kesi ilikuwa inaendelea kufikia mwishoni na ndipo Lameck Cowiti akafika Tarime tarehe 24 December 2022 akiwa na nyaraka za kukamilisha kesi hiyo ili Mzee Jonathan Waluse aweze kukabidhiwa nyumba yake.
NJAMA ZA KUMKAMATA LAMECK COWITI TARIME
Baada ya Simon Kilesi, Range Boazi Range (maaruru kama) na Peter Zakaria kupata taarifa kuwa Lameck Cowiti yuko Tarime wakaanza kupanga njama za kumpa kesi ili wamkamate na kumfungulia kesi ili wadidimize juhudi zake za kumsaidia Mzee Waluse kupata nyumba yake, na pia kulipiza kisasi kwa kuhakikisha Simon Kilesi anafunguliwa kesi ya mauaji ya Jonathan Msiranga.
Njama hizo zimepangwa na watuhumiwa hao wakishirikiana na RPC Tarime Rorya, na baadhi ya maofisa wa Usalama wa Taifa Tarime.
BAADA YA NDUGU KUFIKA POLISI
Ndugu zake Lameck Cowiti walipofika kituo cha Polisi walifukuzwa na kunyimwa fursa ya kumuona Ndugu yao.
Na awali siku ya kwanza walikatazwa hata kumpelekea Chakula.
POLISI NA USALAMA WARUSHIANA MPIRA.
Viongozi wa Polisi walipoulizwa kuwa ndugu wanataka kujua kosa la ndugu yao ni nini walisema kuwa wao hawajamkamata bali amekamatwa na idara ya Usalama wa Taifa.
Walipoulizwa ni Idara ya Usalama Dodoma au wapi ili waende wakasema ni Idara ya Usalama Tarime na kuwa wao wamemtunza tu.
WAHAHA KUTAFUTA WATU ILI WASEME ALIWATAPELI, WASHINDWA KUMCHUKUA MAELEZO HADI LEO.
Baada ya wao kumkamata na hatimaye ikajulikana tofauti na walivyodhamiria toka tarehe 30 Desember hadi leo hawajamchukua maelezo wala kumpeleka mahakamani.
Wamekuwa wakihangaika kutafuta watu wasimame kama wametapeliwa nae kwa kutumia jina la Idara ya Usalama wa Taifa.
Hadi leo tarehe 3 January bado hawajapta idadi ya waliotarajia kwani hakuna ushahidi katika waliyokusudia bali ni kutaka kumkomoa.
WAFANYABIASHARA NA WANASIASA WALIOFIKA KITUONI KUMTISHA.
Tarehe 31 Disemba 2022, Lameck akiwa KITUONI, Mfanyabiashara Range Boazi Range maarufu kama Jura alifika kituoni tena mbele ya Askari Polisi waliokuwa zamu na kumtisha kuwa huwa anajidai mjanja na sasa amekwisha.
Leo Tarehe 3 January 2023, aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye maarufu kama Namba Tatu naye alifika kituo cha Polisi na kumueleza kuwa ripoti yake aliyoandika kwa wakubwa kuhusiana na rafiki yake aliyekamatwa anaiba mafuta katika mradi wa Umeme wa Mwl. Nyerere ndio ulifanya jina lake likatwe kutetea nafasi yake hivyo nae atahakikisha wanamkomesha.
OMBI KWA VIONGOZI WA SERIKALI
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara wafanya magendo Tarime, Wauaji na wakwepa kodi au wanasiasa wanaotumika kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya Serikali na pia kudhurumu Haki za watu wasio na nguvu au utetezi.
Kundi hili linakula na viongozi wa Idara nyeti za Serikali na ndio maana pamoja na Uhalifu na uozo wao bado wako uraiani.
Imefikia hatua hata wananchi wanaogopa kutoa taarifa za Uhalifu kwa kuhofia maisha yao au kubambikiwa kesi kama ilivyo kwa Bwana Lameck Cowiti.
Hili kundi linaongozwa na Mfanyabiashara Peter Zakaria na vijana wake kina Jura, Simon Kilesi (muuaji), Namba Tatu, Kiraa na wengine wengi wakishirikiana na VIONGOZI wa Vyombo vya Dola.
ZAIDI WAANGALIE KESI YA MAUAJI ILIYOKUWA INAMKABILI SIMON KILESI YENYE USHAHIDI WA WAZI ILIISHAJE KWA YEYE KUACHIWA HURU WAKATI ALIUA?
Zaidi waangalie usalama wa Lameck Cowiti akiwa kituo cha Polisi Tarime kwani kwa namna alivyokamatwa kama wasingejulikana huenda walikusudia kumuua au kumdhuru kwa namna yoyote.
Na hadi sasa wamemnyima mawasiliano na ndugu zake, kwani ndugu zake wakienda kituoni wanafukuzwa.
Pia suala la nyumba ya Mzee Waluse asaidiwe kupata Haki yake.
Na wafumue watendaji waliopo katika Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Takukuru, Uhamiaji, TRA.
NB: Nimeattach barua za mwenendo wa kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili Kilesi ambayo imemalizwa kihuni na bila Haki Kutendeka.
Kundi hili linakula na viongozi wa Idara nyeti za Serikali na ndio maana pamoja na Uhalifu na uozo wao bado wako uraiani.
Imefikia hatua hata wananchi wanaogopa kutoa taarifa za Uhalifu kwa kuhofia maisha yao au kubambikiwa kesi kama ilivyo kwa Bwana Lameck Cowiti.
Hili kundi linaongozwa na Mfanyabiashara Peter Zakaria na vijana wake kina Jura, Simon Kilesi (muuaji), Namba Tatu, Kiraa na wengine wengi wakishirikiana na VIONGOZI wa Vyombo vya Dola.