CP Salum Hamduni anastahili kuwa IGP Mpya

Operation gani Kali serious za kipolisi alishawahi endesha kwa ufanisi

Elezea
Unajua kazi alizowahi kufanya Hamduni? Au kwa vile yeye hatembei na media?
 
Waislamu mmeingia kazini eeh!

Halafu akiishaingia muanze kusema kuna waislamu wenzake wanateseka magerezani?

Taja vigezo na sifa zake watu wazijue na kumpima sio kukurupuka na kuja kuchora chora upupu humu.

IGP mpya hapaswi kutokana na huu mfumo uliooza wa kipolisi nchini.

Safari hii atatoka JWTZ moja kwa moja.
 
Hapo kitoke chuma kiingie chuma... hatutaki wapole sisi. Unajua maana ya askari?
 
Utabidi wako waweza timia ila nina wasiwasi na yule kamishna aliepandishwa vyeo juzi kati kule zanzibar
 
Kwenye siasa ukiwashambulia Polisi unapigiwa makofi mengi Sana na sababu kubwa ni kwamba Polisi wana deal na pande mbili moja ni mlalamikaji na wa pili ni mlalamikiwa kama pande moja haijakubali huduma za Polisi kinachofiata ni hasira dhidi ya Polisi na ule upande uliofanikiwa kwenye kesi.

Hivyo basi ni vigumu kubalance ili pande zote ziwakubali.

Hatahivyo Kuna mambo kadhaa wenzetu hawa wamekuwa wakiyafanya ni ya hovyo Sana ingawa tatizo hili limeenea kwenye taasisi nyingi mno labda ni kwasababu ya mmomonyoko wa maadili Jambo ambao ni janga la kitaifa.

Chakufanya kama nchi HAKI ianze kusimamiwa Kwa utaratibu utakao kubalika kimataifa na kitaifa hasa kisiasa,KIJAMII na kiuchumi.

Wanasiasa wasiwe wao ndiyo wanajua kila kitu na kutuamulia mambo Kwa matakwa Yao binafsi pamoja na familia zao na familia za rafiki zao.
 
IGP Siro siku zote tunasema ni Operational Officer na siyo National Leader, siyo mtu wa kufanya maamuzi ya kiuongozi ndiyo maana tunaona jeshi limemshinda, yeye alisikia tu kelele keshakimbia site na kupiga mikwara na kelele lakini mbinu za kumaliza tatizo hana. Hana mbinu za kisasa kulisimamia jeshi.
 
Asante sana kwa kupandisha uzi huu
 
Operation zote za Ugaidi hapa nchini ni kazi yake

Alifuzu mafunzo hayo Marekani miaka ya 2010

Muonekano wake ulisaidia sana kuwanasa Magaidi waliotaka kunajisi Taifa letu
Operation gani Kali serious za kipolisi alishawahi endesha kwa ufanisi

Elezea
 
Wanabadilikaga lingana na mfumo, kiujumla jeshi la police linatakiwa sukwa upya, sambamba na katiba mpya
 
Operation zote za Ugaidi hapa nchini ni kazi yake

Alifuzu mafunzo hayo Marekani miaka ya 2010

Muonekano wake ulisaidia sana kuwanasa Magaidi waliotaka kunajisi Taifa letu
Jambo lingine muhimu alilonalo..sio mpenda rushwa wala kujipendekeza, aliteswa sana na viongozi wake kwani alikuwa hapeleki marupurupu kwao kama wafanyavyo ma RC wengine, ndio maana alihamishiwa mikoa mingi kwa muda mfupi
 
Wanao bisha waende wakamuulize Sabaya kule gerezani anamjua vizuri sana kwenye lile sakata la reli Kilimanjaro
 
Yule Kamanda Awadh, Tundu Lissu na Ernest Mangu kabila lao moja. Wote wa Singida
Utabidi wako waweza timia ila nina wasiwasi na yule kamishna aliepandishwa vyeo juzi kati kule zanzibar
 
Operation gani Kali serious za kipolisi alishawahi endesha kwa ufanisi

Elezea
Kibiti,mtwara,kigoma,kagera hasa ngara,njombe,Tarime na maeneo mengineyo na kwote hali ni shwari kabisa.
 
Hakuna kinachobadilika zaidi ya kusifu na kuabudu
 
Mimi sina shida na Hamdun wala Senior commissioner yeyote yule kutoka Police. Hata Simon Sirro tunayembeza sasa hakuwa mbaya kihivyo kabla hajakuwa IGP. Sirro aliharibiwa na DIKTETA Magufuli, baada ya Magufuli kutengua uIGP wa Ernest Mangu aliyekuwako toka enzi za JK. Sirro alisoma hadi Seminari Kuu na alibakiza miaka 2 kuwa Padre wa Kanisa Katoliki. Mtaniuliza kwa nini alikubali kutumikia mfumo kandamizi? Angeweza kujitenga na maamuzi mabaya ya Magufuli pengine yangeweza kumkuta mabaya toka kwa yule shetani.

Watendaji wa Rais kwenye vyombo kama Polisi huenda na haiba ya Rais ambaye ndiye anayewapa uteuzi. Tumeona kwa vile Rais SSH hapendi unyanyasaji na DHULUMA basi IGP yeyote atakayemteua itabidi awe mtu wa namna hiyo.

HITIMISHO:
Teuzi za wakuu wa vyombo vya Dola kama TISS, POLICE, TPDF zitapata suluhisho tu kwa kupitia Katiba Mpya ambayo itataka uteuzi wa Rais uwe na endorsement ya Bunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…