CP Salum Hamduni anastahili kuwa IGP Mpya

Mbona hujatupa wasifu wake kwa kina zaidi ya kumsifia tu
 
Kwa nini siyo promo hii?

Umetaja madhaifu ya Siro, kwa nini usiweke wazi sifa za unayempigia promo, umeishia tu kusifia blah blah bila ya kuweka ama kutaja vigezo vyovyote?

Kwanza tujiulize, huyo mtu unayemuombea u Igp, tangia awekwe Takukuru kaleta mabadiliko gani chanya yenye kuonekana katika taasisi hiyo?

Halafu mi'huwa namuona ni kama jamaa mwenye haiba flani ya upole wenye kupitiliza ambaye angefaa kuwa "mchungaji" wa kanisa flani ama Shehe wa nsikiti?

Ujue kuna ngazi za uongozi wa kadi flani hazitakiwi lelemama ama kupelekwa kisiasa kwa ajili ya kufurahisha watu, hasa hizi kada za kutiisha sheria.
Simjui kwa undani Mkuu..Ila upole ni sura tu,nadhani huwa anajisimamia wakati mwingine,alikataa mchongo wa Sabaya wa kutaka kuwaundia tuhuma feki wafanyabiashara fulani,huko Kilimanjaro,akiwa RPC huko,tena enzi za mwendazake..' Nilisoma Uzi humu'..Wale wafanyabiashara walikataa kutoa ngawila Kwa Sabaya..
 
Wajameni sihitaji kuongelea sura ya mtu, Imani, rangi au ukanda, hapa nazungumzia weledi na hofu ya Mungu. Huyu bwana ana busara, mweledi, mwelewa, ana hofu ya Mungu na ni Mchapakazi.

Kutokana kama kashfa nzito zinazolikabili jeshi la polisi hivi sasa, ni kweli linahitaji mtu aina ya Salum Hamduni. Waswahili wanasema myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, huyu bwana anastahili nafasi hii. Uozo uliopo ndani ya Polisi unahitaji mtu makini na mfuatiliaji na siyo mpiga kelele tu.

IGP Siro siku zote tunasema ni Operational Officer na siyo National Leader, siyo mtu wa kufanya maamuzi ya kiuongozi ndiyo maana tunaona jeshi limemshinda, yeye alisikia tu kelele keshakimbia site na kupiga mikwara na kelele lakini mbinu za kumaliza tatizo hana. Hana mbinu za kisasa kulisimamia jeshi.

Mama ikimpendeza amteue Salum Hamduni kwenye nafasi hii, hanijui mimi kwa namna yeyote ile na wala simpigii promo lakini ninamfahamu kwa uchapa kazi wake.
Wenye nchi yao watakupinga weeeeee,
Kisa watasema huyu mwarabu
Ila jamaa anafaa
 
Kama vp hata Kamanda wa kanda maalum bwana Jumanne
 
Operation gani Kali serious za kipolisi alishawahi endesha kwa ufanisi

Elezea
Hii hapa , ya wizi wa kura Jimbo la Ukonga hebu mwangalie alivyosimama kwa ukakamavu

Uyu_Binadam_kama_angekuwa_Uwaziri_wa_Mambo_ya_ndani_au_Rais_Sijui_Tanzania_ingekuwaje_%3F_%F0%...jpg
 
Tatizo la jeshi la polisi sio IGP kama mtu binafsi ila ni kwamba jeshi hilo limekuwa Heavily Politicized kiasi kwamba hata wamuweke nani kuwa bosi wake ni kazi bure.

Tusidanganyane, huyo bwana unayemfagilia akisikia kwamba wafuasi wa Chadema wamepigwa na kujeruhiwa sehemu unafikiri atachukua hatua yoyote si naye atameza pini tu kama ambavyo wamekuwa wakifanya watangulizi wake.

Hamna kitu hapo, tupate katiba mpya itakayotenganisha huduma za polisi "Police Services" na mambo ya siasa tofauti na hapo ni kudanganyana tu, tutabaki kufagilia watu kwa sababu za "Religious Ties" tu na vitu kama hivyo.
 
Kwa michache tunayojua, hakupenda jeshi kufanya kazi za kisiasa za kudhibiti upinzani au za kihalifu kama kuteka raia na kuwaua kubambikia kesi, kupora mali na fedha, kulazimisha rushwa, na dhuluma nyingine nyingi. Mengine kumhusu hatuyajui, na hatuna sababu za kuyajua kuliko mamlaka za juu yake.

Kwa sifa hiyo pekee, Hamduni ni kiongozi anayefaa kuliondoa jeshi la polisi kwenye uozo lilikojiingiza au lilikoingizwa na wanasiasa. Pia yawezekana akawa kiongozi sahihi wa kusimamia mabadiliko "reforms" mbalimbali kw3nye jeshi hilo, ili kulisogeza kwa wananchi, na kulifanya liwe la wananchi, kuliko lilivyo sasa la serikali.
Hamduni huyuhuyu?
 
Huyu mie namjua maana wote tumezaliwa nzega,tabora japo ni mdogo kwangu,kasoma sheria,akaingia tiss,na kapita jeshini pia,ni mkimya,haba makuu,haogopi na ana ujasiri wa hali ya juu,baba yake ba mana yake ni waarabu,ika baba alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na ndugu zake wote wamesoma.sasa kuwa igp siwezi kujua,rushwa hapokei na anasaidia wanaonewa sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Huu ni uongo wa wazi, hamduni huyuhuyu aliyekua RPC Arusha??
 
Wajameni sihitaji kuongelea sura ya mtu, Imani, rangi au ukanda, hapa nazungumzia weledi na hofu ya Mungu. Huyu bwana ana busara, mweledi, mwelewa, ana hofu ya Mungu na ni Mchapakazi.

Kutokana kama kashfa nzito zinazolikabili jeshi la polisi hivi sasa, ni kweli linahitaji mtu aina ya Salum Hamduni. Waswahili wanasema myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, huyu bwana anastahili nafasi hii. Uozo uliopo ndani ya Polisi unahitaji mtu makini na mfuatiliaji na siyo mpiga kelele tu.

IGP Siro siku zote tunasema ni Operational Officer na siyo National Leader, siyo mtu wa kufanya maamuzi ya kiuongozi ndiyo maana tunaona jeshi limemshinda, yeye alisikia tu kelele keshakimbia site na kupiga mikwara na kelele lakini mbinu za kumaliza tatizo hana. Hana mbinu za kisasa kulisimamia jeshi.

Mama ikimpendeza amteue Salum Hamduni kwenye nafasi hii, hanijui mimi kwa namna yeyote ile na wala simpigii promo lakini ninamfahamu kwa uchapa kazi wake.
Tunajua mnataka kumuondoa Nsiro kwa kuwa yeye hajali huyu ana cheo au la kama mnavyotaka. Sasa mtoeni tu na watoeni Mawaziri wote, manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya wawekeni watu wenu mzudi kufurahi maana mpaka sasa hamjaridhika!
 
Jeshi la Polisi ndiyo jeshi pekee linalotumiwa vibaya zaidi na wanasiasa. Amini, usiamini, hata kama mmoja wa malaika wa Mungu atashuka kuja kuwa IGP, bado Jeshi la Polisi litaendelea kuwa tatizo kwa Watanzania!
Mfumo wa kumpata mkuu wa polisi watakiwa kukarabatiwa.
Hapa kwetu wenye nyota (Commissioned Officers) ni uteuzi wa rais na hapo ndio siasa inapoingilia. Wenzetu Kenya baada ya kupata matatizo ya rushwa na ukabila kwa miaka mingi, wameanza utaratibu wa WAZI zaidi. Waombaji wanatuma maombi, wanachujwa na baadae kufanya interview ya WAZI kwa tume maalum. Mshindi ndio anateuliwa na Rais. KENYA’S NEW POLICE CHIEF APPOINTMENT - kenyaforum.net
Sasa wako mbioni kuanza hayo kwenye hatua ya County ambayo kwetu huku ni MKOA
 
Hiyo approach yao ni prescription ya issue moja tu: ukabila katika upatikanaji wa IGP. Issues zingine zote ziko pale pale. As long as chain of command ya police force inahusisha wanasiasa ndani yake, process nzuri ya kumpata IGP by itself haiwezi kuboresha police force!
 
Wajameni sihitaji kuongelea sura ya mtu, Imani, rangi au ukanda, hapa nazungumzia weledi na hofu ya Mungu. Huyu bwana ana busara, mweledi, mwelewa, ana hofu ya Mungu na ni Mchapakazi.

Kutokana kama kashfa nzito zinazolikabili jeshi la polisi hivi sasa, ni kweli linahitaji mtu aina ya Salum Hamduni. Waswahili wanasema myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, huyu bwana anastahili nafasi hii. Uozo uliopo ndani ya Polisi unahitaji mtu makini na mfuatiliaji na siyo mpiga kelele tu.

IGP Siro siku zote tunasema ni Operational Officer na siyo National Leader, siyo mtu wa kufanya maamuzi ya kiuongozi ndiyo maana tunaona jeshi limemshinda, yeye alisikia tu kelele keshakimbia site na kupiga mikwara na kelele lakini mbinu za kumaliza tatizo hana. Hana mbinu za kisasa kulisimamia jeshi.

Mama ikimpendeza amteue Salum Hamduni kwenye nafasi hii, hanijui mimi kwa namna yeyote ile na wala simpigii promo lakini ninamfahamu kwa uchapa kazi wake.
Pole na kushindwa ramli. Amekuwa RAS
 
Viongozi wengi wa jeshi la Polisi kwasasa ni Waislam

Alhamdullilah
 
Back
Top Bottom