CP Salum Hamduni anastahili kuwa IGP Mpya

Mbona hujatupa wasifu wake kwa kina zaidi ya kumsifia tu
 
Simjui kwa undani Mkuu..Ila upole ni sura tu,nadhani huwa anajisimamia wakati mwingine,alikataa mchongo wa Sabaya wa kutaka kuwaundia tuhuma feki wafanyabiashara fulani,huko Kilimanjaro,akiwa RPC huko,tena enzi za mwendazake..' Nilisoma Uzi humu'..Wale wafanyabiashara walikataa kutoa ngawila Kwa Sabaya..
 
Wenye nchi yao watakupinga weeeeee,
Kisa watasema huyu mwarabu
Ila jamaa anafaa
 
Kama vp hata Kamanda wa kanda maalum bwana Jumanne
 
Tatizo la jeshi la polisi sio IGP kama mtu binafsi ila ni kwamba jeshi hilo limekuwa Heavily Politicized kiasi kwamba hata wamuweke nani kuwa bosi wake ni kazi bure.

Tusidanganyane, huyo bwana unayemfagilia akisikia kwamba wafuasi wa Chadema wamepigwa na kujeruhiwa sehemu unafikiri atachukua hatua yoyote si naye atameza pini tu kama ambavyo wamekuwa wakifanya watangulizi wake.

Hamna kitu hapo, tupate katiba mpya itakayotenganisha huduma za polisi "Police Services" na mambo ya siasa tofauti na hapo ni kudanganyana tu, tutabaki kufagilia watu kwa sababu za "Religious Ties" tu na vitu kama hivyo.
 
Hamduni huyuhuyu?
 
Huu ni uongo wa wazi, hamduni huyuhuyu aliyekua RPC Arusha??
 
Tunajua mnataka kumuondoa Nsiro kwa kuwa yeye hajali huyu ana cheo au la kama mnavyotaka. Sasa mtoeni tu na watoeni Mawaziri wote, manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya wawekeni watu wenu mzudi kufurahi maana mpaka sasa hamjaridhika!
 
Jeshi la Polisi ndiyo jeshi pekee linalotumiwa vibaya zaidi na wanasiasa. Amini, usiamini, hata kama mmoja wa malaika wa Mungu atashuka kuja kuwa IGP, bado Jeshi la Polisi litaendelea kuwa tatizo kwa Watanzania!
Mfumo wa kumpata mkuu wa polisi watakiwa kukarabatiwa.
Hapa kwetu wenye nyota (Commissioned Officers) ni uteuzi wa rais na hapo ndio siasa inapoingilia. Wenzetu Kenya baada ya kupata matatizo ya rushwa na ukabila kwa miaka mingi, wameanza utaratibu wa WAZI zaidi. Waombaji wanatuma maombi, wanachujwa na baadae kufanya interview ya WAZI kwa tume maalum. Mshindi ndio anateuliwa na Rais. KENYA’S NEW POLICE CHIEF APPOINTMENT - kenyaforum.net
Sasa wako mbioni kuanza hayo kwenye hatua ya County ambayo kwetu huku ni MKOA
 

Hiyo approach yao ni prescription ya issue moja tu: ukabila katika upatikanaji wa IGP. Issues zingine zote ziko pale pale. As long as chain of command ya police force inahusisha wanasiasa ndani yake, process nzuri ya kumpata IGP by itself haiwezi kuboresha police force!
 
Pole na kushindwa ramli. Amekuwa RAS
 
Viongozi wengi wa jeshi la Polisi kwasasa ni Waislam

Alhamdullilah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…