Crazy things you did in secondary school

Crazy things you did in secondary school

me niliingia f 5 akatokea mvulana flan hv akajifanya mjuaji akatuchora ubaoni wasichana kama wa5,wewee alijuta kunichora nilimsambazia kichapo kikali,,watuu had leo hua hawanielewi yani,c unajua mtu akiwa na kosa anakua mdogo,,,,,,kichapo hadi walikuja kuamulia f6,had leo huyo jamaa ananiheshim na shule nzima watu shiii af nikapewa uongozi nikawa nikisema kitu watu ndiooo?!!!


Bado unagawa kisago hadi leo?

Just being curious...lol!!
 
Kweli kabisa mkuu,

Kuwa wadau wengi sana, tena muhimu katika huu dunia ya MMU wamepotea sana....

Huyu Da Asha (@AshaDii) kapotea mno hadi anatia shaka. Kuna wadau wengine kama klorokwini, Nyamayao, WoS (@WomanOfSubstance)...na wengine kibao ambao naamini ni wazima ingawa kimya chao kinatia shaka.

Enzi hizo ilikuwa hatari kufungua JF kabla ya kuchapa kazi kwani uwezekano wa kukamatika ulikuwa mkubwa sana. Siku hizi hata ukifungua, bado utaondoka tu....Hakuna sumaku tena!

cc😡Mbu, The Boss, Fixed Point, gfsonwin, KOKUTONA, Preta, marejesho (huyu lazima nimfikishe kwa pilato ndani ya wk 2 zijazo), Blaki Womani, mwenyekiti PakaJimmy na wadau wengine kiboa.....!


Heshima yako babu yangu
 
Nilikuwa nikienda kupiga punyeto!najitayarisha kama naenda library na bweni lazima wajue!!!nabeba kikopo changu,sabuni na picha ya kunipa stimu demu kakaa kihasara ni ya porn! hiyo tulikuwa tunaazimana kwa kila mpiga nyeto!

Wapiga nyeto wote walikuwa na matege ya mikono...muda wote mikono imeelekea kwenye maungo ya siri kama ubanio wa kusongea ugali vile
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!

Mkuu Hii Akili Yako Ni Kama Wa Iyunga Boys Mbeya
 
Daaah,
Miaka hiyooo;
Shule ya msingi, wakati tunarudi home mvulana mmoja alikuwa na tabia ya kutembea na kioo ile mmezubaa njiani mnaongea, kidogo tu unakuta kaweka kioo chini wavulana wanachungulia kama umevaa chup.i.

Siku aliniwekea, bahati nilivaa chup.i ya kitambaa cha jinja, nikasikia wanasema amevaa, loooh.
............. hii ni moja tu, sekondari? chuo? nitarudi tena.
 
Hii koment imenichekesha sana, Mamndenyi kwa nini umeniita huku?

nakumbuka nikiwa la std 7, afu ndo nilikuwa kati ya top 5 wanaotegemewa kubeba bendera ya shule.

Tukafanya mitihani, nikapata inglish 16% walimu walipagawa wakaniita ofisini wananishambulia wanataka kunichapa. Ile kuniuliza nimepatwa na nini.

Nikawajibu, Nimerogwa.

Ilibidi waniache maana nilikuwa nalia kama mfiwa.
 
Last edited by a moderator:
Mie hii ilinifanya nikahama fasta, nilikuwa siielewi elewi, ilikaa ni lesbian zaidi.

Kurudi home likizo nikamwambia mzee, bora simba ile mimi, si samaki aisee. Nikapelekwa shule mchanganyiko, na huko ndio nilijifunza 'escape from sobibo'. Girls pekee ningekuwa mzembe sana.

Ila, ***** wale mabinti, bahati walinikuta nna akili za kujiongeza tu, ila sijui kama winfrida alitoka akiwa mtu tena, kama waliendelea vile?

unakumbuka kuwa na vijembe......unakuwa na ukoo hapo shule ambao mnaheshimiana kama unavyoheshimu wazazi wako na pengine hata zaidi ya siblings wako. Unakuwa na mtoto, mama, bibi, aunt and so on.
 
Thread imenifanya nimecheka..

Mie changu kituko nilikua na tabia ya kutoroka jioni na mabest kwenda kula chips..sasa kule kuna baridi vibaya inabidi kuvaa suruali ya track ndani na sketi ya shule juu....ile tumetoka tukashauriana tukatafute kwanza matunda..eneo limejaaliwa matunda hatari.

tukachuma peaches jaza kwenye makoti kwenye suruali ilimradi tumebeba...ile tumechomoza barabarani tu mkuu wa shule huyu hapa...na alitufahamu kutokana na mie nilikua binti mrefu zaidi kwa hivyo alishanikariri...aisee alitukimbiza sitosahau...nikakimbilia kwenye kijumba hakijakamilika vichaka kibao.

hapo kiza kimetanda! Mara mtu akapiga simu kimlio cha motorola aisee..nilitoa betri kama mwendawazimu

nikapita njia ambayo siikumbuki mpaka leo nikajikuta bwenini dkk 5 mkuu huyo akaitisha rollcall....hapo nikabadili nguo nikaenda.

Sitosahau ile siku kwa kweli..
 
Me nakumbuka shule as girls school kuna kaugonjwa kakucheka cheka, basi kipindi hicho sijui tulikua hatujawekewa mafuta ya taa???

Basi tukaanza kucheka hahahaaaa uuuuuuuuuu!!!!! Basi darasa hadi darasa yani likitoka hili wanapokea hawa,,walimu wakaja darasani kwetu wameingia tu, tukaangua kicheko weee majanga wakasema tunawacheka wao, tulisambaziwa kichapo jamani huku tunacheka bado unachapwa huku unachapwa,

tukatolewa nje kwenye jua kupiga magot bad tunaangu kichek balaa tulichapw had nikalazw hospital wik nzim sijielewi.
 
Siku ya Graduation pale Mazengo Sec mwaka 1985, kiongozi wa sherehe alikuwa mshikaji wangu Kasanga. Basi nilimfuata na Kisadolini changu na akanijazia Pilau.

Pilau la Mazengo miaka hiyo lilikuwa kali sana. Kwa wenyeji wa Dodoma watakuwa wanamkumbuka Mzee Mapilau na yale Mapipa yake (SHABA). Nilikula siku hiyo hadi nikawa siwezi kuhema. Jamaa walishangaa kuwa mbona hawaoni tumbo kutokea. Basi kutoka siku hiyo nikajulikana kuwa nina tumbo kama la Mamba, linafutuka pembeni.......

Upuuzi wa Mazengo ilikuwa ni chooni. Utakuta mtu anapita koridoni na karatasi yake anaipekecha ili ilainike.... "pyeke pyeke pyeke..." na akitoka huko basi anapita kwenye ule mti nyuma ya bweni la Mwongozo na kujipigapiga na mtawi. Hii ilikuwa inasaidia kuuwa ile perfume uliyoikwaa kule NYUMBA KUBWA. Ule mti ulikuwa na harufu moja kali sana na ukitoka hapo unanukia freshi. Mabinti wa Msalato, mlivumiliaje ile harufu??

Mkuu umenikumbusha mbali mno japo mie sijasoma miaka hiyo. Nyuma ya mwongozo ule mti ulikuwa mpilipili manga na pembeni kiwanja cha Basketball.

Na jikoni sisi alikuwa mzee Shed ambaye akimuona jamaa wa kugawa maharage anampa mtu vijiko viwili (kijiko ukubwa wake kama nusu nazi ama kifuu) anapewa vibao vya maana kwakuwa anamaliza ma beans.
 
Hahahaa, Mzee Shedi na Chonya wake hahahhaaa. Utasikia wanawaambiwa "Mpishi, chikulomba Malenga" na wao wanajibu "Malenga msina." Hapo ni kuwa Maji hakuna. Au unasikia "Chikulomba Ukoko...."

Mhhh, hata ukoko hawatoi vilevile. Ile shule ilikuwa nzuri sana kama unataka kusoma pamoja na shida zake zote.

Mkuu umenikumbusha mbali mno japo mie sijasoma miaka hiyo. Nyuma ya mwongozo ule mti ulikuwa mpilipili manga na pembeni kiwanja cha Basketball. Na jikoni sisi alikuwa mzee Shed ambaye akimuona jamaa wa kugawa maharage anampa mtu vijiko viwili (kijiko ukubwa wake kama nusu nazi ama kifuu) anapewa vibao vya maana kwakuwa anamaliza ma beans.
 
nakumbuka nikiwa kibaha sekondari nilifumwa gizani naimbisha mtoto wa mwalimu wacha kabisa second master alinipa kipondo heavy hadi nilisinzia

kipondo cha mtongozano lusungo ulikipata very late..........

nakumbuka darasa la tano primary nilipokea stiki za kutosha mbele ya class kisa niliandika barua ya kumuimbiza wifi yake ticha wangu wa kiswahili............ siwezi kusahau maana hata papuchi sikula aseeeeh!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Asee nilikuwa std 6 siku hiyo nikaenda shule nimevaa malapa zile ndala kabisa za kuogea
kama zali Mwl. Mkuu akaniita kwa ishu zingine tu si nikaenda nachechemea nkajifanya nna kidonda
akanituma nimuite dogo mwingine sijui mtego nikaondoka natembea kawaida nkasahau kuchechemea kumbe kashtukia
mweh naulizwa umeumia wapi? Nkabaki natoa macho tu nilipigwa stiki 15 pale pale

.....Na leo wewe ni mwalimu.
 
Back
Top Bottom