Leo nimeenda kwenye moja ya ATM za CRDB Bank nikiwa na nia ya kutoa fedha kiasi cha 200k+. baada ya majaribio kadhaa ya kujaribu kutoa kiasi hicho ambacho nilikuwa na uhakika ninacho kwenye akaunti kushindikana ikabidi niangalie salio, sikuamini baada ya kukuta kiasi cha Tshs. 96,280.
Kimekatwa kwenye akaunti yangu bila mimi mwenyewe kujua. Nimepiga simu call centre yao majibu niliyopewa eti fedha ilikatwa tarehe 31.12.2024 kwa miamala ambayo nimekuwa nikifanya mfano kutoa kwenye ATM ambayo siyo ya crdb na kusafiri nje ya Nchi kitu ambacho sijawahi kufanya.
Nauchukulia huu kama wizi kwasababu Statement inaonesha miamala ambayo imefanyika tarehe hiyo na mimi sikufanya miamala hiyo kwa siku hiyo ambayo jumla yake ni Tshs. 96,280. Screen shot imeambatishwa.