Mimi Nilifunga account kwa ajili ya huo ujinga wao.. Ninashangaa sana watu wanaopata huduma katika bank hii.
Nashawishika kuamini kuwa mkuu hujatuambia kila kitu kuhusu ugumu ulioupata. Naamini hivi kwasababu kama muda wa kupewa cheque book ni week moja hadi mbili, haiwezekani miezi mitatu ipite halafu usipewe sababu ya kutopewa kwa muda wote huo. Kwangu mie kuambiwa tu bado haijatoka hiyo sio sababu. Naamini kuna kitu/sababu/requirement wamekuambia ambacho hujaisema hapa. Isikute kuna requirement wanataka ukamilishe na wewe ndo hujakamilisha. Hebu funguka zaidi.
Hilo libenk kwa nje huwa linajitangaza sana...lakini kwa ndani lina uozo sana...
Nenda barclays,they ar so systematic,au nipm
nataka mastercard / visa card ya hawa jamaa ila nasikia gharama zake juu sana...
kwa sasa natumia ya CRDB inafanya kazi sana ughaibuni ila kipindi kama cha miezi mitatu ilianza kusumbua mpaka kero
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.
Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.
Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.
Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?
Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.
Nimezunguka benki nyingi lakini hadi sasa nimeamua kutulia na Azania bank maana sijawahi kupata tatizo.
Kitabu cha hundi ni nini? Inaitwaje kwa kiinglish labda ntaelewa..au ndo hawala ya fedha?
Karibu sana mdau
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.
we pia mzugaji ulichukua hatua gani baada ya kuona cheque book yako inachelewa je ulienda kumwona manager ukamwelezea tatizo lako jamaa wako poa huwezi linganisha na bank yoyote hapa ya kibongo adress tatizo lako sehemu sahihi wafanyakazi sio malaika mmoja mmoja anaweza kosea