CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

Mimi Nilifunga account kwa ajili ya huo ujinga wao.. Ninashangaa sana watu wanaopata huduma katika bank hii.

Mkuu unajua bana mifumo ya bank zetu za kibongo ni yakizamani sana na inakuwa shida sana kama bank ishakuwa na wateja wengi sababu mambo mengi ya centralized
So kama wewe ni mtumiaji mkubwa wa mabank huwezi kuzikwepa hizi bank kubwa, lakini kama ni mtumiaji wa kawaida nashauri fungua bank hizi mpya ndogo ndogo huduma zake ziko fasta kuliko maelezo na utahudumiwa kama mfalme, tatizo ni wanamitandao midogo wengi wanaoperate dsm tu
 
Kitabu cha hundi ni nini? Inaitwaje kwa kiinglish labda ntaelewa..au ndo hawala ya fedha?
 
Nashawishika kuamini kuwa mkuu hujatuambia kila kitu kuhusu ugumu ulioupata. Naamini hivi kwasababu kama muda wa kupewa cheque book ni week moja hadi mbili, haiwezekani miezi mitatu ipite halafu usipewe sababu ya kutopewa kwa muda wote huo. Kwangu mie kuambiwa tu bado haijatoka hiyo sio sababu. Naamini kuna kitu/sababu/requirement wamekuambia ambacho hujaisema hapa. Isikute kuna requirement wanataka ukamilishe na wewe ndo hujakamilisha. Hebu funguka zaidi.
 
Nashawishika kuamini kuwa mkuu hujatuambia kila kitu kuhusu ugumu ulioupata. Naamini hivi kwasababu kama muda wa kupewa cheque book ni week moja hadi mbili, haiwezekani miezi mitatu ipite halafu usipewe sababu ya kutopewa kwa muda wote huo. Kwangu mie kuambiwa tu bado haijatoka hiyo sio sababu. Naamini kuna kitu/sababu/requirement wamekuambia ambacho hujaisema hapa. Isikute kuna requirement wanataka ukamilishe na wewe ndo hujakamilisha. Hebu funguka zaidi.

Nilipofungua accounts nilipewa check list ya mahitaji ninayotakiwa kutimiza ili wafungue account, nilitimiza mahitaji yao yote ikiwa ni deposit ya fedha kwa account ya fixed deposit na fedha ya kitabu cha hundi. Niliahidiwa ningepata kitabu baada ya wiki mbili badala ya wiki moja kwa sababu kulikuwepo na tatizo la mashine ya kutengeneza hundi.

Waliniahidi wangenifahamisha kwa njia ya SMS mara kitabu kitakapokuwa tayari. Accounts yangu haina tatizo lolote kwani ninafanya deposit kama kawaida. Nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara lakini jibu lao ni kuwa bado vitabu vya hundi kwa wateja wengi havijatoka makao makuu ya benk, leo ikiwa imetimia mwiezi mitatu ya kusubiria bila ya mafanikio yeyote, badala ya wiki mbili.
 
Nenda barclays,they ar so systematic,au nipm

nataka mastercard / visa card ya hawa jamaa ila nasikia gharama zake juu sana...

kwa sasa natumia ya CRDB inafanya kazi sana ughaibuni ila kipindi kama cha miezi mitatu ilianza kusumbua mpaka kero
 
tatizo nililowahi kukutana nalo ni la kulipia Online kwa Visa au masta card kwakweli inasumbua na kila mwezi inabidi unafanye activation ya Card na wanasumbua sana hasa tawi la Chuo Kikuu Dsm huduma zao kimeo
 
nataka mastercard / visa card ya hawa jamaa ila nasikia gharama zake juu sana...

kwa sasa natumia ya CRDB inafanya kazi sana ughaibuni ila kipindi kama cha miezi mitatu ilianza kusumbua mpaka kero

Wabongo weng hatuna elimu ya banking,kiukweli gharama ya barclays sio kubwa watu wanasema hivyo coz wanakatwa at once. Watanzania wamezoea kukatwa kidogo kidogo ila barclays wanafixed amount ambayo inakatwa mwisho wa mwez then unaenjoy service nyingine bila kukatwa chochote. Mfano kuchukua hela kwenye atm,internet banking,kuuliza salio,ordering cheque book etc
 
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.

Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.

Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.

Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?

Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.

Wenzako tunakimbilia CRDB wewe unatokomea, hayaya nenda NMB au NBC maana ndizo zenye mtandao mkubwa.
 
kimsingi benki ya CRDB iko na unafuu kulinganisha na benki zingine hapa nyumbani, huduma yao kwa wateja inadorora siku hadi siku hii ni kwa sababu wanawekeza zaidi kwenye tv na radio advertisement, hii haiwezi kulipa kama existing customers wanaponda huduma wanasahau kuinvest kwenye customer service yaani kuna watu hawastahili kukaa kaunta hawajui kusalimia wala kukaribisha wateja, mteja anajikaribisha, kuhudumiwa mpaka apige makelele kaunta, cashiers wanatoa lugha chafu kwa wateja. naishauri hii benki counter na cash wakae happy staffs, benki iko bize inatafuta wateja wapya kwa matangazo wakati waliopo inashindwa kuwahudumia, kwa nini uende porini kutafuta matunda pori wakati nyumbani kwako una apple tree yenye low hanging fruits, wape huduma nzuri wateja waliopo watakuletea wateja wengi zaidi mr KIMEI.
 
Mkuu pole sana. Nadhani wamekusikia na watajirekebisha. Kwa maoni yangu nadhani CRDB bado ni benki wanaojitahidi kutoa huduma kulinganisha na mabenki mengine hapa nchini. Japo si jambo la kawaida ni vema umwone mkuu wa idara au meneja umweleze issue yako.Mimi ni mteja wao tangu 2002 kuna changamoto kweli lakini zisikufanye ukate tama.
 
Karibu sana mdau

Asante mkuu,napaheshimu sababu nilikuwa na hitaji huduma flani pale Azania Samora Avenue kuna jamaa anaitwa Godwin alinihudumia kiungwana tena kwa haraka kitu ambacho sijazoea benki nyingine tena bila kutaka chochote!!! Kiukweli nikawa very impressed maana huko kwingine unatanguliza kabisa mlungula ili upate huduma kwa wakati.
 
Mimi nilifunga account yangu CRDB nikaambiwa nirudishe card yao kisha nitaopewa hela ya kitabu. NAKWNDA NA CARD YANGU WAKANIMBIA HELA KWENYE ACCOUNT YAKO IMEFIDIWA KWENYE HIZI GHARAMA ZA CARD ZAKO. JAMANI NILISIKITISHWA SANA NA USHENZI HUU NIKASEMA SIENDI POPOTE NIKAMWAMBIA YUHO DADA NAMWACHIA MUNGUKWA HIYO KIUKWELI CRDB BANK KUNA ADHA FULANI AMBAYO INAKATISHA TAMMANAKUSHAURI NENDA STANDARD CHARTERED BANK TANGU NIJUINGE NAO SIJAPATA USUMBUFU JAPO SINA HATA MWAKA NAO MPAKA SASANI USHAURI TU PENGINE WENGINE WATASEMA ADHA ZAO WALIZOKUTANA NAZO
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.
 
Pole mkuu kwa usumbufu but usikae kimya nenda kwa BRANCH MANAGER umuulize (Acha woga wa Kitanzania). uliposema CRDB ukanikumbusha siku moja nilienda CRDB AGENCY MABIBO HOSTEL NDANI tukiwa kwenye foleni teller (wa kiume) akawa ana maongezi marefuu na binti (mteja) tulikaa kumsubiri "mteja" huyo kama 25 minutes kusema ukweli ikabidi nimfuate yule Teller kumuuliza kulikoni mbona tumekaa sana bila wateja wengine kuhudumiwa? aaah!! Teller akanijibu mbovu daah hapo ndipo alipoibua Hasira zangu nkamuambia kama hawez kuhudumia wateja kwa haraka ni bora akakae nyumbani, nilichafua hali ya hewa pale benki maana nilimuwakia kiasi kwamba Manager akatoka ofisini kuja kutuliza... na samahani kibao. hawa jamaa bila kuwa mkali watakuendesha ka baiskeli ya miti. Siku hizi nikienda pale huduma ni Fasta.
 
we pia mzugaji ulichukua hatua gani baada ya kuona cheque book yako inachelewa je ulienda kumwona manager ukamwelezea tatizo lako jamaa wako poa huwezi linganisha na bank yoyote hapa ya kibongo adress tatizo lako sehemu sahihi wafanyakazi sio malaika mmoja mmoja anaweza kosea

amweshakwambia akitaka kuchukua hela lazima manager apitishe kwanza...which means manager yupo well informed na comfortable ...CRDB is badnews ndugu yangu.....hata ATMs zao huwa ni msiba tu hasa siku za weekend!
 
Back
Top Bottom