CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

...... a place that is u will not miss a chagga.
 
Eti siku moja kadi imemezwa saa 4 asubuhi pale CRDB TRA branch Arusha wakaniambia ni mpaka kesho yake ilihali nilikuwa nasafiri. Ilibidi niweke high frequency(majibizano makali) then mkuu wao pale akaagiza nikaletewa kadi. pale nikagundua kila mtu ni Kimei pale
 
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.

Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.

Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.

Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?

Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.



pole sana kwa mabenki aya ya kibongo, ila kiukweli iyo benki ina wafanyakazi friendly sijaona benki zingine...kuna wakati nlienda NBC kulipa karo ya mtoto ila nlikaa foleni kama masaa2 alaf foleni ina watu kama 7 -10 tu , nimekaribia mtu wa 2 kufika , cashier kafunga na kuondoka ,then kama robo saa ndo karudi, yani sijawai kuona benki nyingine kwa kweli. Mfano unaweza kwenda Exim hata dakika 10 kwenye foleni haifiki, uwa nafaidi sana uku, though najua ni kwa kuwa wana wateja wachache ila raha sana. Crdb kwa foleni wanajitaidi ila kwa mikoani kiukweli wanajitaidi yani unaweza kukuta cashier ana foleni mpaka mlangoni ila haichukui nusu saa, unafika kwa cashier....wana madirisha meeeengi ila teller ni 2, ajabu sana. Sijui kwa nini hawakubali kuajiri wakti vijana mtaani hawana kazi...alaf na kimei ajiangalie bhana, yani yeye naskikia mshahara mnono ila staff wake wanacheza na laki 8, 9 per month, sijui kwa maisha ya sasa iyo lak8 pamoja na makato na mikopo mtu anaishije jamani, kimei ukipita uku fanyia kazi iyo kitu,usibane kivile alaf kwenye magazeti mnasema mmepata faida bilioni 100 wakati wafanyakzi wako wanalia njaa.
 
Eti siku moja kadi imemezwa saa 4 asubuhi pale CRDB TRA branch Arusha wakaniambia ni mpaka kesho yake ilihali nilikuwa nasafiri. Ilibidi niweke high frequency(majibizano makali) then mkuu wao pale akaagiza nikaletewa kadi. pale nikagundua kila mtu ni Kimei pale

mvumbuzi ,nijuavyo kuna utaratibu wa kibenki kuwa kadi ikinasa kuna muda wa kuitoa,sasa kama Manager aliamuru itolewe kwenye machine ni kuwa ulimsaidia meneja kuvunja kanuni za benki ila si kuwa ulikuwa na haki...ilishanikuta uku dar city centre nami nikahoji ila waliniletea kanuni ya benki kuwa ATM itafunguliwa mara moja kwa siku au mara mbili kama itakuwa karibu na tawi,ujue hawasemagi kila kitu ila kuna utartibu unawaguide....Pia umesema pale TRA dah kumbe tunatofautioana, yani nikiendaga arusha watu wangu wananiambiaga ukitaka huduma ya fasta nenda pale TRA,kweli pale jamaa wako active ila duh, ka jengo kanajaa alaf hakuna hewa pale, usiombe kwenda siku za kulipa kodi , utakoma pale kwa foleni...Kiukweli kwa arusha hakuna sehemu wafanyakazi wa CRDB wako active na upendo kama pale,yani si cashier si bosi woote utakuta wana furaha,very active,yani vizuri...Tatizo kama unatoa pesa nyingi kama sisi ukitoka mkoa mwigine duh urasimu huo wa ajabu sana, eti mpaka wapate authority ulikofungulia akaunti as if ela ni benki na umeweka mwenyewe. Pale TRA pazuri bhana mi nawapa big up,sijui wanawachaguaje, yani wa pale tofauti kabisa na CRDB kwingine kote....
 
"The Bank that Listens".....wanaenda kinyume kabisa na slogan yao:disapointed:
 
Crdb ni benki bora ya Kitanzania haina ubishi. Haya mambo mengine ni chuki tu na tusipokuwa waangalfu litagawanya Tanganyika tarajiwa
 
ATM masasi bomu kabisa mwisho kuchukua pesa ni jioni,usiku au alfajiri kadi inazama,sasa hivi kadi yangu imezama ningekuwa na uwezo ningeivunjavunja hii ATM kwa shoka,pesa yangu dili langu limevurugika!!!nafikiria kuhama.
 
Back
Top Bottom