CRDB Iringa- Kwa wizi huu mmezidi sasa!!

CRDB Iringa- Kwa wizi huu mmezidi sasa!!

Song'ito

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
348
Reaction score
147
Wandugu mimi ni mfanyakazi wa taasisi moja binafsi hapa iringa, kuna mishahara ya wafanyakazi inapitia bank ya CRDB Iringa branch... Mishahara ya mwezi huu imeingia ila watu karibu 9 wamekuta account nyeupe kabisaaaa tena kwa mpigo. Kwenda kufuatilia wanaambiwa wamechukua hela eti visiwa vya shelisheli na wengine msumbiji... wakati hawajawahi kwenda hizo sehemu!! Katika kufuatilia bank inasema eti wasubiri 45 days wanachunguza kuna nini kimetokea, ila majibu rahisi ya mwanzo ni kuwa wameibiwa kwa nia za mtandao...
Mi nadhani kuna wafanyakazi crdb sio waaminifu hasa upande wa IT ambao wanacheza na system... ambapo kazi inabidi ifanyike kuwabaini... Wafanyakazi zaidi ya 30 wanaazimia kufunga account zao huko....
Nasema this is too much...
 
Poleni sana! Duhhh.... Benki itawalipa. Nasikitika kwa kuwa itakuwa hasara kwa Benki
 
Vijana wengi graduates wanaajiriwa kwenye Benki, wanapata tamaa za kuwa na magari na kunywa bia kwenye starehe ila vijimishahara vyao ni vidogo hivyo wanakuwa wezi tu.
 
Tatizo inawezekana pia ni aina ya mfumo unaotumiwa na benki hiyo na nyinginezo kwani teknolojia katika mabenki hayo ni ile iliyo kwisha tumika ulaya hivyo ni mitumba na waliokwisha itumia inakuwa rahisi kwao kutemper na kuiba kwa urahisi hasa kupita ATM.
 
Poleni sana! Duhhh.... Benki itawalipa. Nasikitika kwa kuwa itakuwa hasara kwa Benki
sijui kama watalipa mana wakati wafanyakazi wanafatilia hayo, wamekuta mzee mmoja mwezi wa pili huu nae anafatilia hilo hilo... nae walichomoa hela zake zoote
 
Vijana wengi graduates wanaajiriwa kwenye Benki, wanapata tamaa za kuwa na magari na kunywa bia kwenye starehe ila vijimishahara vyao ni vidogo hivyo wanakuwa wezi tu.
usemalo ni kweli mkuu... shida ni kuwa wanataka kutajilika kupitia migongo ya wavuja jasho wengine!!
 
Tatizo inawezekana pia ni aina ya mfumo unaotumiwa na benki hiyo na nyinginezo kwani teknolojia katika mabenki hayo ni ile iliyo kwisha tumika ulaya hivyo ni mitumba na waliokwisha itumia inakuwa rahisi kwao kutemper na kuiba kwa urahisi hasa kupita ATM.
aisiii hii inawezekana kweli....
 
Vijana wengi graduates wanaajiriwa kwenye Benki, wanapata tamaa za kuwa na magari na kunywa bia kwenye starehe ila vijimishahara vyao ni vidogo hivyo wanakuwa wezi tu.

Naunga mkono hoja tena ukiwakuta bar,wanaendesha magari kama hawana shida kumbe wanakula pesa za watu.
 
Mfumo wa mabenki karibu yote yanavisa mfano CRDB,NMB,NBC kute kumetokea matukio ya wateja fedha zao kuchukuliwa ktk utata. Kwa utaratibu huu lazima turudi kuhifadhi fedha kwenye vibubu,makopo,kuchimbia ardhini na sehemu tofauti na benki. Wakishindwa kurudisha fungueni kesi watu wanavuja jasho wao wanataka kula kiulaini haiwezekani.
 
songíto;4946410 said:
wandugu mimi ni mfanyakazi wa taasisi moja binafsi hapa iringa, kuna mishahara ya wafanyakazi inapitia bank ya crdb iringa branch... Mishahara ya mwezi huu imeingia ila watu karibu 9 wamekuta account nyeupe kabisaaaa tena kwa mpigo. Kwenda kufuatilia wanaambiwa wamechukua hela eti visiwa vya shelisheli na wengine msumbiji... Wakati hawajawahi kwenda hizo sehemu!! Katika kufuatilia bank inasema eti wasubiri 45 days wanachunguza kuna nini kimetokea, ila majibu rahisi ya mwanzo ni kuwa wameibiwa kwa nia za mtandao...
Mi nadhani kuna wafanyakazi crdb sio waaminifu hasa upande wa it ambao wanacheza na system... Ambapo kazi inabidi ifanyike kuwabaini... Wafanyakazi zaidi ya 30 wanaazimia kufunga account zao huko....
Nasema this is too much...

warning: Unapoagiza kadi mpya kuna software ziko sokoni, ambazo wanatumiya computer kuscan hizo kadi mpya na kufanya duplicate ya kadi yako, na kwavile watakuwa na namba yako ya siri, ni rahisi sana kufanya hujuma kwenye account yako muda wowote. Hii ni kwa dunia nzima. Wizi utokea kwenye kuagiza kadi yako kabla ya kukupa utoa duplicate.
 
Iringa bwana si unajua miaka kama ya 2009 Barclays Bank nayo wafanyakazi wake branch ya Iringa mjini waliipiga michuzi ya kutosha wakapelekwa rumande then wakatolewa kwa dhamana mpaka leo wapo mtaani wanadunda na maprado ya nguvu
 
Songíto;4946410 said:
Wandugu mimi ni mfanyakazi wa taasisi moja binafsi hapa iringa, kuna mishahara ya wafanyakazi inapitia bank ya CRDB Iringa branch... Mishahara ya mwezi huu imeingia ila watu karibu 9 wamekuta account nyeupe kabisaaaa tena kwa mpigo. Kwenda kufuatilia wanaambiwa wamechukua hela eti visiwa vya shelisheli na wengine msumbiji... wakati hawajawahi kwenda hizo sehemu!! Katika kufuatilia bank inasema eti wasubiri 45 days wanachunguza kuna nini kimetokea, ila majibu rahisi ya mwanzo ni kuwa wameibiwa kwa nia za mtandao...
Mi nadhani kuna wafanyakazi crdb sio waaminifu hasa upande wa IT ambao wanacheza na system... ambapo kazi inabidi ifanyike kuwabaini... Wafanyakazi zaidi ya 30 wanaazimia kufunga account zao huko....
Nasema this is too much...
Kaka poleni! Hiyo ni Hasara kwa Bank after investigation inayochukua 45 days watarudishiwa but ni vzuri kufuatilia from time to time, nami ilishanitokea CRDB ilichukua zaidi ya miezi miwili hela kurudishwa.
 
mie niko bank though siyo crdb wat i know ni kwamba kuna wizi mkali sana unaoendelea sasa hivi katika ATM zetu kuna vifaa ambavyo jamaa(matapeli) wanafunga kwenye atm ambacho kina detect number za siri, za mteja na hivyo kuwawezesha kutengeneza za kwao na kuja kupiga hela. swala la siku 45 ni sahihi kabisa maana kumrefund mteja ni swala ambalo watakiwa kujihakiki sana. coz siyo kila anae claim ni kweli kaibiwa wengine ni janja janja tuu. so poleni sana.
 
dunia si salama kadri siku zinavyozidi kwenda na maendeleo yanavyozidi kuja.
 
mie niko bank though siyo crdb wat i know ni kwamba kuna wizi mkali sana unaoendelea sasa hivi katika ATM zetu kuna vifaa ambavyo jamaa(matapeli) wanafunga kwenye atm ambacho kina detect number za siri, za mteja na hivyo kuwawezesha kutengeneza za kwao na kuja kupiga hela. swala la siku 45 ni sahihi kabisa maana kumrefund mteja ni swala ambalo watakiwa kujihakiki sana. coz siyo kila anae claim ni kweli kaibiwa wengine ni janja janja tuu. so poleni sana.

KIMAROO wewe kama sio mchaga basi mpare....tena uko benki....MUNGU TUHURUMIE tuhela twetu katika mikono ya hawa majamaa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom