CRDB kuondoa Salary advance imekaaje?

CRDB kuondoa Salary advance imekaaje?

Chonde chonde CRDB msitufanyie hivyo. Mnatuaibisha tulishaanza kunywa bia toka jana sasa leo kuondoa salary advance ndio nn?

Fanyeni mambo basi tunawaaminia.

Yaani unalipa alaf fasta unakopa[emoji23][emoji23][emoji23]
Lakini menu wamebadilisha nilitumiwa meseji jana kwahyo angalia vizuri. Ingia kwenye menu yao cheki Option Na. 5 ndio kuna mikopo hapo
IMG_1242.jpg
 
Mkuu kama hutajali, hapa mnamaanisha kitu gani? Yani unapata mshahara afu unapewa advance ya nini?
Mkuu. Yaani tufanye Mshahara wako unaingia Tar 25 February. Sasa Ukishaingia unaweza kukopa Mshahara wa mwezi March asilimia kadhaa. Sasa ikifika Tarehe 25 March Bank watakata ile uliokopa na viasilikia kidogo na kitakachobaki wanakupa.

Tatizo ukisha anza huu mchenzo ndio basi tena.
 
Shukrani kwa ufafanuzi kiongozi.

Nimeelewa.

Kweli hako ni kamchezo hatari . Ukishakaanza ni vigumu sana kukaacha. Siku ukitaka kukaacha njaa itakusuta.
 
Back
Top Bottom