CRDB mmefanya kibaguzi haiwezekani Zanzibar mtoa mikopo isiyo na riba,Tz bara mikopo iwe na riba

Crdb bank wa ajipendekeza kwa Dr. Mwinyi.
Ikukwe hata kipindi cha JPM walikuwa wanajipendekeza mpaka wakafungua brach kubwa sana Chato.
Hii imekaaje wadau naona imekaa kibaguzi sana,ina maana sisi Tanzania bara hatuna uhitaji na hiyo mikopo au? Zanzibar ni wa muhimu sana kwenu kuliko sisi? Au Zanzibar ni masikini sana mmeamua kuwapa upendeleo?
Kila siku wajasiriamali wanalia kuhusu riba lakini mmeweka pamba masikio.
Kama swala ni imani kuwa hakuna riba bhasi kaeni hivyo hivyo bila kufungamana na upande wowote
View attachment 2118030
View attachment 2118031
 
Kwamba crdb inashirikiana na serikali ya mapinduzi znz kutoa Mikopo isiyo na riba... Maana yake serikali ndo inatoa 'ruzuku' kwa kulipa riba za hiyo Mikopo ya crdb.

Program hiyo itanufaisha wazanzibar zaidi ya laki 7, maana'ake ni zaidi ya nusu ya wazanzibar wote watanufaika.

Si ajabu fedha inayotumika kwenye program hiyo ni ya Tanganyika
Si ndio ile migao ya mabilioni..ambayo bi tozo yupo ufaransa kuomba mingine ili mgao uendee tena jambiani..

Kwahi juzi hujasikia wajambiani wanasambaziwa umeme bure.

Soon utasikia maji bure..elimu hadi chuo kikuu bure.

Wazee wa chako changu..changu changu.

Mikopo wanataka ila kulipa watalipa wa Tanganyika.

Yana mwisho wake.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
Bank zipi?wewe mchamba wima..jidanganye..hakuna kitu kama hicho sio kwenye banki..yani ukope milion 3 uripe milioni 3...jidanganye.

RIBA wanaita FAIDA.
Mfano unataka kopa 10mil ununue gari IST ulipe 14mill. Wanachofanya wanakununulia IST kwa 10mill badala ya kukupa hela. Kisha wanaweka FAIDA yao 4mill. We we utalipa 14mill.
Kitu kilekile tofauti maneno.
 
Kama shida yako ni fedha taslimu, ukikopa tsh 10m cash, utarejesha ngapi?
 
Waongo tu hao..na wanafiki watupu..eti islamic bank hakuna riba?..thubutu uone..PBZ riba kama zote...hizi dini kwa unafiki zimejariwa.

Shetani hanaga rafiki..watakulima riba mpaka uchanganyikiwe.

#MaendeleoHayanaChama
riba ipo kama kawaida
sema wamebadilisha neno riba
wanasema ukikopa ukafanya mradi mnagawana faida na benki,
benki zinajiendesha kwa riba
wao wamebadilisha jina la riba
kuwa faida.
 
Crdb bank wa ajipendekeza kwa Dr. Mwinyi.
Ikukwe hata kipindi cha JPM walikuwa wanajipendekeza mpaka wakafungua brach kubwa sana Chato.
Crdb mbona imeanza muda mrefu chato, hata kabla Magufuli hajawa raisi.
Crdb chato ipo toka 2009. Au ulitaka kusemaje?
 
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
Umeeleweka vizuri
Nahisi uislam unachangia wao
Kupata mkopo bila riba huko

Ova
 
Kw
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
Kwa hiyo wafanyakazi wa benki isiyotoza riba yoyote wanalipwa kwa fungu gani?
 
Yaani anakopa 2M anarudisha 2M? Hebu nifahamisheni kwa mifano.
Riba ipo inabadilishwa jina tu. wanachofanya bank nyingi hizi wanaojifanya wanatumia jina la islamic bank nakupa mfano mdogo, wewe unataka kununua gari million moja bank za kawaida unaenda unanunua na unalipa 1.2 million mfano hapo kama 20% huko kwenye bank za dini wanasema ok unataka gari linauzwa million 1 sisi tunalilinunua halafu tunakuuzia 1.2 million kwa uhalisia na yale yale ila unashawishiwa hii sio sawa hii sawa. Utapeli kila sehemu riba ipo tu ni style tu kama rushwa na facilitation hata kwenye ma hospital yetu ukitaka kukaa foleni lipa alfu 10 ukitaka haraka lipa alfu 20 ndio rushwa za kisasa zamani ukifika unampa muuguzi alfu 20 uitwe haraka siku hizi unazilipa rasmi tu.
 
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
Kumbe ila ingekuwa ni takwa la upande wa pili ungesikia wameanza chokochoko za kidini.Kuna nguvu ya ibilisi ktk hili kiasi kwamba inakuwa vigumu ku-neutralize.
 
RIBA wanaita FAIDA.
Mfano unataka kopa 10mil ununue gari IST ulipe 14mill. Wanachofanya wanakununulia IST kwa 10mill badala ya kukupa hela. Kisha wanaweka FAIDA yao 4mill. We we utalipa 14mill.
Kitu kilekile tofauti maneno.
Kuna mazuzu yanadai eti hakuna riba.

#MaendeleoHayanaChama
 
Riba ipo inabadilishwa jina tu. wanachofanya bank nyingi hizi wanaojifanya wanatumia jina la islamic bank nakupa mfano mdogo, wewe unataka kununua gari million moja bank za kawaida unaenda unanunua na unalipa 1.2 million mfano hapo kama 20% huko kwenye bank za dini wanasema ok unataka gari linauzwa million 1 sisi tunalilinunua halafu tunakuuzia 1.2 million kwa uhalisia na yale yale ila unashawishiwa hii sio sawa hii sawa. Utapeli kila sehemu riba ipo tu ni style tu kama rushwa na facilitation hata kwenye ma hospital yetu ukitaka kukaa foleni lipa alfu 10 ukitaka haraka lipa alfu 20 ndio rushwa za kisasa zamani ukifika unampa muuguzi alfu 20 uitwe haraka siku hizi unazilipa rasmi tu.
Sawa na kumpa kijana bodaboda boxer ya milioni 2 arejeshe elfu 10 kwa siku. Kwa mwaka itakuwa milioni 3.65, FAIDA ni milioni 1.65.
Au umpe cash milioni 2 kwa mwaka alipe milioni 3.65. RIBA milioni 1.65
Janja janja nyingi
 
Hii imekaaje wadau naona imekaa kibaguzi sana,ina maana sisi Tanzania bara hatuna uhitaji na hiyo mikopo au? Zanzibar ni wa muhimu sana kwenu kuliko sisi? Au Zanzibar ni masikini sana mmeamua kuwapa upendeleo?
Kila siku wajasiriamali wanalia kuhusu riba lakini mmeweka pamba masikio.
Kama swala ni imani kuwa hakuna riba bhasi kaeni hivyo hivyo bila kufungamana na upande wowote
View attachment 2118030
View attachment 2118031
Mbona nanino alijenga sana kwao mkawa kimya?
 
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
Benki ya watu wa Zanzibar PBZ ina matawi ya riba Kariakoo na Tazara na Islamic bank Lumumba. Benki gani ya kiislam isiyo na riba hapa Tanzania?
 
Waongo tu hao..na wanafiki watupu..eti islamic bank hakuna riba?..thubutu uone..PBZ riba kama zote...hizi dini kwa unafiki zimejariwa.

Shetani hanaga rafiki..watakulima riba mpaka uchanganyikiwe.

#MaendeleoHayanaChama
Ha ha nakazia .. hakuna cha bure duniani.
Acha wajichanganye watapigwa riba mpka wachakae [emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom