CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni

CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni

Kuna siku nilikuwa German, nikatumia CRDB viza card kulipa, wakaniambia mtandao haujajibu. Nikaacha, nikiwa naendelea na manunuzi yangu ktk duka hilo hilo, nikaitwa na yule mhudumu, huku akinionesha risiti ya malipo yangu ambayo mtandao wa CRDB ulikataa mara ya kwanza. Fikiria kama ningeondoka ktk duka lile ingekuwaje? Tusikatae ushauri, ni vizuri tukachukua tahadhali kabla ya hatari.
 
Ahsante sana Manitoba. Umeanzisha thread nzuri ambayo naamini itatusaidia wengi. Mimi mwenyewe nimeshachukua hiyo card ila nilikuwa nasitasita kuitumia online kwa sababu zinazokaribiana na hizo, ukifika pale customer care CRDB M.City utacheka sana!! Kuna yule dada anayetoa kadi za visa, Mungu wangu, yaani hajui hata maana ya 'online transaction'' yeye anachojua ni ''kadi za internet'' basi!!!! Mi nilimuuliza maswali mawili matatu kuhusu matumizi ya kadi hizi nikagundua kuwa ndo kwanza nampa misamiati ambayo hajawahi kusikia, basi nikaamua kumwacha na kuchukua kadi, mengine nilijua mbele kwa mbele. All in all CRDB hawajajipanga na hizi card. Kama wafanyakazi wenyewe hawajui linaloendelea, itakuwaje ukienda na tatizo la fraud???????
 
Kwa hili CRDB wamepiga hatua, ila nafikiri cost ya hii kitu itakuwa ni kubwa zaidi ya Benefit. Cha kufanya kwa wale wenye kutaka huduma hii ni bora kuwa na account mbili yaani Moja ni kwa ajili ya transaction za online, unahamisha pesa na kufanya transactions on spot, hapo hapo. Nyingine ni kuhifadhia pesa kama una wasiwasi

Huu nafikiri ni ushauri mzuri. Kuwa na Account mbili. Moja kwa ajili ya kuhifadhia VGcent vyako na ya pili maalumu kwa ajili ya Online Transactions ambapo unaweka hela pale tu unapotaka kufanya manunuzi on line. yes, nadhani hii ni njia bora wakati tukiendelea kusubiri uboreshaji wa huduma hii muhimu sana...!
 
Mkuu, inaonyesha wewe umesome tu kwenye shule kuhusu credit cards. Mimi siyo mtalaamu wa uchumi wala mtu wa banki, ila nimetumia CC kadhaa. Labda siwezi kueleza zaidi kwa sababu hiyo. Ila kuhusu wizi kwa credits cards na compensation unaweza check hapa upate info zaidi ya ile niliyokupatia. <http://en.wikipedia.org/wiki/Credit_card_fraud>
Huyu jamaa pamoja na huyu <http://www.securityfocus.com/news/11493> wanakuambia kuwa ni hela nyingi sana zinaibiwa Duniani kwa CC kila mwaka. Hao wote si CRDB. SOma kwa makini sana.

Inawezekana sijaenda hata shule kaka ... lol ... I am fine with that ... Ila turudi kwenye mada ...

Sawa fedha nyingi zinaibwa kwa CC. Kitu kimoja ambacho hujajiuliza ni kwamba hizo pesa zinazoibwa mwisho wa siku ni hasara ya nani? Wewe moja kwa moja uaka-assume mwenye kadi ndio anakula hasara.

Labda nikusaidie kufikiri kidogo. Kama yote hiyo ingekuwa na hasara ya wenye kadi, basi concept ya "Charge Back" isingekuwa ina-exists, au ingebaki ni pambo tu. The fact kwamba concept ya "Charge Back" iko mpaka kwenye sheria za wenzetu, ingekufanya labda ufikiri kwamba wapo watu wanaorudishiwa pesa zao pindi kunapotekea fraud. Hiyo ingepelekea ufikirie kwamba kama wapo wanaorudishiwa pesa hizi, basi pengine hasara hiyo yote si ya mwenye kadi tu, bali ni ya yule anayemrudishia mwenye kadi. Na pengine ungejiuliza swali zuri sana: hizo pesa anazorudishiwa mwenye kadi baada ya fraud, zinatoka kwa nani? Hiyo ingekupelekea kutafuta ukweli wa ni nani hasa anayekula hiyo asara baada ya pesa kuibwa na mwenye kadi kurudishiwa.

Hivi hiyo linki uliyotusaidia ( Credit card fraud - Wikipedia, the free encyclopedia ) umeisoma? Mbona inajieleza vizuri tu? Labda line hii hapa ulii-skip "Merchants in high-risk industries anticipate a certain amount of credit card fraud, and set prices accordingly. These higher costs are then passed onto the customer". Does that make u rethink your beliefs about who caries the burden of the stolen money? I hope u see that its not really the card holder. (at least not directly).

Au hii line uliiona kwenye hiyo tovuti uliyotupatia: "In the case of fraud, the merchant and not the credit card company pays the full cost of the fraud plus a chargeback fee or the merchant's chargeback insurance covers it. In addition credit card companies have to pay for preventing fraud while maintaining a good customer experience."

Kama bado inakupashida kuona: wenye kadi wengi huwa wanarudishiwa pesa zao. Kama wewe kwa experience yako ulishawahi kuibiwa na mtu aliyetumia CC yako na ukakaa kimya, basi pole. Lakini wenzako wengi huwa wana-comlain na kurudishiwa.

Hatubishani ila tunaongelea kwa uzoefu wa kutumia na si kusoma shule na pia kupeana ujumbe kwa kutumia experience. Siwateti CRDB kwa namna yoyote ile na CRDB hawawezi kufanana na Inter-national companies za America au Europe za CC. Pia pamoja na kuwa kuna hiyo disclamer kwa CRDB nimewahi fanya makosa ya k-transaction kwa tune ya equivalent ya 500,000TSHS. Nili-report international Banking section pale CRDB TZ wakarekebisha in three days.

Exactly my brother. Point mojawapo niliyokuwa nataka kuweka ni kwamba hawafanani. Na moja ya tofauti ni kwamba safety yako kwa kadi ya CRDB ni ndogo kuliko ya hao. Kama unadhani hapo nimekosea, basi niambie nimekosea. Wapo waliojibu hii mada waking'ang'ania kwamba wanafana na kwamba term CRDB Visa Card hazina tofauti na nyingine zote "duniani", wakati mtu clearly unaweza kuona kwamba kuna tofauti.

Kama wewe ni mzoefu wa kutumia CC, basi ni vizuri. Na kama ulikuwa hujui kwamba issuer wako huko anachukua steps kukulinda, sio kosa lako. Lakini pengine ungejua hivyo ungeona tofauti na CRDB.

Bottom line, tumia hiyo card huku ukijua kwamba uking'atwa hakuna msaada kutoka CRDB. Na sisemi kwamba CRDB lazima ifanane na hao wengine, la hasha. Ninachosema ni kwamba wewe mtumiaji ujua kuna tofauti, pengine kubwa tu.

Ila ninasema kwamba wako sawa sawa kulingana u-TZ kule. Wata-improve tu service zao with time. Sio muda wa kuanza kwaponda kuwa wao nyuma na hawajali rights za wateja wao. Kuna banks kadhaa za SEA zina masharti magumu sana na nilishangaa sana jinsi wateja wanavyo-chargiwa services a hizo benks ukifananisha na Europe au TZ na jinsi wanavyolalamika sana. Lakini bankers wana sababu.

I hope humaanishi kwamba kama mtu akiona matatizo basi akae kimya tu na kuamini kwamba wata"improve tu service zao with time". Maana fikira kama hizo ndio chanzo kimojawapo cha umasikini wetu.

Halafu naomba kama ungekuwa na mda urudie maandiko yangu yote halafu unionyeshe wapi nimewaponda CRDB. CRDB ni benk kubwa yenye heshima TZ, sasa mimi nani nisiye na hata kibanda kuwaponda? Lakini kwa upande mwingine, sioni kwa nini unadhani natakiwa nikae kimya nikiona kuna tatizo. Kwani ni uongo kwamba hawajali maslahi za wateja wao kwa upande huu wa hizi kadi?

Nimeshatoa mifano kadhaa ya jinsi wengine wanavyofanya kuhakikisha kwamba mwenye kadi inalindwa. Na hizi steps ni standard, zinajulikana, na Visa Internation supports them. Sasa kwa CRDB kuchagua kutochukua hata moja ya hizi steps kunanifanya niamini kwamba hawajajali maslahi ya wateja wao katika hili. Na nimesaini kale kamkataba nikijua hilo. Na nikiibiwa kuna uwezekano mkubwa sitaangaika kuwa-contact CRDB kwa nia ya kurudishiwa pesa zangu. Ila point niliyotaka kuweka, ambayo kaka naona unairuka na kudhani nataka kuwaponda CRDB, ni kwamba wewe mteja unayetumia kadi ya CRDB ujue ukweli ulivyo.

Na naomba nisisitize: sijasema CRDB lazima achukue hizi steps, la hasha! Wao ni wafanyabiashara, na hiyo ni biashara yao. Na nilikuwa nalijua hilo wakati natiasaini kale kamkataba. Ninachosema ni kwamba CRDB hawajachukua hizi hatua.

Kama ninasema uongo niambie, lakini usinihukumu kwa ambacho sijasema.

Tujitahidi kupenda home na vitu vya home. Vilivyo majuu havikushuka. Vilianza hivi hivi.

Nafurahi kusikia kwamba wewe ni mmoja wa wanaopenda vya nyumbani. Labda nikufundishe kitu kimoja. Huko kwa wenzetu havikushuka, lakini unajua vilikujaje? Vilikuja kwa sababu consumers walikuwa wanapigia kelele huduma ambazo hawaridhiki nazo.

Kweli havikushuka, lakini havikuja kutokana na watu kukaa kimya hoping kwamba vitu vita-improve vyenyewe. Unadhani huko kwa wenzetu hao card issuer walipenda interests za mwenye kadi zilindwe kisheria? No they didnt. Na kama nchi zao zingekuwa zimejaa watu wanaosema "tusubiri tu with time vitu vita improve", then usingekuta sheria kama hizo zimepitishwa.

Penda vya nyumbani, na usisahau kudai ubora. Utakuwa unajisaidia wewe na nchi yako. Na hata huyo bepari wako in the long run. 🙂

Take home message: Shule ina umuhimu wake. Ila uzoefu wa siku nyingi una umuhimu zaidi. Rubani aliyekuwa trained kuendesha Boeings za abiria mwaka jana, hawezi kuanza na 747-400 immediately. Lazima aanzie chini kwenye 737-200 kwanza!

Du! mzee naona umenikaba kweli kwenye hilo la shule. Sijui nini kumekufanya ufikirie kwamba hata nimeenda shule kihivyo basi. Elimu ya muhimu niliyonayo ni kusoma na kuandika kiswahili, na ka-kingereza ka kishkaji. Tofauti yetu labda ni kwamba napenda kufuatilia zaidi na kuujua ukweli kuliko kutegemea tu experience yangu.

Na tofauti nyingine ni kwamba nikikupa reference (website, kitabu etc) mimi ninakuwa nimeisoma na kujaribu kadiri ninavyoweza kuielewa ... hapa am just teasing u man ... don't get all red on me 🙂

Tukirudi kwenye mada ... hata mimi ntaitumia kadi ya CRDB. Nimeona niseme hivi kwasababu muheshimiwa na wachache wengine wanadhani ninasema "CRDB should close this service" au "CRDB has done a really bad job". Ila Ninajua risk zake fika, na ninajua jinsi ya kuzipunguza. Na ningependa mtu mwingine yeyote azijue kwanza. Na kwasababu CRDB inazitangaza tu bila kusema chochote kuhusu risks zake, wasiwasi wangu ni kuna watu wataingia bila kuzijua risks na kuanza kulalama baadaye.

Kama wewe unawaambia watu hakuna tatizo kwa sababu ya experience yako, nadhani basi only time will tell ... napenda kuwa proven wrong, kwa sababu ndio jinsi rahisi yakunikumbusha ujinga wangu ...
 
Kuna siku nilikuwa German, nikatumia CRDB viza card kulipa, wakaniambia mtandao haujajibu. Nikaacha, nikiwa naendelea na manunuzi yangu ktk duka hilo hilo, nikaitwa na yule mhudumu, huku akinionesha risiti ya malipo yangu ambayo mtandao wa CRDB ulikataa mara ya kwanza. Fikiria kama ningeondoka ktk duka lile ingekuwaje? Tusikatae ushauri, ni vizuri tukachukua tahadhali kabla ya hatari.

Kwa kesi kama hii, na kam ungeondoka bila hata kuchukua kitu, kale kamkataba ka CRDB kanasema "utajiju".

Lakini kwa wenzetu, zipo taratibu rahisi za kufuta ili urudishiwe pesa zako.
 
Ahsante sana Manitoba. Umeanzisha thread nzuri ambayo naamini itatusaidia wengi. Mimi mwenyewe nimeshachukua hiyo card ila nilikuwa nasitasita kuitumia online kwa sababu zinazokaribiana na hizo, ukifika pale customer care CRDB M.City utacheka sana!! Kuna yule dada anayetoa kadi za visa, Mungu wangu, yaani hajui hata maana ya 'online transaction'' yeye anachojua ni ''kadi za internet'' basi!!!! Mi nilimuuliza maswali mawili matatu kuhusu matumizi ya kadi hizi nikagundua kuwa ndo kwanza nampa misamiati ambayo hajawahi kusikia, basi nikaamua kumwacha na kuchukua kadi, mengine nilijua mbele kwa mbele. All in all CRDB hawajajipanga na hizi card. Kama wafanyakazi wenyewe hawajui linaloendelea, itakuwaje ukienda na tatizo la fraud???????

lol

Mimi siwezi kuwalaumu wale wahudumu kwa kweli. Wao wamepewa kazi ya kufanya, na pengine wanaifanya kadiri ya uwezo wao (ingawa uwezo wao unaweza ukawa limited kidogo).

Mimi tawi langu ni pale Azikiwe kabisa, nadhani ndio makao makuu na ninajitahidi kupiga kwata pale tu.

Kuna dada pale ndio ana-deal na hizi card, kwa kweli anajitahidi. Huwa nnapataga hasira sana, lakini baadaye nikifikiria naona kweli si kosa lake.

Mfano mimi mpaka kuwa na hii kadi ikifanya kazi jasho lilinitoka.

Siku ya kwenda kuchukua nikauliza mara mbili-mbili, "kwa hiyo ipo tayari kuitumia kwenye internet?", kwa sababu ndio sababu pekee kwa nini nilitaka kadi ya CRDB. Nikajibiwa "ndio". Kwenda kujaribu ikagoma, ikisema issuer amegome contact your issuing bank. Nikawanendea, ndio wakaniambia sasa kwamba inabidi ujaze kamkataba ... lol

Haya nikajaza mkataba, nikauliza baada ya mda gani itakuwa tayari, wakaniambia siku mbili. Baada ya siku tatu nikajaribu, ikagoma tena. Nikarudi tena. Yule dada akawauliza watu wa "Card Center" nadhani ambao ndio ma experts sasa. Sasa sijui hiyo fomu yangu ikawa imepotea au ilikuwaje. Nikaambiwa nijaze nyingine. It was clear lakini kwamba halikuwa kosa la yule dada.

Haya nikajaza fomu nyingine ya kale kamkataba. Nikauliza tena "siku ngapi?", "mbili". Baada ya siku nne nikajaribu ikagoma tena. Nikarudi tena CRDB, yule dada akaongea tena na Card Center ... nikaambiwa baada ya siku 2 itakuwa tayari ...

Baada ya siku 3, guess what? ikagoma.

Baada ya kurudi tena mara 2, ndio nikaambiwa sasa kwamba kadi yangu namba zake ziko kwenye range ya kadi zenye matatizo, kwa hiyo inabidi niombe nyingine ...

Kweli baada ya kuomba kadi nyingine, ikakubali ... miezi 4 baada ya kuanza process ya kuomba kadi.

Na trip zote nilikuwa narudi pale ilikuwa inabidi nijaribu kuwaelewesha kwa nini ninafikiri tatizo ni lakwao na sio langu. Saa nyingine nilikuwa nakereka mpaka nilikuwa nawapa offer waitumie wao kadi hiyo kwenye mtandao waangalie kama inafanya kazi, maana mi nawaambia haifanyi kazi wao wananing'ang'anizia inafanya.

Sasa hivi napata shida kupata details ya transaction moja tu ya sh 2,579TZS iliyofanyika october mwaka jana. Na nashindwa kupata. Je, ingekuwa case ya kuibiwa hizo fedha ingekuwaje?
 
am not sure which card these guys are talking about,But if it's the one with 4 digit passcode then that is a BIG NO NO!!do not use it online,especially in "not so obvious websites"

online banking and security is a HUGE issue,kuna part ya vendor wa kadi yako na part yako.

part ya vendor insures that they have strongest encryption mechanisms possible on their passcodes..,puting a 6 digit code is a way 2 go. not four.it takes less than 7 mins to break any 4 coded password and use it.vendors pia has to make sure their site has what it takes for a safe online precense ya wateja wake
a quick look at their website reveals that they are not that serious with security
that RC4 128bit encryption they are using is Ok but not top of the line.security is a very serious matter and it needs highest level of dedication and seriousness.

BUT that aint all,the biggest problem is actually on consumer side.

buying stuffs online especially through websites is a huge toll for average tanzanian consumers,most people are using pirated anti viruses and antispywares which are loaded with enough malaware(s) than they can think of.good thing that Tanzanian shopping online do not excite that many phishers.but with economic improvements that could be another case.

all in all this is a fantastic move by CRDB that needs cleaning up,shining a lil bit and clear some dusts.

taking care of encryption issues,moving that 4 coded password a step higher or give users a more viable solutions like hardware encrypted password alternative etc.
 
CRDB ni benki kubwa na ina uwezo wa kurekebisha mambo mengi haraka kwa kutumia wataalamu wa hali ya juu, uwezo wa kulipa wanao (angalia faida zao kwa mwaka) Lakini kwa uzoefu wa mahusiano na CRDB, kwenye hizo card na katika huduma nyingine hata kuwaangalia tu wanavyoendesha mambo yao ninaona mapungufu katika "creativity na entrepreneurship". Wana tatizo la kuwa wakubwa kiasi kwamba ni kazi kubwa kwao "kuona tatizo na kulirekebisha".

Nimekwisha hangaika sana na hiyo kadi yao nikiwa safarini na niliifutilia mbali kwa sababu nilipowaambia hata hawakujali, ili nisiendelee kugombana nao nikarudi kwenye huduma ya kawaida. Nilikwenda huko kwenye kadi kwa vile nilijua ni huduma nzuri na inahitajika.

Ninakumbuka kuna wakati ilikuwa ukiweka fedha kwenye account ya mtu mwingine walikuwa wanakuchaji, wakati wenzao walikuwa wamekwisha acha -wao walikuwa bado wanaendelea, mimi niliendelea kuwauliza na hawakuwa na majibu ya kufanya chochote. Miaka mitatu baadaye ndio wanabadili (baada ya baadhi yetu kuamua kutumia banki nyingine kutuma vipesa kidogo kwa wazee wetu.

Tatizo la CRDB
- Hawana mfumo wa "continous improvement system"
- Mafanikio yemewalevya hawasikilizi la mtu.
- NAdhani kuna mapungufu katika utafutaji wa wataalamu au mifumo mizuri ya kufanyia kazi.

NA WAO WANUWEZO WA KULIPIA GHARAMA ZA HUDUMA NZURI KULIKO WENGINE.

Wamekuwa wakubwa bila ya kuwa na mfumo wa uongozi, utawala, usimamizi unaoendana na shughuli zao, ndio maana wanaweka hao akina dada kuhudumia madesk ya hizo kadi wakati wenyewe uelewa wao ni kidunchu kuhusu hizo kadi -Sasa customer service gani hiyo??????????????
- Angalia hata ATM zao, ukienda ATM mara 10, mara nne hutapata huduma, ni mwaka wa ngapi toka wameweka hizo ATM, bado hawajajifunza tu???? Je wanahamu ya kujifunza?????
- Ni vyema CRDB ikawa tayari kujifunza na kusikiliza, nakumbuka mwandishi mmoja wa "daily noise" aliandika siku moja "CRDB Bank, the bank that listens...but does not do anything"
-
- Kufanikiwa kwao si lazima ni kwa vile ni wazuri katika "business management" la ni kwa vile tu wapo mahali sahihi wakati mwafaka na connections nzuri.
- Hivi tumekwisha jiuliza kwa nini vibenki vidogo kutoka kenya vimefungua matawi hapa na crdb wapo bongo tu???????????????? mimi sijui lakini inakupa kawasiwasi ka kukosa "drive"
 
lol

Mimi siwezi kuwalaumu wale wahudumu kwa kweli. Wao wamepewa kazi ya kufanya, na pengine wanaifanya kadiri ya uwezo wao (ingawa uwezo wao unaweza ukawa limited kidogo).

Mimi tawi langu ni pale Azikiwe kabisa, nadhani ndio makao makuu na ninajitahidi kupiga kwata pale tu.

Kuna dada pale ndio ana-deal na hizi card, kwa kweli anajitahidi. Huwa nnapataga hasira sana, lakini baadaye nikifikiria naona kweli si kosa lake.

Mfano mimi mpaka kuwa na hii kadi ikifanya kazi jasho lilinitoka.

Siku ya kwenda kuchukua nikauliza mara mbili-mbili, "kwa hiyo ipo tayari kuitumia kwenye internet?", kwa sababu ndio sababu pekee kwa nini nilitaka kadi ya CRDB. Nikajibiwa "ndio". Kwenda kujaribu ikagoma, ikisema issuer amegome contact your issuing bank. Nikawanendea, ndio wakaniambia sasa kwamba inabidi ujaze kamkataba ... lol

Haya nikajaza mkataba, nikauliza baada ya mda gani itakuwa tayari, wakaniambia siku mbili. Baada ya siku tatu nikajaribu, ikagoma tena. Nikarudi tena. Yule dada akawauliza watu wa "Card Center" nadhani ambao ndio ma experts sasa. Sasa sijui hiyo fomu yangu ikawa imepotea au ilikuwaje. Nikaambiwa nijaze nyingine. It was clear lakini kwamba halikuwa kosa la yule dada.

Haya nikajaza fomu nyingine ya kale kamkataba. Nikauliza tena "siku ngapi?", "mbili". Baada ya siku nne nikajaribu ikagoma tena. Nikarudi tena CRDB, yule dada akaongea tena na Card Center ... nikaambiwa baada ya siku 2 itakuwa tayari ...

Baada ya siku 3, guess what? ikagoma.

Baada ya kurudi tena mara 2, ndio nikaambiwa sasa kwamba kadi yangu namba zake ziko kwenye range ya kadi zenye matatizo, kwa hiyo inabidi niombe nyingine ...

Kweli baada ya kuomba kadi nyingine, ikakubali ... miezi 4 baada ya kuanza process ya kuomba kadi.

Na trip zote nilikuwa narudi pale ilikuwa inabidi nijaribu kuwaelewesha kwa nini ninafikiri tatizo ni lakwao na sio langu. Saa nyingine nilikuwa nakereka mpaka nilikuwa nawapa offer waitumie wao kadi hiyo kwenye mtandao waangalie kama inafanya kazi, maana mi nawaambia haifanyi kazi wao wananing'ang'anizia inafanya.

Sasa hivi napata shida kupata details ya transaction moja tu ya sh 2,579TZS iliyofanyika october mwaka jana. Na nashindwa kupata. Je, ingekuwa case ya kuibiwa hizo fedha ingekuwaje?

Aisii hongera sana muheshimiwa, inaonekana umepigana vita kubwa tofauti yako na mimi ni kuwa wewe umeishinda, mimi imenishinda kabisa!! kila nikijaribu kununua kitu online inaniambia kuwa hakuna communication na bank, nifanyeje ndugu ili nami nifanikiwe? nina midude kibao ya kununua lakini ndo hivo tena kadi inagoma. plz help me out!!
 
Kutumia card ya CRDB kwenye mtandao ni wazo zuri. Na CRDB inabidi wapongezwe kwa hatu hiyo.

Ninachosema hapa ni kwamba CRDB wamejitoa kwenye tatizo lolote litakalotokea kwa matumizi ya kadi yako. Kitu ambacho ni tofauti na kwa wenzetu kwa jinsi ninavyofahamu mimi.

Hiyo inafanya matumizi ya hii card yawe na risk zaidi. Yaani hata kama kosa ni lakwao bado hakuna wa kukusaidia.

Kwa mfano ukinunua kitu online halafu kwa bahati mbaya anayekuuzia akatoa fedha zaidi ya zile alizotakiwa kutoa. Halafu kwa bahati mbaya akawa anasuasua kukurudishia fedha zako. Hapo utakuwa huna jinsi ila kukubali umeliwa kimachomacho. Lakini kwa wenzetu kuna taratibu za kupinga transaction ambayo si sawa au si halali, na mwenye kadi waweza kurudishiwa pesa ambazo hukutakiwa kukatwa. Kwa CRDB inaonekana hakuna kitu kama hicho.

Sisemi kwamba CRDB wanatakiwa waweke utaratibu kama huo. Ila nasema wewe mtumiaji ujue hali ilivyo, usije ukang'atwa siku ndio ukaanza kutoa macho na kuwa mkali na CRDB.

Manitoba,

Nadhani usitegemee hata siku moja mfanyabiashara yeyote atakuwa tayari kubeba mzigo wa hasara ambao anajua unaweza kumwangukia. Ninavyofahamu mimi nikuwa transaction zinazofanywa kwenye credit card zinabeba amount kiasi kwa ajili ya ku-cover insurance kwa upande wa benki au taasisi inayohusika. Iko haja ya kufanya research na kuona kama CRDB ina insurance kwenye credit card zake,
Nafikiri kwa vile ndiyo mfumo umeanza kutumiwa na moja ya benki zetu basi CRDB waongeze kasi ya kuuboresha kwa ni mfumo mzuri na wakistaarabu sana. Inakadiriwa katika kipndi cha mwaka 2004 biashara iliyofanyika kupitia kwenye internet huko Marekani ilifikia dola bilioni 70. Ni wazi kuwa huu mfumo unachukua nafasi kubwa katika kufanya biashara.
CRDB wachukue haya kama changamoto.
 
Aisii hongera sana muheshimiwa, inaonekana umepigana vita kubwa tofauti yako na mimi ni kuwa wewe umeishinda, mimi imenishinda kabisa!! kila nikijaribu kununua kitu online inaniambia kuwa hakuna communication na bank, nifanyeje ndugu ili nami nifanikiwe? nina midude kibao ya kununua lakini ndo hivo tena kadi inagoma. plz help me out!!

Ningekushauri ufungue akaunti ya paypal.com . Halafu tumia paypal kwa manunuzi kadiri inavyowezekana. Kama unajua unachokifanya, tumia kadi yako moja kwa moja.

Hilo swala la kutokuwa na communication na bank, nadhani na natumani ni la mda mfupi. Kama ukijaribu kwa wiki mbili bado inagoma, huna jinsi bali kuwaona CRDB. Ukiona wanakusumbua sana na hata wao inawachanganya, waombe wakubadilishie kadi. Mimi it took ages na trip kadhaa kwenda CRDB ili kuja kuambiwa kwamba hiyo card ndio tatizo.

Katika process ya kufungua na ku-verify kwa paypal utaweza kujua kama kadi yako inafanya kazi ama la.

Wakati wa kuverify, paypal wanatoa fedha kidogo (wastani wa 2,500TZS) kutoka kwenye account yako, na inabidi utafute details za hiyo transaction ili upate code flani humo ambayo utaitumia kuverify kwamba hiyo ni account yako. Wakiweza kutoa hiyo, then utajua kwamba inawezekena kutumia kadi yako. Baada ya hapo, nenda CRDB omba statement yako, watakukata 5,000TZS, na omba mungu uikute hiyo transaction na details zake.

Mimi inakuwa ngumu, maana transaction yangu haina details zozote. Lakini kuna mtu nilikuwa naasiliana naye jana yeye ameweza, na details za hiyo transaction alizipata kwenye statement yake. Kwa hiyo labda mimi ndio nina mkosi, au kuna kamkono ka mtu kananiwekea kamtimanyongo 🙂

Ukifanikiwa tustue tujue kwamba inawezekana kweli.
 
Inawezekana sijaenda hata shule kaka ... lol ... I am fine with that ... Ila turudi kwenye mada ...

Suala la shule kwa hapo ulivyoliweka ni defensive tu. Sijasema hujaenda shule na sina shaka usingekuwepo hapa kwenye forum. Nimeongelea shule na experience. Ni kawaida kabisa. Ukisoma vema ile website utapa info zaidi kuhusu CC fraud and control zake.

Heading yako ya thread inasema kila kitu; kwamba tusitumie CRDB Visa card!. Au sijakuelewa? Maana unasisitiza kuwa hujashauri tuziache! Muhimu zaidi ni kukumbuka kuwa CRDB bank wako katika hatua ambazo ni muhimu kuwasaidia kuweza ku-improve zaidi na zaidi. So far hakuna hilo tatizo lako unalosema kwa CRDB kwa upande wangu. Naamini likitokea litashughulikiwa na siku zote events huwa zina-define future.

Sisi/mimi kama m/wateja wa CRDB, kila wakati kama kuna tatizo lolote nina/tuna-report mara moja. Wao kama bankers bila shaka wanashughukia ku-improve products and services kila siku, week, mwezi na mwaka. Hawajalala kama unavyosema na kudai kuwa ni bora ulalamike ili wai-improve! They work around the clock. Naamini hata thread yako wameisoma tayari na wanaifanyia kazi.

Hii siyo time ya kusema usithubutu kutumia CRDB Visa kwenye mtandao wakati wenzako tunatumia. Business zetu ziko TZ na transactions zinafanyika TZ kwa hii bank. Tunaiamini sana, tena kutokana na uzoefu. Nabakia kukushangaa daima unapoleta propaganda zako hapa kuhusu CRDB Visa! Kama umesoma vema posts zangu kwenye hii thread yako, hii ndiyo message yangu kubwa.
 
Asante kaka.

Umesoma heading yangu. Vizuri! Pengine ina utata. Umesoma na paragraph ya kwanza?

Paragraph ya kwanza ina kimstari kinasema "ila kama tu unajua unachokifanya". Niliona kama vile ningeiongezea hiyo kwenye heading, heading ingekuwa ndefu sana. 🙂 Nakubali kwamba hiyo heading inaweza ikawa ina-misslead. Samahani kwa hilo, na paragraph ya kwanza inaonyesha kwamba sikukusudia ku-misslead!

Unasema kwamba hakuna tatizo na likitokea litashughulikiwa, wakati mimi nina kitatizo hapa na inachukua miezi kupatiwa ufumbuzi. Vipi mzee? Kama uko CRDB niambie ntapenda nije unisaidie wewe hilo tatizo langu. Na kama tatizo hapo ni mimi, basi ntakuwa tayari uniambie hivyo, na uniambie kosa langu. Niambie tawi unalofanyia kazi ni lipi, hata kama liko nje ya dar, ntakuja.

Sawa siwezi kusema kwamba "CDRB yakitokea matatizo yanachukua miezi kushughulikiwa" kwa sababu langu ni moja, na pengine yapo mengine yanashughulikiwa haraka. Lakini wewe kusema "likitokea litashughulikiwa" unasound kama mtu wa PR wa CRDB zaidi kuliko mtu aliyetayari kuuona na kuutambua ukweli.

Sisi/mimi kama m/wateja wa CRDB, kila wakati kama kuna tatizo lolote nina/tuna-report mara moja. Wao kama bankers bila shaka wanashughukia ku-improve products and services kila siku, week, mwezi na mwaka. Hawajalala kama unavyosema na kudai kuwa ni bora ulalamike ili wai-improve! They work around the clock. Naamini hata thread yako wameisoma tayari na wanaifanyia kazi.

Hata mimi ni mteja wa CRDB. Na sijasema kama wamelala
PHP:
. Implications za kitu nilichoandika zipo nyingi, sijui nini kimekufanya uchague kwamba nimesema wamelala. Implecation nyingine kwa mfano inaweza ikawa kwamba wako busy sana, na priority zao ziko kwenye kingine na sio hiki.

Hata mimi huwa naripoti moja kwamoja, na hili limenichukua miezi mitatu na halina ufumbuzi. Labda mimi ndio nina mkosi basi. Au labda mimi akaunti yangu haipo katika hiyo plan ya "siku, week, mwezi na mwaka".

Sio kwamba nawaambia CRDB "wanatakiwa wafanye nini", kwasababu wanajua options zilizopo na wakaamua kuchagua walizochagua. Nawaambia watumiaji wenzangu "CRDB hawajafanya nini", na nikiwa naamini kwamba information hiyo itakuwa muhimu kwa watumiaji wenzangu, ili wajue kuna risk kiasi gani; risk ambazo CRDB hawajawaambia. Kama unadhani nimeongea uongo sema.

Kila mtu works arround the clock. Hata mimi katika kazi zangu I work arround the clock. Hilo sio swala hapa. Kama nikiona tatizo nitajaribu kulisema. Kama unadhani sio tatizo sema, usiniambie people work arround the clock; we all do work around the clock.

Na usiniambie kwamba thread hii wameisoma wakati nimetoka kuongea na jamaa wa card center sasa hivi tu. Na story ni tofauti na unayoongea wewe. Kama wewe ni shareholder wa CRDB, basi nawapongeza kwa kazi nzuri. Lakini usiniambie niridhike tu kwa sababu umesoma hii thread, na tatizo langu bado ninalo.

Hii siyo time ya kusema usithubutu kutumia CRDB Visa kwenye mtandao wakati wenzako tunatumia. Business zetu ziko TZ na transactions zinafanyika TZ kwa hii bank. Tunaiamini sana, tena kutokana na uzoefu. Nabakia kukushangaa daima unapoleta propaganda zako hapa kuhusu CRDB Visa! Kama umesoma vema posts zangu kwenye hii thread yako, hii ndiyo message yangu kubwa.

Naanza kuwa na wasiwasi kama unaelewa jinsi transaction za hizi kadi zinavyofanya kazi kuanzia unapo-place order yako, mpaka pesa zinapotolewa kwenye account yako. Ungekuwa unaufahamu angalau kiduchu, usingesema kwamba "transactions zinafanyika TZ kwa hii bank" tu, kwa sababu story ni pana kuliko hivyo. Sasa hivi nimetoka kuongea na mtu wa card center CRDB na anasema kwamba transaction huwa zinafanyika kwingine, na CRDB huwa inakuwa notified, na saa nyingine inakuwa notified later. Na huo utaratibu ndio chanzo cha tatizo la transaction yangu ya paypal. Halafu wewe unaniambia kwamba "transactions zinafanyika TZ kwa hii bank".

Kama umechukulia hizo ni propaganda, naomba nisamehe. Naomba nikuhakikishie sina maslahi yoyote na CRDB kupigiwa propaganda hasi. Cha msingi ni kwamba kama kuna sentensi ambayo nimeiandika na ni ya uongo niambie, kama vile mimi ninavyokuambia unapokuwa umeandika sentensi ambayo si ya ukweli. Mtu akisema "pale mlimani branch ya CRDB kuna msururu mpaka nje" sio propaganda ni statement of fact. Ila mtu akisema "usijali huo msururu, situation ita-improve tu with time" hiyo ndiyo propaganda kwa sababu kuna uwezekano haina msingi wowote wa ukweli, na inakuwa propaganda kwa hakika pale aliyotoa hiyo statement anapokua mkali akionyeshwa kwamba pengine statement yake haijalalia kwenye ukweli.

Kama umekasirika samahani kaka. 🙂 Lakini habari ndio hiyo, kwamba there are unhappy customers out there. Na wewe kuwa happy customer sio sababu tosha ya kumlazimisha kila mtu awe happy customer. Take it or leave it.
 
Ningekushauri ufungue akaunti ya paypal.com . Halafu tumia paypal kwa manunuzi kadiri inavyowezekana. Kama unajua unachokifanya, tumia kadi yako moja kwa moja.

Hilo swala la kutokuwa na communication na bank, nadhani na natumani ni la mda mfupi. Kama ukijaribu kwa wiki mbili bado inagoma, huna jinsi bali kuwaona CRDB. Ukiona wanakusumbua sana na hata wao inawachanganya, waombe wakubadilishie kadi. Mimi it took ages na trip kadhaa kwenda CRDB ili kuja kuambiwa kwamba hiyo card ndio tatizo.

Katika process ya kufungua na ku-verify kwa paypal utaweza kujua kama kadi yako inafanya kazi ama la.

Wakati wa kuverify, paypal wanatoa fedha kidogo (wastani wa 2,500TZS) kutoka kwenye account yako, na inabidi utafute details za hiyo transaction ili upate code flani humo ambayo utaitumia kuverify kwamba hiyo ni account yako. Wakiweza kutoa hiyo, then utajua kwamba inawezekena kutumia kadi yako. Baada ya hapo, nenda CRDB omba statement yako, watakukata 5,000TZS, na omba mungu uikute hiyo transaction na details zake.

Mimi inakuwa ngumu, maana transaction yangu haina details zozote. Lakini kuna mtu nilikuwa naasiliana naye jana yeye ameweza, na details za hiyo transaction alizipata kwenye statement yake. Kwa hiyo labda mimi ndio nina mkosi, au kuna kamkono ka mtu kananiwekea kamtimanyongo 🙂

Ukifanikiwa tustue tujue kwamba inawezekana kweli.

Ahsante mkuu kwa ushauri wako,

Nimefungua Paypal account, nikajaribu kuverify kwa kutumia hiyo kadi ya CRDB, lakini imekataa wananipa message hii ''We were unable to verify this credit card. Please check if the information you entered is correct. Please also make sure your credit card billing address matches your paypal street address''

Nimejaribu kurudiarudia mara kwa mara lakini bado message inakuja ileile, nahisi hii kadi itakuwa haiwi recognized online, naomba ushauri kwa hili, au niwaendee hawa jamaa wa CRDB nione kama watajaribu kurekebisha?
 
Kaka hapo kama bado unahamu ya kutumia hiyo kadi ya CRDB inabidi uwe mvumilivu kwel kweli. Uwezokano mkubwa hapo tatizo lipo CRDB. My guess itakuwa kwamba hiyo kadi haijawa activated kwa ajili ya internate. Unauhakika kwamba iko activated? Na ulijaza kale kamkataba?

Nenda CRDB, hasa pale Azikiwe, waelezee Tatizo. Ukiona hamuelewani, waambie wakuunganishe na jamaa wa Card Center. Ukiongea na jamaa wa card center wasisitizie hiyo message, maana saa nyingine hata wao wanakuwa hawaelewi. Jibu watakalokupa, lipost hapa tafadhali.

Hatimaye mimi nimefanikiwa baada ya miezi kadhaa ya kupiga kwata na kupiga simu CRDB. Na tatizo lilikuwa kwamba system zao zilijikoroga, transaction ile ya paypal yenye verification code haikufanyika automatically, ikabidi ifanywe manually. Na mtu aliyefanya manually hakuona kwamba zile zina umuhimu wowote, akaziachilia mbali. Kwa hiyo hata kama ningekuwa natumia online account, nisingeweza kuona chochote.

Chakushangaza ni kwamba mtu wa mwisho niliyeongea naye aliyenitatulia tatizo haikumchukua hata masaa mawili kutrace hizo information kwenye intermediate servers. Sasa sijui siku zote nilikuwa naongea na vilaza ama nilikuwa nawakuta kwenye bad-mood, au nilitakiwa niwahonge ... sijui. Inawezekana mimi ndio mwenye mkosi ...
 
...Mkuu, hapo mimi umenivunja moyo kabisa maana ndio kwanzaa nimetoka kuomba hiyo kadi! MIEZI KADHAA PAMOJA NA KUPIGA SIMU??? OMG!
 
...Mkuu, hapo mimi umenivunja moyo kabisa maana ndio kwanzaa nimetoka kuomba hiyo kadi! MIEZI KADHAA PAMOJA NA KUPIGA SIMU??? OMG!

Lol

Usiogope mzee. Wapo ambao hawapati tatizo kabisa. Omba tu usiwe mmoja wa wachache wenye vijinuksi kama sisi.

Yaani omba usipate tatizo, maana utaanza kuona jinsi ulivyo na nuksi pale unapoenda kaunta na unakuta unayemuelezea tatizo anakuangalia kama vile haelewi unaongea lugha ghani.
 
''We were unable to verify this credit card. Please check if the information you entered is correct. Please also make sure your credit card billing address matches your paypal street address''

Yawezekana kadi haina tatizo, tatizo lipo hapo kwenye maandishi niliyokoleza. Verification inafanyika kwa kutumia Credit card billing address na paypal street address. Kama hazifanani, then paypal hawawezi kuikubali. Hivyo, hakikisha address unazotumia kwa credit card na paypal zinafanana, neno kwa neno, nukta kwa nukta. Usikosee hata herufi moja. Mara nyingine inabidi uandike mahali ili usisahau.
 
Kwa kadi ya VISA ya CRDB, address verification haifanyiki. Nimejaribu na inaonekana address yoyote inakubali.
 
What if nikikariri zile namba 3 za nyuma kisha nikazifuta kutoka kwenye kadi yangu, inaweza kunilinda kidogo?
 
Back
Top Bottom