Mkuu, inaonyesha wewe umesome tu kwenye shule kuhusu credit cards. Mimi siyo mtalaamu wa uchumi wala mtu wa banki, ila nimetumia CC kadhaa. Labda siwezi kueleza zaidi kwa sababu hiyo. Ila kuhusu wizi kwa credits cards na compensation unaweza check hapa upate info zaidi ya ile niliyokupatia. <http://en.wikipedia.org/wiki/Credit_card_fraud>
Huyu jamaa pamoja na huyu <http://www.securityfocus.com/news/11493> wanakuambia kuwa ni hela nyingi sana zinaibiwa Duniani kwa CC kila mwaka. Hao wote si CRDB. SOma kwa makini sana.
Inawezekana sijaenda hata shule kaka ... lol ... I am fine with that ... Ila turudi kwenye mada ...
Sawa fedha nyingi zinaibwa kwa CC. Kitu kimoja ambacho hujajiuliza ni kwamba hizo pesa zinazoibwa mwisho wa siku ni hasara ya nani? Wewe moja kwa moja uaka-assume mwenye kadi ndio anakula hasara.
Labda nikusaidie kufikiri kidogo. Kama yote hiyo ingekuwa na hasara ya wenye kadi, basi concept ya "Charge Back" isingekuwa ina-exists, au ingebaki ni pambo tu. The fact kwamba concept ya "Charge Back" iko mpaka kwenye sheria za wenzetu, ingekufanya labda ufikiri kwamba wapo watu wanaorudishiwa pesa zao pindi kunapotekea fraud. Hiyo ingepelekea ufikirie kwamba kama wapo wanaorudishiwa pesa hizi, basi pengine hasara hiyo yote si ya mwenye kadi tu, bali ni ya yule anayemrudishia mwenye kadi. Na pengine ungejiuliza swali zuri sana: hizo pesa anazorudishiwa mwenye kadi baada ya fraud, zinatoka kwa nani? Hiyo ingekupelekea kutafuta ukweli wa ni nani hasa anayekula hiyo asara baada ya pesa kuibwa na mwenye kadi kurudishiwa.
Hivi hiyo linki uliyotusaidia (
Credit card fraud - Wikipedia, the free encyclopedia ) umeisoma? Mbona inajieleza vizuri tu? Labda line hii hapa ulii-skip "Merchants in high-risk industries anticipate a certain amount of credit card fraud, and set prices accordingly. These higher costs are then passed onto the customer". Does that make u rethink your beliefs about who caries the burden of the stolen money? I hope u see that its not really the card holder. (at least not directly).
Au hii line uliiona kwenye hiyo tovuti uliyotupatia: "In the case of fraud, the merchant and not the credit card company pays the full cost of the fraud plus a chargeback fee or the merchant's chargeback insurance covers it. In addition credit card companies have to pay for preventing fraud while maintaining a good customer experience."
Kama bado inakupashida kuona: wenye kadi wengi huwa wanarudishiwa pesa zao. Kama wewe kwa experience yako ulishawahi kuibiwa na mtu aliyetumia CC yako na ukakaa kimya, basi pole. Lakini wenzako wengi huwa wana-comlain na kurudishiwa.
Hatubishani ila tunaongelea kwa uzoefu wa kutumia na si kusoma shule na pia kupeana ujumbe kwa kutumia experience. Siwateti CRDB kwa namna yoyote ile na CRDB hawawezi kufanana na Inter-national companies za America au Europe za CC. Pia pamoja na kuwa kuna hiyo disclamer kwa CRDB nimewahi fanya makosa ya k-transaction kwa tune ya equivalent ya 500,000TSHS. Nili-report international Banking section pale CRDB TZ wakarekebisha in three days.
Exactly my brother. Point mojawapo niliyokuwa nataka kuweka ni kwamba
hawafanani. Na moja ya tofauti ni kwamba safety yako kwa kadi ya CRDB ni ndogo kuliko ya hao. Kama unadhani hapo nimekosea, basi niambie nimekosea. Wapo waliojibu hii mada waking'ang'ania kwamba wanafana na kwamba term CRDB Visa Card hazina tofauti na nyingine zote "duniani", wakati mtu clearly unaweza kuona kwamba kuna tofauti.
Kama wewe ni mzoefu wa kutumia CC, basi ni vizuri. Na kama ulikuwa hujui kwamba issuer wako huko anachukua steps kukulinda, sio kosa lako. Lakini pengine ungejua hivyo ungeona tofauti na CRDB.
Bottom line, tumia hiyo card huku ukijua kwamba uking'atwa hakuna msaada kutoka CRDB. Na sisemi kwamba CRDB lazima ifanane na hao wengine, la hasha. Ninachosema ni kwamba wewe mtumiaji ujua kuna tofauti, pengine kubwa tu.
Ila ninasema kwamba wako sawa sawa kulingana u-TZ kule. Wata-improve tu service zao with time. Sio muda wa kuanza kwaponda kuwa wao nyuma na hawajali rights za wateja wao. Kuna banks kadhaa za SEA zina masharti magumu sana na nilishangaa sana jinsi wateja wanavyo-chargiwa services a hizo benks ukifananisha na Europe au TZ na jinsi wanavyolalamika sana. Lakini bankers wana sababu.
I hope humaanishi kwamba kama mtu akiona matatizo basi akae kimya tu na kuamini kwamba wata"improve tu service zao with time". Maana fikira kama hizo ndio chanzo kimojawapo cha umasikini wetu.
Halafu naomba kama ungekuwa na mda urudie maandiko yangu yote halafu unionyeshe wapi nimewaponda CRDB. CRDB ni benk kubwa yenye heshima TZ, sasa mimi nani nisiye na hata kibanda kuwaponda? Lakini kwa upande mwingine, sioni kwa nini unadhani natakiwa nikae kimya nikiona kuna tatizo. Kwani ni uongo kwamba hawajali maslahi za wateja wao kwa upande huu wa hizi kadi?
Nimeshatoa mifano kadhaa ya jinsi wengine wanavyofanya kuhakikisha kwamba mwenye kadi inalindwa. Na hizi steps ni standard, zinajulikana, na Visa Internation supports them. Sasa kwa CRDB kuchagua kutochukua hata moja ya hizi steps kunanifanya niamini kwamba hawajajali maslahi ya wateja wao katika hili. Na nimesaini kale kamkataba nikijua hilo. Na nikiibiwa kuna uwezekano mkubwa sitaangaika kuwa-contact CRDB kwa nia ya kurudishiwa pesa zangu. Ila point niliyotaka kuweka, ambayo kaka naona unairuka na kudhani nataka kuwaponda CRDB, ni kwamba wewe mteja unayetumia kadi ya CRDB ujue ukweli ulivyo.
Na naomba nisisitize: sijasema
CRDB lazima achukue hizi steps, la hasha! Wao ni wafanyabiashara, na hiyo ni biashara yao. Na nilikuwa nalijua hilo wakati natiasaini kale kamkataba. Ninachosema ni kwamba
CRDB hawajachukua hizi hatua.
Kama ninasema uongo niambie, lakini usinihukumu kwa ambacho sijasema.
Tujitahidi kupenda home na vitu vya home. Vilivyo majuu havikushuka. Vilianza hivi hivi.
Nafurahi kusikia kwamba wewe ni mmoja wa wanaopenda vya nyumbani. Labda nikufundishe kitu kimoja. Huko kwa wenzetu havikushuka, lakini unajua vilikujaje? Vilikuja kwa sababu consumers walikuwa wanapigia kelele huduma ambazo hawaridhiki nazo.
Kweli havikushuka, lakini havikuja kutokana na watu kukaa kimya hoping kwamba vitu vita-improve vyenyewe. Unadhani huko kwa wenzetu hao card issuer walipenda interests za mwenye kadi zilindwe kisheria? No they didnt. Na kama nchi zao zingekuwa zimejaa watu wanaosema "tusubiri tu with time vitu vita improve", then usingekuta sheria kama hizo zimepitishwa.
Penda vya nyumbani, na usisahau kudai ubora. Utakuwa unajisaidia wewe na nchi yako. Na hata huyo bepari wako in the long run.
🙂
Take home message: Shule ina umuhimu wake. Ila uzoefu wa siku nyingi una umuhimu zaidi. Rubani aliyekuwa trained kuendesha Boeings za abiria mwaka jana, hawezi kuanza na 747-400 immediately. Lazima aanzie chini kwenye 737-200 kwanza!
Du! mzee naona umenikaba kweli kwenye hilo la shule. Sijui nini kumekufanya ufikirie kwamba hata nimeenda shule kihivyo basi. Elimu ya muhimu niliyonayo ni kusoma na kuandika kiswahili, na ka-kingereza ka kishkaji. Tofauti yetu labda ni kwamba napenda kufuatilia zaidi na kuujua ukweli kuliko kutegemea tu experience yangu.
Na tofauti nyingine ni kwamba nikikupa reference (website, kitabu etc) mimi ninakuwa nimeisoma na kujaribu kadiri ninavyoweza kuielewa ... hapa am just teasing u man ... don't get all red on me
🙂
Tukirudi kwenye mada ... hata mimi ntaitumia kadi ya CRDB. Nimeona niseme hivi kwasababu muheshimiwa na wachache wengine wanadhani ninasema "CRDB should close this service" au "CRDB has done a really bad job". Ila Ninajua risk zake fika, na ninajua jinsi ya kuzipunguza. Na ningependa mtu mwingine yeyote azijue kwanza. Na kwasababu CRDB inazitangaza tu bila kusema chochote kuhusu risks zake, wasiwasi wangu ni kuna watu wataingia bila kuzijua risks na kuanza kulalama baadaye.
Kama wewe unawaambia watu hakuna tatizo kwa sababu ya experience yako, nadhani basi only time will tell ... napenda kuwa proven wrong, kwa sababu ndio jinsi rahisi yakunikumbusha ujinga wangu ...