CRDB wameniibia Zaidi ya Tsh 200,000

Head teacher

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2012
Posts
1,796
Reaction score
412
Tarehe 23/07/2013 niliamisha sh 300,000 kutoka M-Pesa kwenda Akaunti yangu ya CRDB. M-pesa, katika muda huowa kuhamisha, walinithibitishia kuwa hela yangu imeenda CRDB katika akaunti yangu.Cha kustaajabisha, mpaka hivi leo tarehe 28/07/2013 ni Shilingi laki moja (100,000) tu imeingia , na LAKI MBILI (200,000)haieleweki imepotelea sehemu gani ndani ya CRDB. Nimetoa taarifa CRDB tarehe 24,25,26, ikiwa pamoja nakujaza Complaint Form, bado hamna madadiliko katika akaunti yangu. Hii inanitia hasara sana kifedha kwani kwa siku ninaangalia salio zaidi ya mara 10 kwa kutumia Sim-Banking(kwani mimi nipo mbali na ATM), ambayo kila nikifanya hivyo nakatwa charges na Vodacom, M-Pesa, na CRDB......Ninaamini JF ni kila kitu, mwenye ushauri namna ya Kupata pesa yangu nitamshukuru sana.
 
Mkuu haya mambo hutokea sana, sometimes mitambo huwa inajicontadict na kufanya mafyongo
Kama umekwenda bank na kujaza complain form lazima walikupa muda wa siku kadhaa tatizo lako litakuwa tayari
Na kama muda umekwisha basi rudi tena bank kawaeleze watakwambia tatizo ni nini

Kwa haraka haraka inawezekana kabisa mitambo ya Vodacom ilijichanganya ikaripoti transaction imekamilika na kukupa taarifa hiyo ila kiukweli transaction haikukamilika na pesa bank haija kwenda na kwenye acc yako ya mpesa imetoka ipo ina hang
CRDB hawawezi kukupa pesa ambayo haijaingia kutoka Vodacom, inabidi wawasiliane na voda, voda waiingize manually ndio wewe unaweza kuichukua kwenye acc yako......so tatizo lipo Voda na sio CRDB
Pole ndio kadhia ya teknolojia hiyo mkuu ila hawajakuibia pesa yako
 
Maelezo mazuri sna mkuu. Ni kweli kwamba hata vod nao kuna wakati wanachemka. Juzi walithibitisha kwamba hela yangu imeshatutwa crdb na crdb wakanipa ujumbe kuwa wamepokea. Voda walithibitisha kuwa wametuma 100,000 kwenda crdb na crdb na watilhibitisha kuwa wamepokea 10,000 kutoka voda. Iliniumiza kichwa sana na nikaangalia salio cfdb nikuta ni kweli wamepokea 10,000 kutoka voda na pia nikaangalia salio ktk voda nikakuta imetika 100,000. Nilianza na voda kuwauliza waknambia kuna ttzo la mtandao kwahyo 90,000 ilikuwa bdo haipo crdb wala ila baada ya saa 24 wlinambia hela itarudi ktk voda ili nitume tena na ilirudi kweli. So mkubwa ajaribu kucheki na voda pia
 
Asante, ila nitajitoa Sim-Banking,licha yakuwa gharama, haziaminiki
 
Dah, hizi technolojia za kichina kumbe hatari hivi..
 
Ndani ya CRDB kuna wezi hasa kitengo cha IT! Kama ni tatizo la technlgia isingeenda hela yote....lakini kama imeingia kiasi na kilichobakia hakijulikani kilipo...huo ndio wizi ndani ya tekelinalokujia!

Kuna mshakaji wangu naye kiasi cha hela yake kilikuwa hakinekani kiajabu tu katika acc yake CRDB.....akawa akienda anajibiwa kama wewe.....nikamshauri akienda tena aombe kuonana na Branch Manager kama majibu ni yaleyale.....wale wafanyakazi waliokuwa wanamzingua mshikaji wangu waliposikia jamaa anataka kuonana na mkuu wao...hela ilirudi (walimwambia baada ya masaa kadhaa akaangalie acc yake zitakuwa tayari- na ikawa hivyo). Nami nakushauri omba kuonana na mkuu wao (branch manager - halafu uone)!
 
Kuna wizi, nafikiria kufungua kesi mahakamani.Mashahidi ni M-pesa
 
usitumie kabisa huduma ya m-pesa to bank, m-pesa to nmb / m-pesa to crdb etc wengi wamelizwa
 
Sasa hapo waliokuibia ni cedb au voda?

look at it this way. Kama umemuagiza mtu akupelekee pesa bank, akakutumia ujumbe kuwa kashakuwekea pesa bank, lakini ulipoenda bank umekuta pesa hazijawekwa. Who will be your first suspect, bank au yule uliyemuagiza? Kama ukihitaji kushtaki nani utamfikisha mahakamani, bank au yule uliyemtuma?
 
Inanipa shida kidogo, CRDB wananiambia tatizo halipo Mpesa bali CRDB, wao wanakiri lakini hawaweki pesa akaunti.
 
Kwa nini bank au mpesa wanaanzisha huduma wasiyoiweza. Shame
hapo ndio kaazi kweli,

kama ku-deposit bora niende kabisa bank kudeposit but sio kwa mpesa,

kama nikutoa bora nitafute atm ilipo but sio kwa mpesa, au kama sina kadi bora nitumie cardless service najitumia mwenyewe kwenye laini yangu nyingine nakwenda toa!
 
Imetokea pia kwangu leo,nilikuwa naweka Tsh 58000 tu,cha ajabu imeingia 8000 pekee. Hii nyingine sijui imekwenda wapi. CRDB wana matatizo sana na sym zao aise.
 
Imetokea pia kwangu leo,nilikuwa naweka Tsh 58000 tu,cha ajabu imeingia 8000 pekee. Hii nyingine sijui imekwenda wapi. CRDB wana matatizo sana na sym zao aise.
duh, pole.Inabidi hizi huduma zisitishwe.Zitachangia wizi hizi...
 
Kuna nchi huduma za bank kupitia mobile operators zimejengewa mazingira ambayo haziwezi kuendeshwa, na badala yake watu wanakuwa na trust na mabenki tu
 
Biashara ya hela kufanya bila risiti au kithibitisho ni hatari c kwa cmu banking tu bali hata kwa wanaodraw hela atm bila kuchukua receipt,mtalia yalinikuta csahau
Uctumie mpesa sababu huna receipt na n wachache wanaotunza sms pia atm kumbuka receipt walioweka hvyo c wapumbavu shortcut znaponza ndg zanguni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…