Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 412
Tarehe 23/07/2013 niliamisha sh 300,000 kutoka M-Pesa kwenda Akaunti yangu ya CRDB. M-pesa, katika muda huowa kuhamisha, walinithibitishia kuwa hela yangu imeenda CRDB katika akaunti yangu.Cha kustaajabisha, mpaka hivi leo tarehe 28/07/2013 ni Shilingi laki moja (100,000) tu imeingia , na LAKI MBILI (200,000)haieleweki imepotelea sehemu gani ndani ya CRDB. Nimetoa taarifa CRDB tarehe 24,25,26, ikiwa pamoja nakujaza Complaint Form, bado hamna madadiliko katika akaunti yangu. Hii inanitia hasara sana kifedha kwani kwa siku ninaangalia salio zaidi ya mara 10 kwa kutumia Sim-Banking(kwani mimi nipo mbali na ATM), ambayo kila nikifanya hivyo nakatwa charges na Vodacom, M-Pesa, na CRDB......Ninaamini JF ni kila kitu, mwenye ushauri namna ya Kupata pesa yangu nitamshukuru sana.