Emory Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 478
- 572
Card sio account number, ukibadilisha card bado utakuwa kwenye DDiS, utatakiwa kuseti Simbanking ambapo unaenda kwenye tawi la karibu au lililoandikishwa kwa huduma za usajili wa Fingerprint(DDiS).Kwa sisi kubadilisha card ni process ndefu sana.
Maana tayari tumeshajiunga mpaka na mfumo wa alama za vidole na hizi accounts!
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Hii inakuwaje bila ya password.mbona Kuna sehemu huwa wanakuomba paswedi ili waruhusu muamala mkuu.ila pia hii kitu nishawahi kuisikiaMtu akichukua card yako akachukua namba ya card (sio a/c no), expire date na cvv basi. Hapo atajiunga na malipo yoyote online na utakatwa wewe. Ila CRDB kwa miamala yoyote online hua wanatuma message ya kawaida kwako vipi.
Fuatilia ujue huko itune ni nani amejiunga.
Mimi transactions online bora kutumia mpesa mastercard
Footage inakusaidia kumkamata mwizi wa POS?Ila ukiomba foottage za siku ambazo sio wewe uliyetoa ATM si utamuona aliyetoa au haiwezekaniki hiyo Mkuu?
Mambo ya kuacha acha kadi ya bank au kuonyesha onyesha huenda kuna mtu alimark baadhi ya taarifa za kadi then akawa anatumbua tu.Habari za wakati huu Great thinkers!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Ni kawaida kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa pesa kutoka katika account zao za benki kidogo kidogo.
Huo ndio mwanya wanaotumia CRDB kuwatapeli fedha zao, kivipi?
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS). Mara nyingi, kama ilivyo kwa wanafunzi wengi, natoa pesa kidogo kidogo. Hilo hupunguza hata risk ya kuibiwa, natoa pesa ambayo nina matumizi nayo tu!
Tangu naanza kupokea Boom la kwanza, nilikuwa na wasiwasi kwamba pesa yangu inapungua. Lakini pasipo kufuatilia na pasipo kujua nika'assume' kwamba itakuwa nyingine inaishia kwenye makato!
Lakini ile hali ya kwamba pesa inapungua haikunipa amani kabisa!
Baada ya Boom la mwisho kwa mwaka huu ambapo kwa MUHAS tunapokea Takribani Tsh 665,000/= nikatoa laki 3 kwa ajili ya kulipa madeni na matumizi mengine.
Nilipokuja kutoa tena kiasi cha fedha elfu 50, nikashangaa kuona imebaki 190,000/=!! Hata kama ni Makato yanakuwaje makubwa hivi?
Nikaenda kuwauliza CRDB Kariakoo Branch wakasema hawawezi kunisaidia labda niende kwenye Bank niliyosajilia bank account yangu. Hivyo basi nikaenda Azikiwe branch na baada ya mvutano mrefu mwisho wakaniambia niombe bank statement.
Nikaomba ya June na July, nilichokikuta ndio hicho hapo chini! Hizo sehemu zenye duara ni malipo madogo madogo ambayo sija yafanya na wanadai nimeyafanya.
Ikumbukwe kwamba sijalipia premium kwenye App au sehemu nyingine yoyote na wala sifanyi manunuzi ya mtandaoni.
Itoshe kusema kwamba, CRDB ni wezi! Na huenda ikawa wanaibia wengi kwa staili hii hii bila wao wenyewe kujua. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wanafunzi wengi sio wafuatiliaji.
Na je, hivi ni kweli hizi Tembo card zinaweza kutumika kwenye kulipia malipo ya mtandaoni? (iTunes)
Nimelileta hili jukwaani, ili watu walitambue. Binafsi nitaangalia namna ya kuwahama japo ni process ndefu kwa mujibu wa taarifa nilizopewa. Lakini je, huko kwingine vipi?
Inauma sana!
View attachment 1871494View attachment 1871494
Basi waulize bank hicho ni nini?Hakuna message yeyote iliyoingia boss. Message ya mwisho ni pale nilipoingiziwa Boom.
Na Simbanking sina boss
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Sio website zote inaombaga password, kuna nyingine inaenda tuu.Hii inakuwaje bila ya password.mbona Kuna sehemu huwa wanakuomba paswedi ili waruhusu muamala mkuu.ila pia hii kitu nishawahi kuisikia
Kuna mtu anatumbua kadi yako, Aliyekuambia kufanya POS mpaka mtu awe na password yako ya bank nani?Mkuu, subscription inaweza kufanyika hata kama sijatoa taarifa zangu za bank? Na hata hiyo Application ya iTunes sina kwenye simu yangu, hilo linawezekana vipi?
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Anything can be changedKwa sisi kubadilisha card ni process ndefu sana.
Maana tayari tumeshajiunga mpaka na mfumo wa alama za vidole na hizi accounts!
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Mimi nikichukua hiyo kadi yako tu, nakomba hela zote hata kama sina namba yako ya siri.Daaah ila anaweza vipi kuitumia kama hajui namba ya siri?
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Akisoma hapa atakuelewaMtu akichukua card yako akachukua namba ya card (sio a/c no), expire date na cvv basi. Hapo atajiunga na malipo yoyote online na utakatwa wewe. Ila CRDB kwa miamala yoyote online hua wanatuma message ya kawaida kwako vipi.
Fuatilia ujue huko itune ni nani amejiunga.
Mimi transactions online bora kutumia mpesa mastercard
Unasema kadi yako ni VISA halafu hapohapo unasema haina hivyo vitu alivyotaja huyo jamaa. Haupo serious.Card yangu haina hivyo vitu mkuu. Nafkiri labda huzijui Tembo card za wanafunzi
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
basi inawezekana kuna mtu kafanya kutimia taarifa zako za benki fuatilia wala sio CRDB hao
iko wazi ila kiongozi hii yeye haitakiInawezekana kabisa ana mtu alitumia kadi yake kujisajiri kwa online purchases maana ile hai hitaji namba siri za ya majina,kadi namba na expiration yake!
Cheki na jamaa zako unao share nao room au mchuchu kama mmoja wapo ana iphone huyo ndio anatumia kadi yako.
Thank youSio website zote inaombaga password, kuna nyingine inaenda tuu.
Hili suala ni hatari sana. Ndiyo maana mimi maina account na ninayofanyia malipo ni tofauti. Haina usalama kabisa.Mkuu
Kama ulijiunga na Internet Banking na ukaruhusu malipo ya online ni rahisi sana kuibiwa
Kufanya malipo online mtu anahitaji namba ya Visa/Mastercard na CVV [Card Verification Code], ile number inakuwa na digits 3 nyuma ya kadi. Mtu akiona tu kadi yako na akachukua hizo details anafanya malipo bila ya kuwa na password yako.
View attachment 1871595