CRDB yawa ya 8 kwa kutoa huduma Tanzania!

CRDB yawa ya 8 kwa kutoa huduma Tanzania!

Mkuu Jethro kuna thread humu nafikiri mwaka jana iliyoichambua CRDB na Kimei wake kwa kina. Wengi wetu tuliliona hili linakuja kutokana na uozo wa management ya juu ya CRDB. Corporate vision na Mission naona ina matatizo hasa baada ya Denmark kuondoa ubia wake.

Hili tulilisema sana, lakini wengine wakasema tuna mwazo ya kikoloni na hatujiamini.

Sasa tunaona uzalendo wa Kimei unapotufikisha, bila kusahau kuwa suala la EPA na CRDB lilijikita tena sana.

Institutions kama hizi hazendeshwi kisiasa ama sivyo CRDB na NBC ya zamani ni kama nyani wasiochekana kundule.
CRDB is a conduit to a few individuals personal glory

check who gets guarantees fromCRDB
 
Sijawahi Kujaribu Banks Nyinginezo Lakini kwa sisi watu tunaosafiri Mara kwa Mara .. VISA CARD ZA CRDB zinasaidia saaaaaaaaaaana!!! NAWAPA HONGERA KWA HILO..:becky:
 
Mkuu kwa kuongezea
Kuna baadhi ya wafanyakazi wa CRDB wana nyodo sana. Mfano UDSM Branch. Unamuuliza mfanyakazi akupe maelezo ya aina fulani ya akaunti na inafanyaje kazi anakurushia karatasi kama vile wewe umekwenda kuomba hela. Watu wanasahau kusoma na kuelekezwa hasa kwenye mambo ya hela ni vitu tofauti. Kwenye desk la maulizo huwa hakuna utaratibu wowote wa kusikilizwa. Mfano mtu anakuja anakukuta umekaa zaidi ya nusu saa unasubiri kuhudumiwa, anapitisha makaratasi juu ya kichwa chako, baada ya muda unaona pesa zinapitishwa tena juu ya kichwa chako anaondoka

Ukikutana na nyodo za Lucy Kimei utatamani kufunga account kabisaaaaa. Lucy anaweza kuongea na simu kwa dakika hata 15 wakati kuna mteja kwenye desk lake! Achia mabali majibu yake ya kunya na kubetulia wateja midomo. CRDB UDSM customer care ni sifuri.....
 
Ukikutana na nyodo za Lucy Kimei utatamani kufunga account kabisaaaaa. Lucy anaweza kuongea na simu kwa dakika hata 15 wakati kuna mteja kwenye desk lake! Achia mabali majibu yake ya kunya na kubetulia wateja midomo. CRDB UDSM customer care ni sifuri.....
kaka usinikumbushe, nilimaliza ud 2008, katika wafanyakazi wa CRDB Hapo, udsm mwenye nyodo, ni huyo lucy, yaani hana customer care hata kidogo, ni jeuri sanaaaaaaaaaaaaaa
 
kaka usinikumbushe, nilimaliza ud 2008, katika wafanyakazi wa CRDB Hapo, udsm mwenye nyodo, ni huyo lucy, yaani hana customer care hata kidogo, ni jeuri sanaaaaaaaaaaaaaa

Ana haki zote benki si ni ya kwake "Kimei" nani atamuuliza bosi kuhusu utendaji wake mbovu? Labda bodi ya wakurugenzi na yeye anawadhibiti kwa vibahasha vinono kabla ya kila kikao, watamkemea?
 
Wajameni mliojisajili naomba Masada wa kujua namna ya kujisajili. Maana mi naishia pale penye tarehe ya ukomo wa matumizi ya kadi. Kadi yangu imeandikwa VALID THRU 12/14 sasa nijazeje hapa?
 
Tanzania hamna huduma nzuri kwa asilimia kubwa ni makampuni machache yanayotoa huduma nzuri na miongoni ya hayo ni yale yenye wateja wachache.
 
CRDB is a conduit to a few individuals personal glory

check who gets guarantees fromCRDB

duh, mpaka CRDB wakupe mkopo lazima upungue kilo kadhaa
 
Kwa kweli wanatakiwa wajirekebishe!!Uchache wa wafanyakazi unaboa sana!! Mfano Mapato Branch,Arusha.Counter ziko 4,ila utakuta 2 ndio zinafanya kazi!Ukienda hapo ujiandae kupoteza zaidi ya lisaa limoja pale!!!
 
manufaa ya mabank yote ya Tanzania kwa mtanzania wa kawaida ni kuweka na kutoa fedha bank, na ndiyo maana haya mabenki mengi hujiita commercial banks

deposits acrued at the bank is not eguivalent to gains a customer receive, very rediculous

testimonial: niliwahi kutuma Telegraphic Money Transfer (TT) kwenda japan in August 2011 kutumia CRDB Bank PLC in which i am their client, fee ya TT ni US $ 50 per transaction, baada ya hapo unatakiwa kupewa transaction advice slip inayoonyesha TT ilivyo kuwa processed to the beneficiary including intermediary bank, kawaida haitoki kwa wakati siku hiyo hiyo, basi nikaambiwa niende siku yoyote kuchukua, kilichotokea kwa vile sikua naihitaji recently nikaenda kuichukua after one month kwani nilyemtumia TT (beneficiary) alishanitumia email kuwa amepata within two days, basi nilipokwenda CRDB kuchukua TT advice slip nikaambiwa nilipie TZS 15,000 eti ni search fee, nikawaambia wapi terms and conditions once i processed the TT , jibu likawa hamna mwisho wa siku nikapewa advice slip yangu which was my lawful right

it is discouraging
 
Kweli inasikitisha sana kwa Bank kama CRDB kushika nafasi ya 8 kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Matatizo nayo yajua yaweza kuifikisha hapo CRDB kama mie mteja wao ni

  1. Feature plan zao mbovu au haziwakidhi wateja waliopo na kuwavutia wateja wapya
  2. Branch Managers-kwa jinsi mie navyo oona managerz wachache sana wanakuwa makini kwa branch chao na wengi wao wapo pale kujilimbikizi mahela tuu kwanini nasema hivyo utakuata manager wa branch fulani anajifanya ati anabana matumizi kumbe anaba hivyo ili azisukumie kwake huku wafanyakazi wake hata kuwaboreshea vitendea kazi kama viti desks au stationaries za kufanyia kazi anajifanya ati muwe mwaijua cut coast. me na uhakika Kimei akituma jopo la wakaguzi kwa managers watakuja na mambo mengi na wasiwulize managers kupata uhakika wawaulize wafanyakazi wa hizo bank na wateja wanao hudumiwa na mbaya zaidi hakuna suggestion box ikiwepo ni boss ndie anasoma hapo kweli ukweli utamfikia kimei??
  3. Motisha - esp kwa wafanyakazi wa CRDB ni kuwa wanaupendeleo au ndio nini mishahara ni midogo sana na ukizingatia hali ya maisha imeisha anza kuwa ngumu uchumi uko juu sana haulingani na mishahara wanayo pokea,wanakumbwa na matatizo ya usafiri,kodi ya nyumba, sijui wana hisa wa CRDB wanalionaje hilo swala je wao wanafurahi hiloo???
  4. Uchache wa wafanyakazi ndio kabisaaaa sijui siku hizi ndio style ya kufanyisha watu kama kile kipindi cha slave na master? mwategemea mtu mmoja ahudumie customers wanao kuja front dest,Tailor, na sehemu hizo zote ni mtu mmoja au kwa tailor unakuta wako wa wili foleni ya watu zaidi ya 150 hiyo niu asubuhi tu waingiapo.
  5. ....
  6. .....
  7. ......
  8. ,.......
Wadau changieni zingine zimfike kimei na member board ya CRDB inatuuma sana bank yetu inakuwa ya 8 kwa uzembe wa Board inashindwa jua hali halisi au kumekuwa na siasa nako au watu wamekuja kuchuma pesa CRDB??

Tupatie top tuone performance ya banks
 
Sijawahi Kujaribu Banks Nyinginezo Lakini kwa sisi watu tunaosafiri Mara kwa Mara .. VISA CARD ZA CRDB zinasaidia saaaaaaaaaaana!!! NAWAPA HONGERA KWA HILO..:becky:

Charge zake vp?
 
Tupatie benki au kampuni ya kwanza hadi ya saba ili tujadili,pia elezea hiyo ranking imeangalia vigezo gani, vinginevyo uache majungu.
 
Sijapata nafasi tu, actually nataka kufunga account ya crdb nifungue bank nyingine. Always foleni ni ndefu bank, kuna dirisha za kuhudumia wateja zisizo na wahudumu. kero kubwa zaidi usithubutu kujidai unalipa bill ya hotel kwa kuchanja kadi labda ulipe kabla kama mr bean! kujibiwa 'we can reach your banker at this time' ni jambo la kawaida kabisa! Hukawii kuhang hotelini for a few more hours ukingojelea 'try again later' ifike, manake wasipokubali simu ya tochi na handbag kama rehani,mweh!
 
JETHRO kizungu chako Mmmmh!!!

Ni kweli kina utata bora angenyoosha kwa kiswahili maana hata mie kanichanganya hapo kwy namba 4, tailor??? Huyo fundi cherehani anafanya nini tena humo CRDB? au ana maanisha teller??!!
 
Back
Top Bottom