Wapendwa wana Jamvi,
Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.
Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?
Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.
Tiba