huyo yupo kama mimi, hata mke wangu tukija suala la maza huwa anajadili kwa makini sana kwasababu anajua anagusa kwenye moyo. I love my wife, na watoto wangu, lakini wote wajue kwa miezi 9 nilikuwa natumia damu ya mama yangu, nilikuwa nakula anavyokula, amenisafisha hadi kinyesi, nimemnyea na kumkojolea sana, amevumilia mengi sana, alinipenda sana, hata nilipokuwa mkubwa alionyesha upendo wake wote, hadi leo anaonyesha upendo wake wote, nipo moyoni mwake na yeye yupo kwangu kwasababu tulikuwa mwili mmoja awali. niliishi tumboni mwake. mimi ni last born, nafikiri mnaelewa nikiongea hivi.
wife ameamua ampende mamangu kwa moyo wote, na huwa ananikumbusha huduma kwake zile ambazo nimetingwa. wakati nasoma sekondari alikuwa anauza vikuku vyake ananiwekea pesa mfukoni kwa sairi hata dingi ihajui na yeye anabaki na pesa kidogo, kipindi cha njaa alikuwa lazima alikuwa anaweka hazina ya kunilisha mimi hata kama wakubwa zangu hawatashiba sana. kifupi, alinipenda upendo wote, sasahivi ni mtu mzima sana na ni zamu yake kufaidi matunda yangu.