Cristiano Ronaldo kuukosa mchezo wa Manchester Derby, United wapata presha

Cristiano Ronaldo kuukosa mchezo wa Manchester Derby, United wapata presha

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Manchester United inatarajiwa kumkosa mshambuliaji wake mkongwe, Cristiano Ronaldo katika mchezo dhidi ya Manchester City, leo Jumapili Machi 6, 2022 kutokana na kuwa majeruhi.

Hizo ni taarifa mbaya kwa United kwa kuwa mchezo huo ni muhimu kwao dhidi ya City ambayo inaonekana kuwa vizuri kuliko United.

Straika mwingine mkongwe wa United, Edinson Cavani inaelezwa naye hayumo katika mipang ya Kocha Ralf Rangnick.

Kwa mana hiyo United inaweza kumtegemea Marcus Rashford kusimama kama mshambuliaji wa kati.

Taarifa hizo zimewapa presha mashabiki wa United kwa kuwa wanajua timu yao haipo katika kiwango kizuri, hivyo kumkosa Ronaldo inawezekana kukaongeza nguvu kwa City katika mchezo huo wa Premier League.
 
Hata kama angekuwepo Ronaldo lazima kipigo kingekuwa pale pale tu ...!
 
Yàani mashabiki wa man u hawaumii kama sisi wa Liverpool...draw ingetufaa sana
 
Kwani huyo nae ni mchezaji wa kutegemewa kwenye timu? tupen stats zake mwaka huu nyie timu penaldo wa jf
 
Back
Top Bottom