MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hii ni kama utapeli wa Jatu au Mr Kuku ila imetokea nchi jirani ya Zambia. Wakurugenzi watatu wa Kamono Farms wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa makosa ya kujipatia pesa kilaghai kutoka kwa wananchi kwa kuwashawishi wawekeze fedha zao kwenye kilimo kwa ahdi ya kupata faida kubwa sana kitu ambacho hakiwezekani. Kwa miezi kadhaa wananchi wengi wamekuwa wakijitokeza na kulalamika kutokuwa na mrejesho wowote kuhusu uwekezaji walioufanya huku uongozi wa Kamono ukiwakwepa. Wanatuhumiwa kujipatia kiasi cha Tsh 17b (kwa exchange rate ya kwacha kwenda tsh). Account zao zote zimefungiwa na pia zimekamatwa kama kwacha 760,000 cash.
Kimsingi kilichotokea Jatu na Mr Kuku ndo kimetokea kwa wenzetu. Yaani mambo ni yaleyale. Stori ya Mr Kuku, Jatu na Kamono ni moja tofauti ni nchi tu. Cha kushangaza watu kuendelea kuwaamini. Mimi nadhani serikali zetu zianze kuwakamata pia hawa wananchi wapumbavu wasiojielewa ambao wanaona moto na kwenda kujiingiza kisha kuanza kulia wanaungua.