Hello bosses kwanza kabisa naomba mods msiedit heading ya huu uzi.
Kumekuwa na wimbi la watu kutoheshimu professions za wengine na hili linabackfire mdg mdg.
Watu wengi siku hz wanadhan kila mtu anaweza kuwa investor wakiongozwa na kaka yao fln kule twitter lkn niwaambieni tu hio ni profession kama profession nyingine na inabidi uisomee ili usijeukakutana na majanga yalowapata wale investors wa hii Luna coin.
Kwanza ntaelezea kwa nn watu walidanganya na wakadanganyika. Kwenye crypto hizi coins bei yake inabadilikabadilika sana so wengi huogopa kuinvest. Sasa akatokea jamaa mmoja anajiita somebody 'Kwon' raia wa korea na muhitimu wa Stanford akabuni coin moja ambayo ilikua pegged kwenye 'stable coin' fln inaitwa UST (Terra USD).
Subiri, najua unaweza kujiuliza stable coin ni nn. Stable coin ni coin ambayo iko in sync na asset au currency ambayo haibadiliki sana value yake (less volatile asset/currency) hivyo kufanya hio coin kuwa stable. Stable coin nyingi zinakua pegged kwenye usd kwa mfano (hadi wiki ilopita) 1UST ilikua ni sawa na 1 USD ($ dollar). So hio inamaanisha value ya hio TerraUSD ni inakua sawa na value ya Dollar. Mfano mwngine wa stable coin maarufu ni Tether (USDT) hii ipo kwenye blockchain ya etherium.
Sasa huyu Kwon akatengeneza coin hii inaitwa Luna ambayo sio stable coin lkn akaipeg na Stable coin hio ya TerraUSD (UST).
So watu wengi wanaojiita investor wa crypto wakaona Luna Coin ni deal coz iko pegged kwenye stable coin(bila kujua how hio UST inavyopata stability yake). So wakanunua na coin ilifika mbali sana last week value ya coin moja ya luna ilikua ni $85.
Kumbe haya mambo yanahitaji utaalam na investors wakurupukaji hawakujua hilo.
Iko hv, nmesema stable coin zinakua pegged na less-volatile assets, so wengi hutumia USD DOLLAR. Mfano value ya USDT inachezea kwenye 1 dollar, na value ya UST (TerraUsd) ilikua inachezea humohumo. Tofauti ni kwamba USDT inatumia Real Dollar Reserve, lkn hii UST inatumia virtual au tuuite 'Algorithmic dollar'. Yaan huyu Kwon alitengeneza mechanism fln kwenye program yake ambayo inatumia bitcoin reserve ili kumantain value ya UST (stable coin anayotumia kubackup Luna).
Sasa kwa wachache walolifahamu hilo walijua kwamba aidha wasiinvest kwenye Luna coz stablecoin yake UST haitumii real Dollar kama zilivyo Tether (USDT) na stable coin nyngne Au watumie strategy kwamba bitcoin ikianza kushuka kwa kasi basi ni muda kwa kuuza Luna coz behind the scenes Luna inategemea Bitcoin.
Lakini wale wanaojidai kujua kila kitu waliposikia Luna iko pegged kwenye stablecoin UST moja kwa moja waka-buy.
So kilichotokea ni kwamba kama ulikua na Luna 1000 last week ungeweza nunua Range mpya ya 2021 na ukabakiza chenji ya kutosha tu ila kama bado unazo leo hii basi hazina tofauti na trash coz hata IST used choka mbaya kutoka japan haupati.
Note::Kuna wanaojipa moyo kuwa Luna itaregain value yake lkn ni kitu ambacho haiwezekani coz madudu yake yashawekwa wazi na issue ya kutumia virtual dollar imewakatisha tamaa sana waloamini Luna coin. Na isitoshe hapa nnavyoongea huyo Kwon 'Aloanzisha Luna' alikua anaomba msaada polisi coz watu walivamia nyumba yake juzi na jana wakimshutumu kuwadanganya khs coin alotengeneza.
Ukipewa ushauri khs kuinvest na mtu fln kuwa makini sana coz kasoma summary ya kitabu thn akatengeneza summary yake ndo akatumia hio summary yake kukyshauri
~Peace
Kali Linux
Stable coin inakuwaje pegged na unstable coin>>luna, btc nk zilikuwa zinatumika kama reserve, kumbuka walinunua btc za dollar bilioni 1.5 na ndio maana baada ya luna kuyumba na wao inasadikika wakajiuzia zao ile reserve ya btc ndio maana market yote ilicrash
Ngoja nikusaidie, kwanza kabisa terraUst walifeli kwenye apy inayotelewa kama incentive kwa stakers, 20% ni kubwa sana kwa stable coin
Kitaalamu mpaka hapo ni tayari ilikuwa ponzi
Pili elewa kabisa kwamba stable coin au most of currency zinazotumika huku kwenye real world zinakuwa pegged against usd
Protocol ilivyokuwa inafanya kazi ni kwa kuhakikisha kila Ust inavyokuwa deppegged against usd inabidi watrade Ust in exchange to 1$ in luna kwa wale waliowahi kufanya arbitrage trade kwa kutumia flash loans watakuwa wananielewa hapa
Tunaposema Ust deppeged from Usd ina maana imeshuka kwa kiwango chake mfano 1Ust = 0.98$
Kwa kila luna ya 1$ atayoipata yule aliyetrade against ust atakuwa na faida ya 0.02$, kwa kufanya hivi unapunguza circulation ya Ust>>>luna mint
Na ikatokea Ust ikapanda zaidi ya 1$ hivyo basi utaruhusiwa kuitrade against 1$ in luna ambapo kwa kila1$ ya luna utapata faida kiasi na hii ilikuwa inaongeza circulation ya Ust kwenye market>>>Ust mint
Kilichotokea ni withdrawal kubwa ya Ust ilifanyika kwenye curve finance na zile ust zilikuwa traded against usdc hii ilileta hofu kwa stakerswa Ust kwenye anchor protocol, hivyo na wao wakaanza kufanya withdrawal kwenye anchor protocol na njia mojawapo ilikuwa ni ya kupitia Ust-luna pair kwa sababu na luna yenyewe tayari inashuka thamani tayari unakuta mtu akitaka apata ile value ya 1$ ya luna inabidi kiwango cha kumint luna kiongezeke na hii ikawa inaongeza circulation ya luna
Ndio maana zote zili collapse kwa mara moja
Uzuri ni kwamba ust ilishuka mpaka 0.38 na ikarudi tena kwenye 0.98$ kwahiyo nna uhakika raia waliokuwa makini walisalimika
Huwezi ukaingia kwenye crypto usipate hasara.Lazima ujifunze kwa njia ngumu ili kesho usirudie makosa pia huwezi ukamsikiliza mtu hivi vyote utafundishwa sokoni na mimi nilijifunzia huko, na mwisho siwezi nikamlaumu ontario maana anajitahidi kusupport portfolio yake