Crystalline Canopy Theory na gharika la Nuhu

Hahahhaa acha tu, naelewa sasa kwanini Mgambilwa ni mntu alitokwa povu kule kwenye uzi wake yaani nimeumiza kichwa kusoma huo mkitabu afu mtu anasema NAPOTOSHA bila hata kunipa jibu wakati nimeuliza swali !! dah kazi sana
Swali lako ni zuri lakn kwbahati mbya mmb ya mungu n mmb tu ya imani hkuna prove yyt ww km umezaliwa bs amini hvyo lkn ukisema tukupe nondo a up to chee ni ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"....siku ile chemchemu zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu,madirisha ya mbinguni yakafunguka.Mvua ikanyesha juu ya nchi...."Mwanzo 7:11
hapa tunaona kuwa gharika ilisababishwa na vyanzo vitatu,kububujika kwa vilindi(vyanzo vya maji ardhini au chini ya bahari),kufunguka kwa madirisha ya binguni hapa ndipo hayo maji ya juu yalianza kumwagika(bila shaka yalikuwa kama maporomoko) na chanzo kingine ni mvua ya kawaida ambayo ilinyesha kwa muda mrefu.
Kwa hiyo hii theory inaukweli ila haiwezi kuaminiwa kwa 100 kwa sababu haiwezi kuwa proved.
 
Mkuu zitto junior hii mada ni nzuri sana ila nasikitika sana kwa baadhi ya wachangiaji kutoa kejeli bila kutoa hoja za msingi.
Hata mimi nlkua na maswali sana ila haya maji ya juu ya anga nadhani yalikua juu mbinguni. Ingawa sina ushahidi wa hilo

sent using samsung galaxy s8
 
Swali lako ni zuri lakn kwbahati mbya mmb ya mungu n mmb tu ya imani hkuna prove yyt ww km umezaliwa bs amini hvyo lkn ukisema tukupe nondo a up to chee ni ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwanza jifunze kuandika ukaeleweka maana sijui hta umeandika herufi gani hapo.... Pia mie nimeuliza swali MAJI JUU YA ANGA ni nini kama hauna jibu si ukae pembeni wanaojua watakuja sasa kuwahi mada huku ukisema ni mambo ya imani kwani nani hajui biblia ni imani sasa tusiulize swali kisa ni MAMBO YA IMANI?? Sasa mkienda kuhubiri ndio mnajibu watu hivyo wakiuliza swali la biblia??

Kazi kwelikweli
 
Hahahhaa acha tu, naelewa sasa kwanini Mgambilwa ni mntu alitokwa povu kule kwenye uzi wake yaani nimeumiza kichwa kusoma huo mkitabu afu mtu anasema NAPOTOSHA bila hata kunipa jibu wakati nimeuliza swali !! dah kazi sana
Eneo kubwa la Agano la Kale hasa Vitabu 4 vya Torati (Musa), inatumia lugha nyepesi kwa kuwa mlengwa ni Myahudi aliyekuwa mtumwa, ambaye alikuwa masikini, kapuku na asiye na elimu enzi hizo za kutoka utumwani Misri kuelekea Canaan. Shida inakuja kwetu wasomi wa sasa, tunajaribu kutafsiri kifungu kwa kifungu, halafu tuna-relate na uelewa wetu wa kidunia ambao umepatikana kisayansi. Hapo ndo kuna shida.
Wataalamu wa Biblia nao walishakiri wazi kuwa, Biblia iliposema kuwa, Mungu aliumba mbingu na Dunia na vyote vilivyomo ndani ya siku Sita, kamwe hakunaanisha hizo siku za masaa 24. Ndiyo maana kuna uwezekano alikuwa anaongelea namna Dunia ilivyopatikana miaka bilioni 4.5 iliyopita, licha ya kwamba the Big Bang ilitokea miaka zaidi ya Bilioni 12 - 14 iliyopita. Hata Biblia inaposema Mungu akamuumba mwanadamu siku ya Sita, haikumaanisha siku hizo za saa 24, wengi wanakiri kuwa, ni zaidi ya milioni chache (3?) zilizopita.
Kumbuka Biblia inesema kuwa, Mungu alipomaliza kuumba, Dunia ilikuwa haijanyeshewa maji. Hii ni wazi kwa kuwa, baada ya Earth formation miaka bilioni 4.5 iliyopita, ilichukua mamilioni ya miaka (milioni 500) kwa Dunia hiyo kuanza kupoa taratibu mpaka kujitengenezea Atmosphere yake yenye mawingu na Ozone Layer.
So mi nakubaliana kabisa na uchambuzi wao. Hata hivyo, bado kuhusu gharika, siyo kwamba maji yalitoka tu juu. Biblia inaonyesha kuwa, vilindi vya maji vilibubujika maji kutoka ardhini. Hii inaonyesha kuna uwezekano mkubwa sana maji mengi yalitoka chini ya ardhi. Kwenye Conspiracy Theory moja inaelezwa kuwa, maji yaliyomo chini ya Dunia ni zaidi ya mara tano (5) ya maji juu ya uso wa Dunia.

Aidha, Mimi sidhani kama mvua ilinyesha kweli Dunia nzima. Kama ingenyesha Dunia nzima na watu wote duniani wakafa, hiyo inamaanisha sisi wote ni uzao wa Noah. Hapa nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hii hoja. Ukiniambia gharika ilitokea kabla ya 70,000 BC, hapo nitakubali lakini siyo mwaka 2000 BC.
 
Mkuu shida wengi humu wana mahaba ya imani sana yaani ukihoji chochote kwenye vitabu vya dini kwa nia njema tu unaonekana shetani 😀😀 mie nilitegemea hata wataenda download hicho kitabu au hta kuingia google alafu warudi na majibu wameishia kutoa majibu mepesi kazi kwelikweli

anyway ngoja tusubiri wataalam kina mitale na midimu tikakami wa lopelope SALA NA KAZI Son of Gamba wanaweza kuja na majibu ya kueleweka
 
Hivyo basi tukiamini nadharia ni uongo je hayo maji JUU YA ANGA ni yapi mkuu na yalitoweka wakati gani if at all hayakuhusika kwenye gharika??
 
Hivyo basi tukiamini nadharia ni uongo je hayo maji JUU YA ANGA ni yapi mkuu na yalitoweka wakati gani if at all hayakuhusika kwenye gharika??
Mkuu haujasoma kwa umakini,binafsi nakubali hayo maji yalikuwepo na nimesema baada ya madirisha ya Mbinguni "hayo maji yalimwagika kama maporomoka"
Nilichofanya ni kuongezea mambo yaliyopelekea gharika na hayo maji yakiwamo.
Kama hautajali soma tena post yangu ya kwanza
 
mmmh hii ngumu chief,

hoja za watafiti zina-make sense kwa kiasi fulani.....na Mungu pia inawezekana labda alitumia uwezo wake wa kutoshindwa kitu kufanikisha hilo.
 
Hahahhaa acha tu, naelewa sasa kwanini Mgambilwa ni mntu alitokwa povu kule kwenye uzi wake yaani nimeumiza kichwa kusoma huo mkitabu afu mtu anasema NAPOTOSHA bila hata kunipa jibu wakati nimeuliza swali !! dah kazi sana


JIWE kaleta taabu sana kwenye jamii mkuu wangu...yaani kila unayekutana naye ni HASIRA HASIRA HASIRA...wakati mwingine mtu maneno yanamtoka tu ila akitulia halafu ukamuuliza kwa utaratibu...kulikoni ndugu yangu lile povu lote lilikuwa la nn???...hata mwenyewe anashindwa kukuelezea kilichomkuta...(catalyst ya povu....JIWE) kwa hyo mkuu wakati mwingine inabidi kuwasamehe tu.....Huyu JIWE huyu....acha tu.
 
Mkuu zito you are the best unajaribu kufungua akili za watu lakini siku zote utumwa wa dini ni mbaya sana hata umwambie vipi ni ngumu kukuelewa


ila amini nakuambia hakuna kitabu kibovu ktk biblia kama kitabu cha genesis yaan totally shizophrenia
 
Hakuna ukosefu wa maarifa mkubwa duniani kama kusema hili jambo limesumuliwa tu si la kisansi hivo halifai, lakini mtu huyo huyo anaamini bing bang theory, continental drift, Darwin theory nk ambavyo vyote ni mawazo tu ya watu wengine, kama sayansi inaweza kuprove kila kitu hebu nisaidie kuprove uwepo wa NATURE ambayo sayansi inaamini kuwa ipo
 
Niliwahi kusikia(kusoma) toka kwa bwana mmoja kuwa baada ya dunia kupigwa na Asteroid miaka zaidi ya 65, 000,000 iliyopita athari zilizojitokeza baadaye ni pamoja na kuuwawa kwa viumbe wengi (mass extinction), matetemeko makubwa ya ardhi, kuongezeka kwa joto la dunia, kutanda kwa wingu kubwa la gesi ambalo lilifunika dunia yote na hivyo kuifanya ipoe sana kwa kuwa hata mwanga wa jua ulizuiwa kwa kiasi kiasi kikubwa na kwa muda mrefu kufika duniani.
Inawezekana kupoa huku kulipelekea the so called “ICE AGE” na baadaye kufuatiwa na mvua kubwa kunyesha kutokana na lile wingu kubwa lililokuwa limedanda juu ya duia. Hapa linazungumziwa wingu lililosababishwa na asteroid impact, wingu lililoweza kuzuia mwanga wa jua kuifikia dunia kwa muda mrefu mpaka kusababisha Ice age na baadaya the so called “GHARIKA”.
Theory hii pia naiona una mashiko yake japo sina hakika wa uwiano uliopo kwati ya muda wa kwenye biblia unaokadiria umri wa dunia kuwa miaka 6000 na ule wa kisayansi unaokadiria kuwa miaka 4.543 Bilioni.
Asante.
 
Jamani mambo ya Mungu hayachunguzwi kwa akili hizi za kibinadamu. Lazima uende umuombe Mwenyezi Mungu akupe neema ya kukufunulia atakayo. Haya tunayo ya jua kwa kujidanganya eti ni sayansi ndiyo huyu Mungu aliye tufanya tuyajue kwa kutupa ubongo/akili. Hii sayansi ambayo tunaitumia kujaribu kuhoji na kumkosoa ni Mungu aliyetupa huo uwezo tuwenao na kama asingetaka wala tusingekuwa nao. Kumbuka kilichotokea katika ule mnara babeli.

Tujue tu kuwa Mungu ndiye muweza wa yote na ndiye muwezeshaji wa yote. Haiwezekani eti sayansi tena inayotegemea akili za mwadamu aliye umbwa na Mungu ishinde uwezo wa Mungu au itumike kutilia mashaka uumbaji wa Mungu.

Mimi na omba nikuambie kitu, Biblia au Maneno ya Mungu Matakatifu imeongelea yale Mungu aliyo taka tuyasikie kwa utashi wake yeye basi.

Ni kuulize kwenye Biblia unaweza kuniambia maji au kiza viliumbwa vipi? Hata kwa hiyo sayansi ambayo mnaitumia kumtilia mashaka Mungu inaweza kutuambia giza liliumbwa vipi na vilivyo liumba hilo giza vilitokana na nini?

Wanasayansi wakiwa wamefika ukomo wa uwezo wao watakuambia utafiti unaendelea hawakuambii tumeshindwa katu. Unaendelea mpaka lini? mpaka hapo ufumbuzi utakapo patikana. Hizo nguvu za ufumbuzi mnazozisubiria zipatikane mnategemea kuzitoa wapi? Utaambulia blabla tu za akili za mwanadamu tena aliye jawa na kiburi cha uzima. Hivi kwa nini wanadamu wanaojidai kugundua mambo kibao wanalizwaje na kifo? Uchungu wa kifo umemshinda vipi mwanadamu? Hata baada ya Mungu kumjalia kuona na kufika sayari za mbali?
Mungu anasema yeye jina lake ni " NIKO/YUKO AMBAYE NIKO/YUKO". Hana Asili/Mwanzo wala Mwisho/Hatima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…