Crystalline Canopy Theory na gharika la Nuhu

Crystalline Canopy Theory na gharika la Nuhu

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za mchana wana JF natumaini wote humu wazima basi moja kwa moja niende kwenye mada husika.
570_file0081ma10357717-00101.jpg

UTANGULIZI
Wakati nasoma biblia nikakutana na mstari huu ambao ulinipa maswali sana

Mwanzo 1
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo
.

Mstari huu unaeleza kuwa kulikuwa na maji juu ya anga na chini ya anga hivyo nikajiuliza sana hayo maji ya JUU ni yapi?? Kwa haraka nikafikiri ni mawingu ila muandishi wa zaburi akapigia msumari kuwa ni vitu viwili tofauti

Zaburi 148:4
4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu,Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 Na vilisifu jina la BWANA,Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.


Hapa kaweka wazi kuwa kuna maji juu ya dunia na hapa chini kaonyesha ni tofauti kabisa na mawingu tunayofahamu

Zaburi 147:8
Huzifunika mbingu kwa mawingu,Huitengenezea nchi mvua, Na kuyameesha majani milimani

Baada ya sintofahamu hii Wakati natafuta ukweli wa mambo, nikakutana na nadharia hii ya crystalline canopy theory ambayo ilipewa nguvu na wanatheolojia Dk kent hovind na Dk Henry morris muasisi wa movement ya young earth creationist.
canopyspace.jpg

NADHARIA
Kwa kifupi tu nadharia hii inaeleza kwamba anga la Dunia kabla ya gharika la Nuhu ilikuwa imezungukwa na mzingo wa maji yaliyotajwa hapo juu na kwamba hayo maji ndio yaliyokuja kutumika kwenye gharika kwa Mungu kuangusha mzingo huo kwa mfumo wa mvua kupitia mstari huu

Mwanzo 7:11-12
11........ madirisha ya mbinguni yakafunguka.
12 Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku
.

KAZI YAKE
1. Kuwa na hali ya hewa moja dunia nzima hivyo kuepusha uwezekano wa hali za hewa ya maeneo tofauti kuingiliana ambayo ingesababisha mafuriko,vimbunga,n.k

2. Kazi ya pili ni kuiwekea mzingo dunia ili kuiepusha na mashambulizi ya mionzi mikali ya Jua na hii ilisaidia kuongeza umri wa kuishi wa wanadamu.

3. Kazi kubwa zaidi ni pale ilipotumika kuangamiza dunia nzima kwenye gharika la Nuhu ambapo ilileta mvua kubwa iliosababisha kizazi chote kufutika.
10a.jpg


HOJA ZAO
1. Mvua ya siku 40 mfululizo ingehitaji maji ya kutosha ambayo mawingu yakawaida yansingetosheleza maana kijiografia tu haiwezekani pande zote za dunia ziwe na mvua kwa wakati mmoja kama ambavyo haiwezekani jua kuwaka eneo lote la dunia kwa wakati mmoja na kwamba kwa ushahidi wa kisayansi anga letu lote hili likigeuka mvua maji yatajaa dunia nzima kwa urefu wa inchi 1 pekee!! Hivyo wakasema hili lingewezekana kupitia hayo MAJI yaliyokuwa juu ya dunia maana yalikuwa mengi mno!!

2. Pia nadharia inasema hakuna mahala Mawingu yametajwa kabla ya gharika hivyo hiyo mvua ilitokea wapi bila mawingu kuwepo?? Hivyo huenda ni hayo MAJI ya juu ya dunia ndio yalitumika.

Mwanzo 9
14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni

3.Pia inasema hakuna mahali mvua imetajwa kabla ya gharika sababu hapakuwa na mawingu wala mfumo wa kawaida wa hali ya hewa kama sasa hivyo huu MZINGO ulikuwa unaleta unyevu nyevu na miti kuota kwa haraka kupitia umande hivyo hiyo wakahoji hiyo mvua ilitoka wapi wakati wa gharika kama sio hayo maji ya JUU ndio kutumika??

Mwanzo 2
5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi.

Kuhusu unyevu;
Mwanzo 2
6. ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

4.Hoja nyingine ni kwamba kwenye Biblia wanadamu kabla ya gharika walikuwa na maisha marefu kuliko wa baada ya gharika sababu walioishi kabla ya gharika walikuwa chini ya uzio huu hivyo mionzi mibaya ya jua ikawa haiwapati na hivo kuwasaidia kuishi zaidi.
FountainsOfDeep2.gif


USHAHIDI WA KISAYANSI
1. Imegundulika na wanasayansi kwamba zamani kulikuwa na oxygen content ya 35% duniani ilihali kwa sasa ni 21% pekee hivyo hii nadharia inasema kutokana na uwepo wa MZINGO huu basi hali ya hewa ikawa na oxygen content kubwa zaidi hivyo kusupport uwepo wa wanyama wakubwa na wanadamu wakubwa (wanefili) waweze kupumua vizuri. Hoja hii imetokana na kugundulika kuwa Mapafu ya dinosaur na viumbe wengine wakubwa wa kale walikuwa na mapafu madogo na nyenzo za kupumulia nyembamba hivyo wasingeweza kuishi sahivi ambapo kupumua ingekuwa shidia kutokana na MZINGO huo kuondoka na oxygen kupungua % zake hivyo hata waliopona kwenye gharika walipoteza kizazi chao hapo.

2. Pia kugundulika kisayansi uwepo wa ice age ambapo barafu ilitanda dunia nzima huko miaka mamillion iliopita hivyo wakajengea hoja kwamba barafu ya huo MZINGO ( barafu kutokana na baridi la nje ya dunia kupiga hayo maji) ulipoyeyuka na baadae kugeuka maji na kumwagika duniani kwa mfumo wa mvua ulisababisha hali ya hewa kubadilika na kuwa na UBARIDI sana hivyo kuweza kuwa chanzo cha ICE AGE (ukizingatia mpaka leo wanasayansi bado hawajapata sababu conclusive ya kilichosababisha).

3. Pia wanasayansi waligundua dunia ya sasa haipigwi na jua kama dunia ya zamani yaani jua lilipiga dunia 30% dhaifu kuliko sasa, hivyo wakajengea hoja kuwa huenda kuna MZINGO ulikuwa unapunguza nguvu ya jua kumulika dunia hivyo kuhalalisha uwepo wa MZINGO huo.

HITIMISHO
Baada ya kusoma mstari huo na baadae kupitia nadharia hii bado nimebaki na maswali mengi nikaona nije kwa great thinkers humu tuchambue pamoja

1.Je nadharia hii ni ya kweli

2. Na tukiamini si kweli basi tujiulize maswali yafuatayo

je hayo maji JUU ya Anga ni yapi?
Kazi yake ilikuwa nini?
Na yalipotelea wapi au kama yapo yakowapi??

SOURCE: The genesis flood by Dr Henry Morris

Screenshot_2018-08-27-19-36-36.png
 
Kuna mmb mengn ni kuumiza tu kchwa lkn hii nadharia cyo ykweli imejaa simuliz na taarifa Za kusafikika na kuunganisha maneno ykweny bible ili story yao iende sw..hv nani leo atakuja na majbu sahh y swali lko?kiufupi tu hlo jmbo lingetokea kiisayansi leo sayans ingeprove lkn kwkuwa limesimuliwa na mmb y kiimani nkushauri tu inatosha kuamini unavyoamn mara zote mmb ydini huendeshwa na imani na s mmb y kuprove

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika muktadha mbalimbali yako maneno ambayo hurejezea maana tofauti na ile ya lugha ya kiebrania.bandiko lako lote Ni uzushi na limejaa JUMBE m'bovu.jifunze kwanza biblia imebeba ujumbe gani usipotezwe na theory za mataifa wanaompinga MUNGU.uhitaji wa KIROHO na utafutaji wa hekima ya kibinadam Ni vitu viwili vinavyokinzana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Comment m'bovu.hukupaswa kuwepo jamiiforum.hapakufai level zenu watu wa hivi Ni Facebook.nako mnachodhani mnakitafuta hamtakipata.ni lini mtaacha kuacha kuandika Mambo yasiyo na THAMANI?

Sent using Jamii Forums mobile app

we ulitaka niandike nini mkuu?? jamii forum sio yakwako ukitaka hivo tengeneza mtandao wako basi
 
Kuna mmb mengn ni kuumiza tu kchwa lkn hii nadharia cyo ykweli imejaa simuliz na taarifa Za kusafikika na kuunganisha maneno ykweny bible ili story yao iende sw..hv nani leo atakuja na majbu sahh y swali lko?kiufupi tu hlo jmbo lingetokea kiisayansi leo sayans ingeprove lkn kwkuwa limesimuliwa na mmb y kiimani nkushauri tu inatosha kuamini unavyoamn mara zote mmb ydini huendeshwa na imani na s mmb y kuprove

Sent using Jamii Forums mobile app

Kajifunze kuandika kwanza.. Hii mada si saizi yako...
 
Kuna mmb mengn ni kuumiza tu kchwa lkn hii nadharia cyo ykweli imejaa simuliz na taarifa Za kusafikika na kuunganisha maneno ykweny bible ili story yao iende sw..hv nani leo atakuja na majbu sahh y swali lko?kiufupi tu hlo jmbo lingetokea kiisayansi leo sayans ingeprove lkn kwkuwa limesimuliwa na mmb y kiimani nkushauri tu inatosha kuamini unavyoamn mara zote mmb ydini huendeshwa na imani na s mmb y kuprove

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu sayansi ni ngumu kuprove mambo ya dini ndio maana nimeweka angalizo hapo mwishoni kama nadharia hii ni ya uongo je biblia inaposema MAJI JUU YA ANGA inamaanisha maji gani??

Hilo ndio swali langu
 
Katika muktadha mbalimbali yako maneno ambayo hurejezea maana tofauti na ile ya lugha ya kiebrania.bandiko lako lote Ni uzushi na limejaa JUMBE m'bovu.jifunze kwanza biblia imebeba ujumbe gani usipotezwe na theory za mataifa wanaompinga MUNGU.uhitaji wa KIROHO na utafutaji wa hekima ya kibinadam Ni vitu viwili vinavyokinzana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu kuliko kejeli za kusema ni upotoshaji unaweza kutusaidia maana ya MAJI JUU YA ANGA ambayo sio mawingu?? Kumbuka walioleta nadharia hii wana PhD ya theolojia hivyo sidhani kama hawajui kutafsiri biblia unless unafahamu kitu ambacho hawafahamu tufahamishe hapa tuelimike
 
Unajua tukianza kujadili kwa kujiulza jee bible inaposema maji juu ya anga imekusudia nn hatutopata jibu kwasabb vtabu vya imani havijazungumzia mmbo ya asili na namn inavyotokea mfano mdg ukiambiwa mungu aliumba bnadam usfkrie aliumba tu adamu na eva pekee ila aliumba viumbe vyote lkn ukiichunguza bible na qurani huez kukuta kwmba mm na ww tumeumbwa lini mana utaambiwa tu tumezaliwa bs ndyo mwsho wa maandko ayo y mm naww kuumbwa na mungu ni imani tu ambyo tumevshwa lkn hkuna mtu mwenye ushahidi lini..ss tukirudi kweny point y swali lko mzee hakuna jibu kwmba jee asili ya maji hasa mungu aliyatoa wapi na ilkuaje maji yakakaa juu ya anga ila ukihoji sana utajibiwa kiimani na si kw kuja mtu kuprove so nkuombe tu uliza mmbo ambyo tutakujib kw kuprove uelewe mmb y uumbaji hakuna mweny ushahd nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ndio maana nimeuliza ili mnaofahamu mnisaidie je Biblia inaposema maji JUU ya ANGA ni maji gani hayo?? Nisaidie hapo

usipokuwa na moyo mgumu unaweza ishia tukanana na watu bure..
😀 😀 😀

mada imewekwa mezani ili watu wapate kuchangia ila mtu anatoka from no where anakuclash vibaya..

ujue nacheka tu hapa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usipokuwa na moyo mgumu unaweza ishia tukanana na watu bure..
😀😀😀

mada imewekwa mezani ili watu wapate kuchangia ila mtu anatoka from no where anakuclash vibaya..

ujue nacheka tu hapa..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahhaa acha tu, naelewa sasa kwanini Mgambilwa ni mntu alitokwa povu kule kwenye uzi wake yaani nimeumiza kichwa kusoma huo mkitabu afu mtu anasema NAPOTOSHA bila hata kunipa jibu wakati nimeuliza swali !! dah kazi sana
 
Back
Top Bottom