KERO CT scan na MRI kwanini mgonjwa hapewi option ya kuchagua?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa hyo unajua mambo ya afya ww lakini mionz Inapigwa na madokta au na sindano u accompanied na madokta mpk nasoma hilo neno madokta ww unaleta habari za kusikia kutoka kwa wamama walio nje ya dirisha lako achana nazo hzo no taalum za watu tofaut sio madokta unavoita ww
 
Yy anawaita madokta wanajifungia kuogopa mionzi hahaaa jf jf
 
Kama wewe mgonjwa unadhani kazi ya kutibu ni rahisi na unaimudu basi ungetulia zako nyumbani na kujitibu wewe mwenyewe na ukipenda uchague na kipimo cha kujipima.


Ukiamua kwenda hospitali, basi acha ujuaji, hizo blah blah za nini upimwe muachie Daktari mwenyewe, unayo haki ya kujadiliana naye, na ukiona anachotaka kukupima haiko tayari basi unayo haki ya kukataa, lakini HAUNA HAKI YA KUMLAZIMISHA AKUTUME UKAFANYE KIPIMO FULANI AMBACHO WEWE UNAKITAKA TU.
 
Hivi hamuoni kua kunamadhara yakumpiga mgonjwa X-ray kilamara ?? Tusiishi kwakuangalia Leo tuu yamgonjwa .hiyo mionzi nihatari kwaafya yamgonjwa kwabadae

Mimi nilishakua namgonjwa mwenye tatizo lakucheza kwa disk za UTI wa mgongo aliambiwa akafanye x-ray ila niliongea nadaktar akanibishia sana upande wakipimo alichopendekeza ila baada ya kumpulizia mpunga akabadilishiwa akawekwa kwenye MRI namajibu yalipatikana naukumbuke wakati huo alishaniambia kua hilotatizo haliwez gundulika kwa MRI
 
Inategemea hapo kipi kinawapa hela nzuri.
Umewaza kitoto sana.
Daktari anayefanya kazi katika hospitali ya serikali, anapokuwa mama mjamzito ambaye anatibiwa bure kwa msamaha, halafu Daktari akachagua huyo mgonjwa akanye kipimo cha gharama kubwa hapo hospitalini.
Embu niambie huyo Daktari anapata faida ipi kubwa?
 
Wajifanya wanajua kila kitu, wamekariri ndiyomaana tuko nyuma sana kwenye sekta ya afya.
 
Kajifunze kwanza kuwa CT Scan, X-ray & MRI hazitumiki Kupima bali Kupata picha, Alafu ndo uanze kuuliza juu ya uamuzi wa kitaalamu kutoka kwa Daktari.
 
Sio kwamba daktari anapangiwa nikushauriana na daktari sababu kwahyo matatizo ukiwa njee ya nchii unauhuru wakushauriana na daktari, madaktari anakupa faida na hasara na gharama wewe ndiounachagua unapendakipi naunatia Saini kabisa kwenye fomu kua umekubali kulingana naelimu ulopewa.

Kinachobaki nikwawataalamu wakupiga picha sehemu husika
 
Hata Tanzania Tinafanya hivyo ila Inategemea Na nataka Nipime nini

Ngoja Niwape somo Kidogo maana Hamjui na Hamtaki kukubali kuwa Hamjui..

Kwenye MRI mara Nyingi Tunaangalia Pathology za Tishu laini (soft tissues) kama ubongo, uti wa mgongo, misuli, mishipa ya damu, na baadhi ya viungo, Na Hii Ndo inatupa Picha nzuri za Soft tissue na Inapiga Picha kwenye mfumo wa Mulplanar ambayo inasaidia kuona picha kwenye Pande zote yaani 3D


KWAHIYO kalilini hili kuwa MRI hufanya Uchunguzi wa magonjwa ya ubongo, uti wa mgongo, majeraha ya misuli na viungo, uvimbe, mishipa ya damu.,, Tu na Hauwezi kuhusika na Ukaguzi wa Mifupa sijui kana naeleweka..

KwenyE CT scan..
Inawealza Kufanya kazi kama MRI ila tofauti yake ni kwamba CT inapima Mifupa na Kingine kwenye CT tunaangalia sana Mfupa, mapafu, viungo vya ndani, mishipa mikubwa, uvimbe, damu kwenye ubongo.na Ndo inakuwa Prefarable kwenye Hudkma za Dharura kwa sababu ni ya Haraka ,, Ina hasara Moja Kuwa CT Scan inatumia Mionzi mikubwa sana Kuliko XRAY na Kuna wakati huwa tunatumia contrast na contsrast inaweza Kuleta matatizo ya Figo auu Allrgic rxn kwahyo ndo maana haiwezi kuwa Chagua la Kwanza ila Inawwza Kugundua Majeraha makubwa, kugundua kansa, magonjwa ya mapafu, magonjwa ya tumbo, kugundua damu kwenye ubongo.Ila haiwezi kupima Soft tissue Kama MRI ba Kupima magonjwa ya Ubongo na Neural..

Kwahyo Kila Kipimo Kiko Tofauti
 
Kajifunze kwanza kuwa CT Scan, X-ray & MRI hazitumiki Kupima bali Kupata picha, Alafu ndo uanze kuuliza juu ya uamuzi wa kitaalamu kutoka kwa Daktari.
Kwahyo nyie kama madaktari mnasema MRI haiwezi kutoa picha ya hard tissue??
 
Asante umetutoa ushamba walao tumejua tofauti zake
 
Kama umesoma maelezo yangu hapo juu na kuelewa huwezi kuandika hayo tena.

Mimi nimekwambia, kidaktari, kuna factors nyingi zinatazamwa ili kuamua ni kipimo kipi kinafaa kwa mgonjwa wake. Sio jukumu la mgonjwa kuamua (unless daktari akupe pendekezo la kuchagua) ni kipimo kipi ufanye.

Sasa kama ulimpa rushwa Daktari ili ubadilishiwe kipimo cha kufanya, hapo inaashiria nini? Huo ni uhuni tu, sio taaluma ya udaktari. Kwa lugha nyingine, ungeweza hata kumwambia daktari usifanye kabisa kipimo na angekubali. Hiyo inamsaidia vipi Daktari katika kutaka kufumbua fumbo la ugonjwa na tiba kwa ugonjwa wako?

Narudi pale pale, jukumu la kuamua upimwe na upimwe kipimo gani hilo ni jukumu la daktari kwa 100%, maana kipimo kinarakiwa kimsaidie yeye Daktari kujua vyema namna na kutatua tatizo lako.
 
bro binadamu tunaenda kusiko,tunataka kuingilia kazi za madaktari!!!!!
 
Hapana Tatizo la Mgongo Linawwza Kupimwa na MRI ...
XRay haiwez kugundua na Kuonyesha soft tissue Kama Disc za Mgongo ila MRI
 
Kwahyo nyie kama madaktari mnasema MRI haiwezi kutoa picha ya hard tissue??
Haiwezi kutoa Picha yenye details muhimu & Za kutosha ukilinganisha na CT Scan.
 
Nisawa upo vizuri ila wakati daktari anaangalia kipimogani kitamsaidia kupata majibu kirahisi pia mgonjwa anahaki yakuangalia kipimogani hakitomletea madhara kwa baadae sababu mgonjwa akipata majibuyake yeye kashamaliza kazi ila wewe ukipata madhara nijuuyako na maishayako daktari hausiki tena.

Nivyema kama daktari Hana ustadi wakusoma kipimo akuandikie rufaa yakwenda sehemu ambayo wanauwezo nasio yeye kunganganiza
 
Hapana Tatizo la Mgongo Linawwza Kupimwa na MRI ...
XRay haiwez kugundua na Kuonyesha soft tissue Kama Disc za Mgongo ila MRI
Sasa kwanini madaktari wananganganiza wakati anajuakabisa haiwezekan??
Au niukosefu wataaluma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…