KERO CT scan na MRI kwanini mgonjwa hapewi option ya kuchagua?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna Mgonjwa Mmoja Zamani Kidogo aliwahi Kuja Kutibiwa na Mimi Akaanza Kujifanya Mjuaji wa Kujua Sana Vipimo..
Anafika ananiambia..

"Daktari najisikia Kuumwa sana Naomba Nipime vipimo vifuatavyo akavitaja...."

Nikajaribu Kumuelimisha Lakini wapi Kaja Hana Flexibility kaja Fixed sana..sasa Nilichoona Ni kumfundisha Adabu..

Nikaandika Vipimo vyote anavyotaka na Nikaagiza Vifanyike Baadae majibu ya Vipimo vyake Vikaja Negative..

Nikampa Majibu yake Bana Vipimo vyako Vyote ni " Negative"

Akakaa Kwa Muda akaanza Kuniambia Daktari sasa Unahisi Naumwa Nini .....
"Nikamwambia kiukweli Kabisa Hata Mimi Sijui"

Akasema sasa kwanini Hujui Nikamwambia Nitajua Wakati Mimi sio Nilioagiza Vipimo?..
Nikamuuliza Unajua Kwanini daktari anaagiza Vipimo? Daktari anaagiza Vipmo kwa ajili ya Makusudia matano..

Kuconfirm His Diagnosis
Kurole out His Differential
Kuexclude other cause
Kurole out The Complication

Sasa Hapo Mimi sijaagiza Hata kipimo maana Hata DX Yako siijui..

TUjifunze kujua Sio kila kipimo ni Kwa ajili ya Comfirmation
 
Haki iyo utaipata endapo kutakuwepo mbadala wake wenye manufaa sawia.
 
Sasa kwanini madaktari wananganganiza wakati anajuakabisa haiwezekan??
Au niukosefu wataaluma
VIzuri zaidi Ungemuuliza Daktari kwanini anafanya Hivyo..
Kwa sababu kipimo kina Sababu zake..

Kuna Kupima kuthibitisha ugonjwa(Confirm diagnosis)

Rule out differential diagnosis
Rule out complications
na kupima kwa ajili ya Risk assessment

Kupima Kila Daktari huwa na Sababu zake
 
Hapo upo sawa ila kitu chakuangalia haiwezekan mgonjwa anakuja anakwambia minaumwa mgongo miaka minne nimepiga x-ray mara tano nimetumia dawa lakini siponi

Nilipofikia Sasa miguu inakufa ganzi nashindwa kutembea na kuinama napata changamoto

Nimekuja kwako tushauriane sababu kabla sijaja hapa nimepita kwenye hospital ya wahindi wakaniambia kwa idadi ya x-ray hawawezi kukufanyia tena naisitoshe hujapona ila kwahilo tatizo nenda hospital yetu ipo sehemu flani au kama huna nauli yakutosha nenda sehem flani Kuna hospital yenye icho kipimo waelezee watakufanyia MRI ilikujua tatizo kiundani .
Unafika pale unajieleza daktari anakufanyia X ray alaf anakwambia inaonesha huna shida kafanye mazoezi ilimwili ukae sawa πŸ˜‚

Mwisho wasiku unamua kwenda kwa wahindi wanakuambia faida na madhara kwakila kipimo,unapewa na gharama zakila kipimo.
Wanakutibu unapona wakati wabongo wanakuzungusha tuu miaka yote wanashindwa kukwambia kua daktari wetu. Bingwa kasafiri yupo masomoni
 
Mfano:
Mimi ninaishi huku kijiji kimoja ndani ndani Namtumbo, muda mchache uliopita nimepata ajali ya bodaboda na kuumia mguuni na kuna kidonda kinatoa damu, nimefika kituo cha afya hapa kijijini, Daktari wangu ameniambia huenda nimevunjika pia mfupa wa mguu, na hapa Daktari kanipa huduma ya kwanza chap kisha ameniambia kuna hospitali ya mission hapo kijiji cha jirani kanituma niende chap nikafanyiwe X-ray gharama ni kama shilingi Elfu 20 tu. Hapa mfukoni nina kama elfu 50 tu, nategemea bodaboda inipeleke na kurudisha kwa elfu 10, kipimo elfu 20, dawa nimeambiwa nitapata bure, huduma zingine elfu 10, jumla yote elfu 40.

Sasa nimemcheck kwa whatsapp msela wangu mmoja yuko Canada (nilisoma naye sekondari enzi hizo) kwa sasa ni Daktari bingwa wa mifupa kaniambia hapo ni vyema nikafanya kipimo cha MRI au CT scan (kulingana na Daktari atakavyoona) kuliko X-ray. Nimeuliza hapa nikaambiwa hivyo vipimo ni mpaka nisafiri Mkoani (Ruvuma) (safari ya siku mbili nauli ni kama elfu 30) au Muhimbili (Dar) safari ya siku nne mpaka kufika na nijipange kwa nauli ya laki moja , na nijipange kama laki tatu hivi kuweza kufanyiwa kipimo cha MRI au CT scan. Sasa nipo njia panda kweli kweli.

Nishauri hapo.
 
Kwakua huna ela tulia hapohapo huna uchaguzi ila kuamakini sababu wanatabia yakukata miguu ilikurahisisha kazi
 
Matibabu uliyoyapata yalikusaidia ndug?
 
Kama umeishi Norway ni kwa nini nyama ya Kiti moto bei chee, nyama ya ghari sana?
Wakati Tanzania nyama ya Kitimoto bei juu?

Nataka kuona kama kichwani una akili au kasha.

Pili hospitali gani Norway umekuta wagonjwa wamedamka saa 10 usiku kuwahi namba ya kumuona daktari saa 4 asubuhi au atakaa kutwa nzima hospitali kusubiri foleni?
 
Sasa wewe umebandika hivyo hivyo jinsi ulivyouliza kwenye ChatGPT?
 
Pole sana.

Unaweza kuchagua kama unajitibu na unajua unachokitafuta au unacholenga kuona kwa kipimo husika.

Vinginevyo mwachie daktari akutibu kwa kukufanyia vipimo kwa sababu anajua anacokifanya, ni kazi yake kukusikiliza kuamua vipimo na kisha kukuelewesha sababu na umuhimu wa kipimo husika.

X-ray, CT scan na MRI ni vipimo ambavyo kila kimoja kina uwezo wake wa kuweza kusaidia kubaini tatizo mwilini, kwa hiyo kila kimoja hufanyika kulingana na hali ya mgonjwa na kile ambacho daktari anataka kutambua.

Mfano mtu aliyevunjika mfupa inaweza kuoneshwa na x-ray, hivyo hahitaji MRI lakini mwingine kama mchezaji mpira (footballer) aliyeumia misuli huhitaji MRI ili kubaini tatizo la misuli iliyochanika kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa x-ray.

Kila la kheri.
 
Povu linakutoka daktari uchwara.
 
Kwahyo MRI haiwezi kuona mfupa uliovunjika??
 
Kwahyo MRI haiwezi kuona mfupa uliovunjika??

Inaonesha, lakini kwa nini ufanyiwe kipimo cha gharama ya juu sana kwa tatizo ambalo kipimo cha kawaida kitaonesha bila shida yoyote? Mfano hospital nyingi x-ray ni kati ya Tsh. 15,000 hadi Tsh. 20,000, tofauti na MRI ambayo gharama yake si chini ya Tsh. 300,000.
 
MRI kinauwezo wakupima vituvyote iwaje usipendekeze hicho kama mgonjwa karidhia kulipia?
πŸ˜‚πŸ˜‚ Mnakuja kudiscuss vitu hamjui na mnaforce. Unajua kuwa X-ray,CT zinatoa better view za mifupa kuliko hiyo MRI unayoililia livha ya kuwa Ina GHARAMA kuliko ata CT na X ray. MRI ni best solution linapokuja suala la soft tissues na internal organs tu.
 
Asante kwa jibu lakini narudi kwa swali tena je ? Hayo uliyosema kua CT inafanya ukimtumia MRI huwezi pata majibu ??
Ungeenda kusoma health faculties ungekua kiundani kwann MRI ni Kwa ajili ya tissue laini . Wewe umeambiwa tu haitumii mionzi ukagutuka huko ndo best option
 
Mkuu Umemaliza ,somo zuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…