Si lazima CDM kupiga kelele barabarani kila siku ndio watu wajue kwamba wanafanya kazi kubwa kiasi gani kuhusu uwepo wa Katiba mpya nchini mwetu.
Mtu wa Pwani, wewe vuta tu subira utaona kazi inayofanyika pale CHADEMA. Pili, ikumbukwe kwamba CUF, TLP, CHADEMA na vyama vinginevyo vyote ni vyama vyetu sisi wenyewe Wa-Tanzania.
Hatuna sababu ya kutazamana kwa jicho la uchoyo kwani lengo letu ni moja kuboresha maisha ya nchi yetu na mteja wetu sote ni mwananchi wa nchi hii. Kwa msingi huu, mafanikio ya CUF au TLP kamwe hainiumi wala kushindwa kuyatolea pongezi penye ustahili huo.
Lakini kwa kufanya hivyo hakuniondoi CHADEMA hata kidogo. Na hata kuvikosoa vyama hivi haimaanishi kuna chuki isipokua FISADI na WAKUMBATIAJI WAO ni maadui wakubwa wa taifa letu.
Ukomavu kisiasa unahitajika.