Mkuu,
Topical haonekani kama ni "mjinga". Anaonekana yuko kazini, kazi ya propaganda.
Ukipitia michango yake katika threads tofauti utagundua hili. Anajaribu kuwavunja nguvu, moyo watu waaamini kuwa wanachodai hakina tija ni bora kuendelea na kile kilichopo.
Kama hafanyi kazi ya propaganda ya chama chake, yaani,kuwakatisha watu tamaa basi Topical angekuwa anakuja na ushauri mbadala au fikra mpya ya nini kifanyike.
Sasa kufanya propaganda si ujinga ni kazi yake (yawezekana yeye ni spin doctor, propangandist, polilitical party strategist au PR officer wa mrengo fulani.)
Kwa hiyo, anajaribu kuwatoa watu katika hoja, au kuwapotezea focus badala ya kujadiliana kwa hoja, basi kwa vile anatumia provocative language watu wataanza kumshambulia, kumkejeli,kumtusi. Kazi yake inakuwa imefana. Anakuwa amefanikiwa.
Mpeni masuali magumu ili ayotolee majibu hiyo ndiyo dawa yake.
Akiingia mitini, mutakuwa mumejua lengo lake ni nini.