Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

kifupi si pemba tu ata hapa unguja ccm inafosi watu kuipenda na mwisho ya yote ni hatari kubwa ya machafuko inayoinyemelea zanzibar
 
Pasco,inamaana CUF wakiamua kushiriki na wakashinda tena je Uchaguzi utarudiwa???Maana CCM haijawahi kushinda huko ni kulazimisha kushinda.CCM ikishindwa tena kwa kishindo Uchaguzi utarudiwa tena???
 
Pasco CCM haijawahi kushinda Z'bar, je wakishindwa tena Uchaguzi utarudiwa??? Je,Leo Maiga akienda Burundi ati kusuluhisha ugomvi wa Uchaguzi ataambiwaje???Je,Magufuli na Chama chake wanasifa ya kwenda kutatua migogoro kwenye nchi nyingine???
Mwenye akili timamu hatakubaliana na marudio ya Uchaguzi sababu Tanzania haina sifa ya kukemea migogoro ya uchaguzi.Mahiga hana haki wala sifa ya kwenda Burundi na kumshauri Nkuruzinza na Chama chake.
Poleni wanaccm kukubali kushindwa ni heshima.Safari hii kubalini mmeshindwa kwa kishindo
 
Yeah! Kampeni nimkupoteza fedha na kuwapandisha mori wananchi. Vita ingezuka wakati wa kampeni
Nchi ya CCM hii milele.
Lkn je wakiondoka hawa wazee wanaolazimisha nyie vijana mtaweza kuishikilia milele?

Hakuna kazi kubwa kama kukaa na mtu mjinga
 
Pasco,inamaana CUF wakiamua kushiriki na wakashinda tena je Uchaguzi utarudiwa???Maana CCM haijawahi kushinda huko ni kulazimisha kushinda.CCM ikishindwa tena kwa kishindo Uchaguzi utarudiwa tena???
Macho yote ya dunia yatakuwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar, hivyo CUF ikishinda tena this time itatangazwa!.

Kuna hoja kuwa siku zote CUF huwa inashinda uchaguzi wa Zanzibar lakini haitangazwi!, kama hili ni kweli, then lazima kuna sababu kwa nini CUF washinde na wasitangazwe!. Sasa bila kuzijua hizo sababu, watu humu watabaki wanapga tuu kelele!. Watu wangezijua hizo sababu, kisha wajiulize kama siku zote CUF anashinda lakini hatangazwi kwa sababu abc, sasa ili this time shinde na kutangazwa, then hizo sababu nazo ziwe zimebadilika!.

Niliwauliza wenyewe CUF mara kibao, kama ni kweli siku zote huwa wanashinda lakini hawatangazwi, kitu kipi kimewafanya waamini this time wakishinda watatangazwa?!, hakuna mwenye jibu!.

Kiukweli siku zote uchaguzi wa Zanzibar ni twists and tuns, sometimes margin ya mshindi na mshindwa ni just 2% hivyo whoever knows the best game akifanikiwa ku twist, yeye ndio mshindi, ndio maana nimewauliza CUF, kama walishinda kihalali kwa kua nyingi, nini kinachowafanya waogope kurudiwa kwa uchaguzi, si ni watashinda tena?!, hawana jibu!.

Pasco
 
Mkuu GHIBUU, tangu lini rais wa Zanzibar ni rais nje ya Zanzibar?!. Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania bara na Tanzania visiwani, au Tanzania Zanzibar. Ndani ya Muungano, sehemu ya Zanzibar inajitegemea kwa utawala wake wa ndani, lakini nje ya Muungano, hakuna nchi ya Zanzibar, bali kuna sehemu ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT!.

Uchaguzi wa Zanzibar ni mambo ya ndani, uchaguzi wa JMT uliisha kamilika, hivyo JMT haihusiki na uchaguzi wa ndani wa Zanzibar, ila Ulinzi na Usalama sio suala la ndani ya Zanzibar, hili ni suala la JMT, sasa kama uchaguzi wa Zanzibar utaleta tishio lolote la ulinzi na usalama, JMT ipo kuhakikisha hili halitokei!.

Sio tuu rais wa Zanzibar, bali wale wakuu wote 4 wa Zanzibar wanaotembea na vingora, wakija baa au wakisafiri kwenda nje ya nchi, balozi za JMT huwa wanawapatia heshima stahiki.

Pasco
 
Mm huwa nawatahadharisha sana watanganyika,moto wanao uchochea ukija kuwaka wasidhani watanganyika watabaki salama zanzibar.
 
Naona unajikanyaga tu,adui wa wazanzibar kwenye harakati hizi za kujikomboa kwenye makucha haya ya mkoloni anajulikana,wazanzibar wapo tayari kupambana nao liwalo na liwe.
 
Haya yote yanasababishwa na koloni la kupangwa,Tanganyika kujifunika blanket la Tanzania tena mchana wa jua kali tena bila kuona hata joto,matatizo ya Znz yatamalizwa na wa znz wenyewe.
Rais JMT kutoingilia hadi sasa kufutwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar ni kielezo cha kuheshimu Katiba na utawala wa sheria.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Pasco,inamaana CUF wakiamua kushiriki na wakashinda tena je Uchaguzi utarudiwa???Maana CCM haijawahi kushinda huko ni kulazimisha kushinda.CCM ikishindwa tena kwa kishindo Uchaguzi utarudiwa tena???
Tetty: toa ushahidi kwa takwimu. La, acha hisia zako, porojo za siasa maji taka na maneno ya uchochezi.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
What's wrong with you Pasco?

Sheria imeweka limitation ya kwenda kupinga matokeo, sawa, lakini yepi sasa maana yalifutwa kinyume cha sheria na katiba hiyo hiyo?

Mimi kwa mtazamo wangu;

1. Kwanza sikubaliani na mtazamo wako wa jumla ktk bandiko lako kuu kwamba CUF hawana option nyingine isipokuwa kushiriki uchaguzi batili wa marudio au la wajiandae kufutika ktk uso wa ramani za siasa!

2. Option zipo nyingi sana in favour of CUF na kuwatupitilia mbali huko CCM na ulaghai wao. Hata wewe naamini umeandika haya huku ukiutambua
ukweli huu;

Kwanza, unakumbuka Dr Shein mara kwa mara alikuwa akirudia rudia kusema kuwa kama kuna watu wanaamini kuwa muda wake wa kushika madaraka ya urais kikatiba ulishakwisha waende mahakamani?

Kwa nini unadhani alikuwa anaweka mtego huo? Jibu la swali hili ni rahisi sana, kwamba waende mahakamani na kwa sababu ana influence na mahakama, then mahakama hiyo ingetoa hukumu in favour of him. Na kwa hukumu hiyo, CUF au wote wanaomlamimikia Dr Shein wanakuwa wamepigwa goli la kisigino na hata uamuzi wa Jecha wa kufuta matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa trh 25/10/2015 kinyume cha utaratibu, sheria na katiba unakuwa "kama umehalalishwa". Yes, kwani kuna linaloshindikana kwa watawala wa CCM?.....Good enough kuwa CUF na wanademokrasia waliliona hili!

Pili, kwa tunakoelekea na baada ya kutangazwa kwa marudio ya uchaguzi mwezi machi, Jecha (sio ZEC) na CCM wanajiweka kwenye kitanzi wao zaidi kuliko kule wanakofikiri ku accomplish malengo yao. Maana yangu ni kwamba, baada ya hili mazingira yanai feva CUF zaidi kuliko CCM na serikali batili ya Dr Shein. Huko mbeleni hata njia ya kwenda mahakamani ni nyeupe na rahisi zaidi kupinga kilekile walichotaka CCM maalim Seif na wanaomuunga mkono waende mapema!

Lazima tuelewe kuwa, kuna mazingira flani hata mahakama zetu hizihizi ambazo watendaji wake ni wateule wa rais aliye madarakani huwa ni vigumu saaaana kupindisha haki au ukweli.

Trust me bro, hili la kutangazwa kwa marudio ya uchaguzi ndilo limefungua mlango kwa CUF kwenda mahakamani sooner or later. Na hii ndiyo option iliyo salama zaidi na wazi kwa sasa pengine itakayotatua mgogoro huu kwa usalama.

3. There is clear indication kuwa hiki kinachoitwa uchaguzi wa marudio hakitakuwepo, amini usiamini. CCM wanajua exactly wanachokifanya kuwa hakipo kiutaratibu, kisheria wala kikatiba . Na pengine wanajua kabisa tukifanya hivi, wapinzani wetu watakuja na move hii. Lakini amini usiamini kuna mmoja atakosea tu na atapigwa bao na mpaka hapa tulipo CCM wameshakosea, the game is in favour of CUF na wananchi walio wengi wa Zanzibar waliofanya maamuzi yao trh 25/10/2015!

4. All in all, CUF wametangaza kuwa watakuwa na vikao vyao vya maamuzi next week inayoanza kesho. Let's wait and see watakuja na maamuzi gani. Binafsi nililo na uhakika nalo ni kuwa HAKUNA UCHAGUZI MWINGINE na kama utakuwepo behind the scene CUF HATASHIRIKI na iwapo hawashiriki na CCM wakaulazimisha huo uchaguzi na wao kujitangaza washindi (maana that's motive behind), Zanzibar will end up in an endless chaos. Sasa sina hakika kama kuna mmoja wapo kati ya hawa mafahari yaani CUF na CCM wanataka kuifikisha Zanzibar huko kwa jambo dogo kama hili!!


 
Hapa nakubaliana na ww Pasco, iwapo CUF hawatoshiriki hawatakuwa na muwakilishi hivyo watakosa ruzuku. Na kwa kuwa hawatakuwa na muwakilishi wa kisheria hivyo watakuwa nje ya vyombo vya maamuzi. Hali hii itawaacha ccm na uwezo wa kimaamuzi na kwa jinsi hali itakavyokuwa maamuzi mengi yatafanywa kibabe dhidi ya wanacuf kama sehemu ya kuwakomoa na kuwadhalilisha. Sote tunaona dola inavyotumika vibaya panapokuwa na mihemuko baina ya pande mbili zinazohasimiana kisiasa.

Hofu yangu ambayo ni dhahiri itajengeka ndani ya ZNZ iwapo CUF itasusia na ccm kushinda ni vitendo vya kigaidi. Iwapo hali hii itatokea sio ZNZ wala Tanganyika tutakuwa salama. Ni nani asiyejua hatari ya mashambulizi ya kigaidi, Dunia nzima leo hii ni wahanga wa ugaidi leo sisi tunajiwekea mazingira hayo kwa kuacha kufuata demokrsia kwa sababu za kipuuzi kabisa. Leo tunakalia kimya uhuni uliofanywa na Jecha na walio nyuma yake, lakini hicho tunachokipanda soon tutavunan.
 
Hoja ya Pasco ni nzito, asibezwe. Uhai wa chama cha siasa unapimwa kwa wingi wa wanachama na iwakilishi kwenye vyombo vya mamuzi kama udiwani na ubunge. Endapo cuf watasusa, watakosa madiwani na wawakilishi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni sawa na kujifuta kisiasa. Je, uamuzi huo utakuwa na tija kwa cuf . Hapana.

Natumaini viongozi wa cuf wataweka pembeni hasira na kutumia busara na hatimaye kuamua kushiriki uchaguzi. Treni ya jecha inataka kuanza safari. Atakayeshindwa kupanda ataachwa. Asilalamike. Serikali ya muungano haitaruhusu wataotaka kufanya vurugu. Na ukweli ni kwamba bila cuf siasa za zenj zitapooza sana. Hatutaki pia hilo litokee.
 
Pasco.

Zanzibar ni zaidi ya siasa kusema CUF itakufa Zanzibar kwa sababu ya kususia uchaguzi ni kujidanganya.

Mgogoro wa Zanzibar ni zaidi ya siasa wana matatizo yao makubwa ya kihistoria baina ya Unguja na Pemba.

CUF Zanzibar siyo kama Tadea au UDP refer kura za maruhani, CUF wanaweza kususia uchaguzi na CCM wakashinda kila kitu lakini huko kutakuwa ni kujiliwaza na kuhairisha tatizo ni suala la muda tu matatizo yatakuwa pale pale.

Jambo la msingi Zanzibar ni kuwaacha Wazanzibar wenyewe wahamue wanachotaka zaidi ya hapo mgogoro wa Zanzibar hauwezi kuisha huo ndiyo ukweli.

Ubaya na uzuri Zanzibar CUF ipo kwenye mioyo ya watu siyo kwenye makaratasi nawajua vizuri Wazanzibar kusema CUF itakufa huko ni kujidanganya mkuu wangu.
 

Poor Pasco!
Una uwezo mdogo sana wa kutafakari mambo kwa kina tofauti na nilivyokudhania hapo kabla!
Waliosema elimu sio vyeti ulivyonavyo walikuwa sahihi, na watabaki kuwa sahihi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…