MaalimSeif hawezi kwenda Chadema labda aahidiwe uenyekiti. Njia pekee ni yeye kukaa chini na Lipumba wakinusuru chama chao.Wabunge hao watahamia chadema na watachaguliwa tena kupitia chadema
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MaalimSeif hawezi kwenda Chadema labda aahidiwe uenyekiti. Njia pekee ni yeye kukaa chini na Lipumba wakinusuru chama chao.Wabunge hao watahamia chadema na watachaguliwa tena kupitia chadema
UZEMBE WAKE WAKE WA KUCHELEWA KUMCHUKULIA HATUA LIPUMBA SASA AKUBALI KUJIUNGA NA CHADEMA TUUnapaswa kwanza ujue lengo la walio nyuma ya Lipumba.
Walio nyuma ya Lipumba wanataka Kumfuta Maalim uanachama ili;
☞ kumkosesha platform ya kuongelea mambo ya CUF
☞Kudhoofisha madai yake ya urais wa Zanzibar ambayo yamefikia mahali pazuri kwenye jumuiya za Kimataifa.
Ili kujua Maalim afanye nini lazima kujiuliza kwanza ;
Je, walioko nyuma ya Lipumba wakifanikiwa kumfutia Maalim uanachama (Kitu ambacho watafanikiwa ) , Madai ya urais wa Zanzibar ya Maalim kwenye jumuiya za Kimataifa yataathirika kiasi gani?
Kama hayataathirika basi Maalim apractice kile wazungu wanasema -Stop, look, listen, think and wait .
Kama yataathirika basi Maalim anaweza kuchukua ushauri wako hapo juu.
mbona hata alipoamua kakaa pembeni aliitwa msaliti acha afanye yakeSiasa sipendi ila Lipumba anavyowafanyia Wapinzani sio sawa alijiondoa ili kudhoofisha upinzani na ameamua kuja kuua kabisa upinzani haswa chama kilichomkaribisha... kama hawataki tena akae tu pembeni kuugua ukimwi sio lazima uambukize na wengine ili mfe wote
Sio kweli, baada ya kujiunga na Ukawa ndo wakapata walau viti vingi bara. Hivyo usipotoshe ukweli.Mbona kuumaliza huu mgogoro nirahis sana,,maalim kumpigia sim lipumba wakutane wenyewe wawili2 wayamalize halafu waite vyombo vyahabar wawaeleze wafuas wao kua hakuna tofaut.ili kama lipumba ametumwa kumuua seif lazima atakataa maana kazi yake itatibuliwa maalim atakaporud ila kama lipumba atakubali nakumaliza tofaut na seif itakula kwa chadema maana wao ndo wanaoivunja cuf.kwamfano mpaka sasa ugomvi mkubwa wa lipumba niule muungano wa ukawa umeimeza cuf na nccr vibaya sana hata kuhatarisha cuf kutoonekana
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nn asianzishe chama kipya ila akiite "CUF Asilia"walau neno CUF liendelee kumtambulisha maana si rahisi kumtenganisha nalo kihistoria...Mbinu waliyotumia ccm ni pigo kwao. UPINZANI sio CUF kama chama Bali ni watu. Na watu hao wanaweza kuamua kuwa chama chochote, na wakiamua kuwa Chadema ccm ndio watajuta!
Mkuu nakupatia salute aisee. Umeona mbali sana kuliko nilivyokuwa nadhania. Hongera sanaCUF HAITAKUWA IMARA TENA! MISSION IMEKAMILIKA KWA 80+℅
CUF sasa inaishilia, ni kama mpango unakamilika, mpango mkakati umetengenezwa kimkakati zaidi, kuhakikisha CUF haina nguvu tena, ili kuleta unafuu visiwani. Wabunge wa majimbo wakishavuliwa uanachama, majimbo yao yatakuwa wazi, uchaguzi utarudiwa, kama hujui ni mpango,: kumbuka kauli ya juzi ya mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, pale aliposema' ikiwa wabunge wa CUF watavuliwa uanachama, tume imejiandaa kwa dharula yoyote na bajeti ipo! Akili kumkichwa' mkurugenzi wa tume anazungumzia uchaguzi mdogo kwenye majimbo ambayo bado yana wabunge! MISSION
Lipumba sasa anatambuliwa na kila taasisi ya sirikali, anatambuliwa na Bunge, anatambuliwa na Msajili, anatambuliwa mpaka na taasisi ya jikoni! MISSION
Kete kwa upande wa CUF Halisi ilikuwa imebaki moja tu (MAHAKAMA) baada ya makosa kufanyika nyuma! Ndiyo makosa yalifanyika mwanzo kabisa kwa upande wa Maalim Seif kumdharau Lipumba na kumuona ni mtu mmoja tu anayetapatapa kisha atatulia, hawakumuona mapema aliyekuwa nyuma ya Lipumba! Hili lilikuwa Kosa kubwa! Wamekuja kushituka na kuiona nguvu yake kipindi ameingilia bodi ya wadhamini ya CUF! Hapo ndo walishituka na kumbe tayari walikuwa wamechelewa! Walipaswa kumshughulikia mapema!
Sasa kete ya mahakamani nayo inaanza kufeli, kwa nini nasema inafeli?
1😛amoja na kesi ya kutomtambua Lipumba na kauli ya Msajili kuwa mahakamani! Bado Lipumba ameendelea na shughuli za chama kwa kujitanua hadi kufukuza wabunge bila woga na hakuna mhimili unaohoji!
2: Kutupiliwa mbali kwa mapingamizi ya wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama, ni pigo kubwa kwa upande wa Maalim Seif! Hata wakirekebisha vifungu walivyotakiwa kuvirekebisha, wao wako mahakamani, Lipumba anaendelea na shuguli za chama huku akijipanga kuwaita na kuwahoji wabunge wa majimbo!
3: Kutotambulika kwa maazimio ya CUF upande wa Maalim wa kuwavua ubunge wabunge wawili ni pigo kubwa pia.
NANI ALAUMIWE
1. Mtatiro;
Ndiyo, huyu ni mtu wa kwanza kabisa kulaumiwa na wana CUF' atanisamehe. Yeye alipewa jukumu kuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Lakini amekuwa akifanya siasa za mtandaoni zaidi, kila Lipumba akifanya jambo, yeye huja kulalamika mtandaoni na hukomea kuandika tu bila ya kuelezea njia mbadala ( rejea post zake kwenye plofile yake) Sasa kama yeye kiongozi analalamika na kujibu mapigo ya Lipumba mtandaoni, wengine watafanyeje? Yeye huiongelea CUF baada tu ya Lipumba kufanya kisanga, Lipumba akiwa kimya' na yeye yuko kimya. Kwa hiyo amekuwa akicheza ngoma ya Lipumba!
2. Maalim Seif
Yeye namlaumu kwa kutochukua hatua mapema, Lipumba hakupaswa kupewa nafasi mapema, naye sasa amekuwa akijibu mapigo ya Lipumba tu badala ya Lipumba kujibu mapigo yake! Lipumba akiita Baraza lake, naye anaita lake, Lipumba akifukuza wabunge, naye anafukuza! Amechelewa sana!
NINI CUF YA MAALIM IFANYE?
Kwa sasa CUF ya Maalim imebanwa sana na Lipumba, na naona imebakiwa na option mbili tu!
1. Mahakama;
Mahakama pekee kwa sasa ndo imebaki kuweza kuamua kama CUF iwe ya Lipumba au ya Maalim. Na ikitokea mahakama ikaamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, Maalim atabaki na option mbili tu, mosi kuungana na Lipumba au
2. Kuongeza nguvu CHADEMA.
Option ya mwisho kabisa kwa Seif ni kutangaza kuachana na siasa za CUF ya Lipumba na kuongeza nguvu upande wa CHADEMA. Faida kubwa kwa upande wa CHADEMA ikiwa hili litatokea, ni kupata wafuasi wengi Zanzibar bila chenga! Na hapo ndipo msemo usemao "Waliokuwa nyuma ya Lipumba waliruka mkojo wakakanyaga kinyesi" utatimia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki ndicho kinachotakiwa Maalim ndio katumika bila kujijua au kwa makusudi Lipumba kamuita Mara ngapi yeye akawa anashikiwa Akili na watu wenye Akili ndogo.Asilalamike CUF wameshaizika rasmi.Chadema juuuuuuu juuuuuuu zaidi.Wabunge hao watahamia chadema na watachaguliwa tena kupitia chadema
TrueKumuunganisha Maalim Chadema litakuwa kosa kubwa kuliko yote la kimkakati alilofanya Sizonje.
WE WILL BE A LEGION AND NOTHING CAN STOP US!
You never want your enemy to be united against you , Sizonje makes us more than united, he makes us strong.
Mku ni kweli kabisa.new era is coming,2020 ndio mwisho wa cuf kama jina, upinzani ni watu sio chama,upinzani hauwezi kufa, kinachoendelea saivi ni hasara kubwa kwa watawala,wanatumia mbinu zao nyingi sana kwa wakati mmoja ili kupambana na upinzani,
wanachofanya bila ya kujijua ni kujenga nguvu kubwa sana ya upinzani na sio kuua,binadam tulivyo tunajifunza kutokana na makosa,kila ujanja wanaotumia kukandamiza watu,unatafutiwa ufumbuzi, mbinu zao zikishamalizika nao wao watamaliza pia