Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Watu wanapenda kulaumu matokeo hawataki kuangalia chanzo cha tatizo. Tujiulize Lipumba kuachia uenyekiti wa CUF chanzo nini? Je kulikuwa na maridhiano vizuri ni nani ashike hatamu kuiwakilisha CUF kugombea uchaguzi mkuu wa 2015 au watu waliburuzwa ktk kufikia maamuzi hayo? Na kauli gani zilitolewa na walioshinda kumpitimpitisha mgombea wanae mtaka dhidi ya wale walioshindwa ktk majadiliano? Au ilikuwa ile umeshinda vita lakini mapambano bado?
Chanzo nialipewa hela ..sasa utamongopea nani hapa .hizo habari unazosema kawambie kwenye vijiwe vyakahawa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N wasiwasi na ubobezi wa uchumi wa huyu jamaa maana kamwe sijaona faida yake hata kushauri ishu za uchumi
 
We umeiona CUF wakati wa uchaguzi juzi tu? Unajua bara CUF imejengwa na nani? Unakumbuka container la visu wewe? Unakumbuka Ngangari na Ngunguli ya inspector Omari Mahita?
Kwa hiyo unaamini Lipumba akigombea urais kupitia UKAWA atashinda!
 
Kwa hiyo unaamini Lipumba akigombea urais kupitia UKAWA atashinda!

Ukawa ni genge la wahuni, hivyo lipumba ana akili timamu ndio maana haitaki maana ukawa aliyoiasisi si hiyo inayomilikiwa na fisadi lowasa
 
Chanzo nialipewa hela ..sasa utamongopea nani hapa .hizo habari unazosema kawambie kwenye vijiwe vyakahawa .

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi kabisa. Lakini kwa mujibu wa mtazamo wako. Jiulize ilikuwaje hadi akafikia hatua ya kununulika? Nini kilimpa msukumo huo? Kwanini chaguzi za miaka ya nyuma hakununulika kiasi cha kukubali kuachia kiti chake cha uongozi wa chama cha CUF? Think big! Usilewe kirahisi propaganda za kisiasa, mimi nakubali anaweza kuwa kanunuliwa lakini chanzo ni nini hasa kufikia maamuzi hayo ya kupokea pesa(KAMA KWELI KAPEWA PESA/HELA)?
 
Kama ni kweli, Lipumba anaiua CUF kwa mikono yake na njaa zake.

Damu na Jasho la waliopigania CUF wakati wa uchaguzi wakati yeye akiwa mapumzikoni vitamuandama maisha yake yote.

Dhambi mbaya sana hii..
Kwani ana hasara gani anapoteza nini.MWACHENI ACHAPE KAZI
 
Upo sahihi kabisa. Lakini kwa mujibu wa mtazamo wako. Jiulize ilikuwaje hadi akafikia hatua ya kununulika? Nini kilimpa msukumo huo? Kwanini chaguzi za miaka ya nyuma hakununulika kiasi cha kukubali kuachia kiti chake cha uongozi wa chama cha CUF? Think big! Usilewe kirahisi propaganda za kisiasa, mimi nakubali anaweza kuwa kanunuliwa lakini chanzo ni nini hasa kufikia maamuzi hayo ya kupokea pesa(KAMA KWELI KAPEWA PESA/HELA)?
Unaniuliza swali gani lakitoto??nini kilimshawishi kununilika ???hivi mfano mko wanaume wa5 akaja mtu akasena ana billion 1 anataka kati yenu akamtatue malinda akatokea moja akaenda utauliza kwanini kaenda au ndo tabia yake hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi mfano mko wanaume wa5 akaja mtu akasena ana billion 1 anataka kati yenu akamtatue malinda akatokea moja akaenda utauliza kwanini kaenda au ndo tabia yake hiyo.
Kwa uandishi wa namna hii naomba nikuombe radhi, siwezi kuendelea na mjadala na wewe. It is too low! Hapo busara imekaa mbali sana. Sijui umri au unatumia substance flani yenye kuleta shida ya afya.
 
Ukimlaumu Mtatiro utakuwa unamwonea tu. Kambi ya Maalim Seif ilifanya kosa kuchelewa kuziba nafasi ya Lipumba alipojiuzulu mwaka 2015. Kitendo cha kukaa mwaka mzima bila kuziba ile nafasi lilikuwa kosa kubwa linalotumiwa kuwavuruga.
Mtatiro alipewa uongozi mwaka 2016 na bado anategemea sana maelekezo ya Maalim Seif

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili mimi kidogo nalikataa kwa sbb:

1. Labda kabla ya kuhitimisha hivi, tujiulize katiba yao inasemaje kuhusu kuziba nafasi ya kiongozi (hasa ya m/kiti) aliyejiuzuru ama kuachichwa ama kufukuzwa kwa sbb ziwazo zozote zile...

2. Nakumbuka nafasi ya Ibrahim Lipumba, immeaditely baada ya kujiuzuru ilichukuliwa na Twaha Tasilima ktk kile kipindi cha mpito na baadaye nafikiri ndipo Mtatiro akawa m/kiti wa kamati ya uongozi...

Hii inaleta kujiuliza maswali haya:

Je, haya yote yalikuwa yanafanyika kinyume na taratibu zao ?

Na, je Msajili wa Vyama vya Siasa wakati huo alikuwa anatambua/alitaarifiwa kuwa Lipumba kama m/kiti wa CUF taifa alishajifuta kwa kujiuzuru mwenyewe ?

Msajili wa vyama vya siasa kwa kipindi chote ambacho Lipumba alishajiondoa CUF alikuwa anafanya kazi na nani kama m/kiti wa CUF taifa ?

Mimi sina imani na Sina hakika kabisa kuwa huko CUF kuna viongozi ambao hata hawajui taratibu za katiba yao wenyewe zinasemaje !!
 
Kama ni kweli, Lipumba anaiua CUF kwa mikono yake na njaa zake.

Damu na Jasho la waliopigania CUF wakati wa uchaguzi wakati yeye akiwa mapumzikoni vitamuandama maisha yake yote.

Dhambi mbaya sana hii..
kabisa!!!!
 
Kifupi lipumba anatumika tena kwa nguvu zote ukitaka niamini hilo hebu lejerea chaguzi zote kuanzia kwa mkapa mpaka sasa kadri chaguzi zinavyofanyika com wanashuka sana tujiulize magufuri amepita kwa aslimia ngapi, kama zimeshuka sana je unatarajia nn kwa uchaguzi ujao?na kwakuwa ccm akili zao ni zero wanazani wanauwa upinzani lkn ki ukweli upinzani unapata nguvu kubwa sana na majibu tuombe MUNGU tukiwa hai majibu mtayaona lkn kingine wapinzani you sasa ndo muda wao,lipumba kaanza kutumika muda mrefu sana sema trip hii nfo kabisa na serikali kujidhihisha wazi lkn kwakuwa ccm wana mtindio wa ubongo hawalijui hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
basi wewe utakuwa lipumba..manake akili zako zinafanana na zake
Si umeona akili za lipumba zilivyomgaragaza boss wako seif! Na bado, hiyo ni treila tu bado muziki. Hadi atakimbia Pemba.
 
Kumbe ndio maana Mbowe anakomaa kulinda chadema mana anajua kuwa baadhi ya wanaojiita wapinzani ni wasaliti na vibaraka wa CCM.

Ila kwa ushauri wangu ningeishauri serikali ya CCM wasipoteze Rasilimali watu za muhimu kwa kuzipa kazi za hovyo badala ya kuwatumia kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi.

Kama kweli tunataka maendeleo na sio vyama na siasa basi Lipumba ateuliwe kuwa Mbunge na kisha apewe uwaziri. Tunamtumia msomi kuleta fujo na machafuko badala ya kumtumia kuleta maendeleo. Ni jambo ya fedheha sana. Elimu ya Lipumba inaangamia bure.

Mtu mwingine wa kumpa nafasi ni Dr. Slaa.
Hawa watu ni wazi kuwa wanafaa sasa kuitumikia serikali ya CCM kwa mambo ya msingi yenye keleta maendeleo. Inatosha kuendelea kumtumia Lipumba kisiasa badala ya kuleta maendeleo.

Mh. Rais tuletee Dr. Slaa na Prof. Lipumba kwenye baraza lako la Mawaziri.
Bila kumsahau Mzalendo wa kweli Kafulila.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mara ya kwanza nawaona wapemba kumbe si lolote! Nilikuwa nawaaminiaa sana sana! Lakini sasa kama siwaelewi hivi!!!!! CuF inaenda kufa hasa bara......!! Itabakia Zbar sababu hawakupigiw kura bara.....sasa Maalim atabakia hana la kufanya!
 
Back
Top Bottom