Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

CUF HAITAKUWA IMARA TENA! MISSION IMEKAMILIKA KWA 80+℅

CUF sasa inaishilia, ni kama mpango unakamilika, mpango mkakati umetengenezwa kimkakati zaidi, kuhakikisha CUF haina nguvu tena, ili kuleta unafuu visiwani. Wabunge wa majimbo wakishavuliwa uanachama, majimbo yao yatakuwa wazi, uchaguzi utarudiwa, kama hujui ni mpango,: kumbuka kauli ya juzi ya mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, pale aliposema' ikiwa wabunge wa CUF watavuliwa uanachama, tume imejiandaa kwa dharula yoyote na bajeti ipo! Akili kumkichwa' mkurugenzi wa tume anazungumzia uchaguzi mdogo kwenye majimbo ambayo bado yana wabunge! MISSION

Lipumba sasa anatambuliwa na kila taasisi ya sirikali, anatambuliwa na Bunge, anatambuliwa na Msajili, anatambuliwa mpaka na taasisi ya jikoni! MISSION

Kete kwa upande wa CUF Halisi ilikuwa imebaki moja tu (MAHAKAMA) baada ya makosa kufanyika nyuma! Ndiyo makosa yalifanyika mwanzo kabisa kwa upande wa Maalim Seif kumdharau Lipumba na kumuona ni mtu mmoja tu anayetapatapa kisha atatulia, hawakumuona mapema aliyekuwa nyuma ya Lipumba! Hili lilikuwa Kosa kubwa! Wamekuja kushituka na kuiona nguvu yake kipindi ameingilia bodi ya wadhamini ya CUF! Hapo ndo walishituka na kumbe tayari walikuwa wamechelewa! Walipaswa kumshughulikia mapema!
Sasa kete ya mahakamani nayo inaanza kufeli, kwa nini nasema inafeli?

1😛amoja na kesi ya kutomtambua Lipumba na kauli ya Msajili kuwa mahakamani! Bado Lipumba ameendelea na shughuli za chama kwa kujitanua hadi kufukuza wabunge bila woga na hakuna mhimili unaohoji!

2: Kutupiliwa mbali kwa mapingamizi ya wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama, ni pigo kubwa kwa upande wa Maalim Seif! Hata wakirekebisha vifungu walivyotakiwa kuvirekebisha, wao wako mahakamani, Lipumba anaendelea na shuguli za chama huku akijipanga kuwaita na kuwahoji wabunge wa majimbo!

3: Kutotambulika kwa maazimio ya CUF upande wa Maalim wa kuwavua ubunge wabunge wawili ni pigo kubwa pia.

NANI ALAUMIWE

1. Mtatiro;
Ndiyo, huyu ni mtu wa kwanza kabisa kulaumiwa na wana CUF' atanisamehe. Yeye alipewa jukumu kuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Lakini amekuwa akifanya siasa za mtandaoni zaidi, kila Lipumba akifanya jambo, yeye huja kulalamika mtandaoni na hukomea kuandika tu bila ya kuelezea njia mbadala ( rejea post zake kwenye plofile yake) Sasa kama yeye kiongozi analalamika na kujibu mapigo ya Lipumba mtandaoni, wengine watafanyeje? Yeye huiongelea CUF baada tu ya Lipumba kufanya kisanga, Lipumba akiwa kimya' na yeye yuko kimya. Kwa hiyo amekuwa akicheza ngoma ya Lipumba!

2. Maalim Seif
Yeye namlaumu kwa kutochukua hatua mapema, Lipumba hakupaswa kupewa nafasi mapema, naye sasa amekuwa akijibu mapigo ya Lipumba tu badala ya Lipumba kujibu mapigo yake! Lipumba akiita Baraza lake, naye anaita lake, Lipumba akifukuza wabunge, naye anafukuza! Amechelewa sana!

NINI CUF YA MAALIM IFANYE?
Kwa sasa CUF ya Maalim imebanwa sana na Lipumba, na naona imebakiwa na option mbili tu!

1. Mahakama;
Mahakama pekee kwa sasa ndo imebaki kuweza kuamua kama CUF iwe ya Lipumba au ya Maalim. Na ikitokea mahakama ikaamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, Maalim atabaki na option mbili tu, mosi kuungana na Lipumba au

2. Kuongeza nguvu CHADEMA.
Option ya mwisho kabisa kwa Seif ni kutangaza kuachana na siasa za CUF ya Lipumba na kuongeza nguvu upande wa CHADEMA. Faida kubwa kwa upande wa CHADEMA ikiwa hili litatokea, ni kupata wafuasi wengi Zanzibar bila chenga! Na hapo ndipo msemo usemao "Waliokuwa nyuma ya Lipumba waliruka mkojo wakakanyaga kinyesi" utatimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
You said it all! Kwanza wajaribu hii ya mahakama, ikishindwa, CUF Seif wahamie CHADEMA! Lakini hii ya CHADEMA sio nzuri sana kwa upande wa bara! The best option ni kununua Chama cha kisiasa chenye usajili wa kudumu kama vile NLD nk! Hii itakuwa na mashiko zaidi kwa upande wa bara na visiwani na zaidi ya hapo ni vizuri hata kwa usitawi wa UKAWA!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
 
Hongera kwa uchambuzi, ni kweli maalim seif anatakiwa ang'oe timu fasta bila kuwaza ya uchaguzi uliopita, kama kuzulumika atalipwa na mungu wake, namshauri aungane na chadema aiache hiyo cuf ya genge, namwambia hivii.. Achana na mambo ya nyuma, angalia yajao!
 
Hao wabunge hawana jinsi, wamuunge tu mkono Lipumba .Maana kurudi bungeni itakuwa ngumu. As far Lipumba ndo mwenye rungu kwa sasa.
 
Mbinu waliyotumia ccm ni pigo kwao. UPINZANI sio CUF kama chama Bali ni watu. Na watu hao wanaweza kuamua kuwa chama chochote, na wakiamua kuwa Chadema ccm ndio watajuta!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mbinu waliyotumia ccm ni pigo kwao. UPINZANI sio CUF kama chama Bali ni watu. Na watu hao wanaweza kuamua kuwa chama chochote, na wakiamua kuwa Chadema ccm ndio watajuta!


Hivi CCM walimtumia nani kuwazuga kina Maalim Seif wasizibe nafasi ya Lipumba kwa wakati?
 
new era is coming,2020 ndio mwisho wa cuf kama jina, upinzani ni watu sio chama,upinzani hauwezi kufa, kinachoendelea saivi ni hasara kubwa kwa watawala,wanatumia mbinu zao nyingi sana kwa wakati mmoja ili kupambana na upinzani,

wanachofanya bila ya kujijua ni kujenga nguvu kubwa sana ya upinzani na sio kuua,binadam tulivyo tunajifunza kutokana na makosa,kila ujanja wanaotumia kukandamiza watu,unatafutiwa ufumbuzi, mbinu zao zikishamalizika nao wao watamaliza pia
Upinzani unaimarika na wapinzani watashikana kiimani zaidi yaani kiupinzani zaidi than b4,
Watawala wanaona CUF na Maalim ndiyo tatizo ila kwa sababu wamefungwa kimaono kwa ajili ya dhuluma zao hapo ndipo watakapokuja kujifunika asubuhi.
Tusubiri na naomba iende hivihivi.
 
Msiombe CUF ya Maalim iende Chadema.
Move hii ilitarajiwa sana na Chadema.
Ccm anataka cuf ijifie. Uchaguzi ukirudiwa zenji (Pemba) Ccm itapata baadhi ya majimbo. Kumbukeni kutakuwa na cuf vurugu ya lipumba,ADC ,na Ccm.
Wapemba hawajazoea vurugu wengi watakaa bila kupiga kura.
Waunguja wataenda kupiga kura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani ni tunu, amani haichezewi bali amani huenziwa. Chuki ya kisiasa ni mbaya sana kwani ni rahisi kupandwa lakini ikishaota mizizi ni ngumu kuiondoa. Doze doze dola yetu tukufu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kudhoofisha madai yake ya urais wa Zanzibar ambayo yamefikia mahali pazuri kwenye jumuiya za Kimataifa.
kwa hili unadanganya umma....pazuri wapi hapo? Tusidanganyane wandugu katika hili la zanzibar mambo yameshakwisha hakuna atakayekuja kubadili matokeo ya zanzibar only wazanzibar wenyewe ndo wanauwezo huo
 
Kosa lingine la Mtatiro ni kukimbilia USA kusoma wakati nyumba yake inaungua. Mtatiro anasoma ili iweje wakati ana elimu nzuri (Masters) na madaraka makubwa kuliko umri wake? Anataka nini zaidi?
 
Wanaotaka kuiua CUF wafikirie Mara tatu kwa maana mbeleni naona mfalme CHADEMA anaandaliwa .
Kama CUF ya Maalim Seif iliungana na CHADEMA ya LOWASSA wakapata wabunge 10 Tanzania Bara ,akihama moja kwa moja kwanza CUF itakufa na pili CHADEMA itachukua hatamu Bara na Visiwani .
Wasiwasi wangu ni kwamba CCM itapata wakati mgumu Mara dufu kuisambaratisha CHADEMA Visiwani kama inavyofanya kwa CUF ikiwa tu Maalim Seif na kundi lake wataamua kuhama chama

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ya selikali siyo chama, bali seif na madai yake ya urais!

Ndio maana wanamuweka busy kushughulikia issue za cuf, na mwisho wa siku atajikuta 2020 imeshafika.

......
 
Wabunge hao watahamia chadema na watachaguliwa tena kupitia chadema
Kuchaguliwa tena? sijui kama itakuwa rahisi kwani CCM sio Ile ya 2015 sasa hivi watashinda hata kwa nguvu yaani ni ubabe usipime. Maalim Ana option moja ampigie magoti lipumba akubali amezidiwa kete yaishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumuunganisha Maalim Chadema litakuwa kosa kubwa kuliko yote la kimkakati alilofanya Sizonje.
WE WILL BE A LEGION AND NOTHING CAN STOP US!

You never want your enemy to be united against you , Sizonje makes us more than united, he makes us strong.
umesahau kuwa sio wote waliopo CUF watakua willing to join CHADEMA,so its 50 -50 hakuna uhakika kuongezea hapo kumbuka 2015 mlikua vyama vinne still mkashindwa tena uchaguzi wa moto zaidi kuwahi kutokea,leo hii NCCR imekufa kifo baridi,NLD haina kitu CUF ndo hivoo, ACT inazidi kujipambambanua kwa kasi zaidi kihoja na si kwa vihoja mnafikiri mnaguarantee hiyoo unayojinasibu mnayo endapo Seif akija CHADEMA??
 
Back
Top Bottom