Mwiba,
Kaazi kweli kweli!
Yaani posts zako hakuna Thanks hata moja!!! kwa nini?
Fanya reality check...kuna taabu mahali nadhani!
Maneno mengi!!! Substance kidogo!!!
Samahani ndugu na rafiki yangu!
Naenda kivyangu vyangu,mpaka nitaeleweka,si unajua kuna tatizo la wachangiaji ,wengi wetu mnaendeleza hisa za CCM ,hivyo sitegemei kupewa asante kwa kumsema Kikwete au Slaa au Zitto maana hawa wote ni kundi moja.Sio Chama kimoja nimesema kundi moja.
Kikwete anaibeba CCM kuwepo madarakani halikadhalika Slaa na Zitto ndio hivyo hivyo wanasaidia kwa kiasi kikubwa kuipa tamaa CCM.
Mimi ni tofauti na misimamo ya Slaa na wenzake ,Jamii ya akina Slaa imezama katika tuhuma kuituhumu CCM ,kuwa ni wala rushwa au mafisadi wakisaidiwa na nyaraka mbalimbali zinazowapa kuwa kifua mbele katika kunadi shutuma hizo ambazo kwa wanavyoona ni za kweli na ziwe za kweli kama zinavyoonyesha katika data zao.
Vipi CCM wananufaika na matangazo ya akina Slaa na kundi lake ,hapa ndipo msaada utakapouona ,CCM wanatumia mwisho wa kufurukuta kwa akina Slaa kwa kujiuzulu ,kubadilisha Mawaziri na kujinadi kwa wananchi kuwa CCM ni Chama ni imara kwa kuwa kinasikiliza matakwa ya wananchi na wakiona kiongozi mbovu wanamuondoa mara moja ,hivyo ndivyo wanavyojinadi.
Sasa zile purukushani za akina Slaa utaziona hazina faida kwa upande wa upinzani ,si mmeona DC kakumta walimu ,watu wakapiga makelele ,simple tu DC kaondoshwa au tuseme kafukuzwa ,hapo CCM wameshajijenga na walimu wametaka kuandaa maanandamano kumuunga mkono Kikwete au sio na uchaguzi ukifika walimu watakuwa na CCM bega kwa bega ? Hivyo nini faida ya makelele hapa ukumbini ? Je faida ni kufukuzwa kwa DC ,tazama kizungu nkuti hapa wananchi wanamlilia DC na kusema kuwa yeye ni bora kuliko waliokuwa wakipiga makelele ,ni nani hao wanaopiga makelele ,ni mimi na wewe na Slaa na jamii ya akina Zitto.
Sasa tatizo ni kuwa badala ya kuibana serikali jamii ya akina Slaa wanabana mtu mmojammoja na wanaondoka patupu maana CCM wanamuondosha mtu na kumuweka mwingine tayari ushapigwa bao na yule alieondoshwa hafikishwi kwenye sheria anatafutiwa kazi nyingine kama haitoshi hata kwenye Chama hafukuzwi ,sasa ni faida gani inapatikana upinzani gani upo hapo kama si kuisaidia CCM.
Siasa za CUF Zanzibar hazimsemi mtu mmoja mmoja zinawachanganya wote as a Government na hivyo wanamchukukua au wanamteka mwananchi kwa kumuondosha katika ufuwasi wa Serikali iliyopo madarakani na Chama cha serikali hiyo ,hivyo utaliona goli lilivyo . Ila jamii ya akina Slaa wanamfanya mwananchi amuone mtu kuwa ni adui yake na sio serikali na Chama kizima cha CCM ndipo pale CCM wanapozidi kupigilia msumari wakisema huu ufisadi unamhusu mtu peke yake na sio Chama wala serikali. Mpoo ?
Sasa kama upo hapa JF kwa kuhesabu asante , nani kapewa nyingi na nani kapewa kidogo na nani hana hata moja itakupata kazi ,yaani siku zote wewe unachunguza kama nimepewa asante au sijapewa ,jamani hii sasa ni hasara nyingine mpya.Halafu isitoshe kama kweli ulikuwa na ukonsultant au ushauri ungetumia private message lakini kuweka hapa peupe ni njia moja ya kunipiga vita na kunizalilisha ila ndio utakuwa umejitoga.Mwiba
🙂 Najua kama ninachoma ndipo.
Kwa kukusaidia kuangalia data maana huna jingine la kujadili au kusaidia mawazo katika kujenga Nchi yako.Wale polisi waliovuka mpaka serikali yako ya CCM inafaa kuongoza nchi hii mpaka leo haijasema kitu ,zaidi sijui Mkuu wa Mkoa kaenda kasema hivi na vile na mambo sasa ni poa ?Mfano ambao unatakiwa kuibamiza serikali lakini akina Slaa wamelala.
Halafu mara ya pili jaribu kutafuta maana ya Thanks na Thanked na hapo ndipo ulipokwenda mchomo. Samahani ndugu yangu inabidi tufahamishane
Endelea na mahesabu hapa utuletee yako au tuwache watu wa mahesabu wakusaidie na wakupe salio lako
Mwiba
Join Date: Tue Oct 2007
Posts:
1,435
Rep Power: 24
Thanks: 8
Thanked 414 Times in 279 Posts
Credits: 164,426
Mzalendo Halisi
Join Date: Sun Jun 2007
Posts:
2,015
Rep Power: 26
Thanks: 1,305
Thanked
643 Times in
422 Posts
Credits: 47,244