CUF wamtaka Jintao Z'Bar

CUF wamtaka Jintao Z'Bar

Je, Serikali ya Tanzania ina tamko gani kupanga ratiba ya ugeni wa kiongozi wa kimataifa? Rais wa China anakuja na schedule yake, na sidhani ya kwamba raisi wa nchi yetu anaweza kumpangia rais wa China ni sehemu gani za nchi afanye ziara. Kama hamna projects zenye umuhimu kwao hawatatembelea sehemu hiyo ya nchi.

Jaribu kufikiria wewe ni Rais wa Tanzania uunataka kwenda China na pengine umealikwa kwenda huko, utajuwa wapi kwa kutembelea? ukishapata jawabu la suala hilo utakuwa umepata jawabu la uliyoyasema.
 
Mungu atuepeshe tu..kama sii Muungano visiwani ingekuwa kama Comoro!

Sasa watu 1 m hamtaki kukaa pamoja na kuelewana??

Hivi kwa nini Hu hakuamua kwenda Comoro?

Naona mda may be ulikuwa taiti akaishaia Dar!
 
Kwani Makamu wa Rais ambaye maalum kutoka Visiwani hakuwepo kati ya viongozi waliomlaki na kuzungumza na Rais huyo wa China. Haya mambo hayaendi kwa nusu-kwa nusu yakheee

Jee tushauri kuwa mara ijayo Ziara ya Rais ifanywe Zanzibar na Waziri Mkuu awepo kuiwakilisha Tanganyika. Kama mambo hayaendi nusu nusu penye wawili huwepo zamu.
 
Hivi jamani hawa CUF wanaoperate vipi?

On one side, wana CUF wanalalamika kuwa Hu JIn nTao hajaenda Zanzibar

On the other side, Mwenyekiti wao Profesa Lipumba anaonekana ikulu akipeana mikono na HU Jin Tao kwenye hafla ya kitaifa

Hikichama kinaendeshwaje? nacho kina mamlaka mbili?

8D6U7471.JPG

Picha kwa hisani kubwa kabisa ya MICHUZI blog

Kilichoelezwa na CUF ni kuitembelea Zanzibar sio kukitembelea CUF. Yaani mwenzangu unataka kusema kuwa Zanzibar ni CUF. Pia unataka kusema kuwa kuwepo mwakilishi au mzaliwa wa pahala ndio mgeni amefika huko? Ni vyema kuangalia suala kwa macho yasiyo na kengeza.
 
LOL Ngekewa sio makengeza, actually ndo context yenyewe hiyo, CUF wanalalamika nini huku waliwakilishwa na Mwenyekiti wao kwenye hafla? kwani huyu rais wa China lazima afike Zanzibar? na je mawazo ya CUF ni ya wazanzibari wote? Kipi ambacho Hu Jin Tao angefanya zenji ambacho hakingewezekana akiwa bara ukitilia maanani logistics nk?

NA sina mana Zanzibar ni CUF ila wanadai kuwa aende Zanzibar, kwa nini wasidai aende pia Arusha? AU Songea? Kwa nini CUF wadai aende tu sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano,, kwani watu wa Kigoma walimwona?
 
Nyani
.........whats happening dude........kwema huko?
 
..........no man.....peleka kule kunakohusika.....ndio nini ku-flood thread namna hiyo....umesahau sheria za JF..........au Nyama Hatari kaiba password yako......huh
 
..........no man.....peleka kule kunakohusika.....ndio nini ku-flood thread namna hiyo....umesahau sheria za JF..........au Nyama Hatari kaiba password yako......huh

Yeah man..Nyama probably stole my password....you know he did that way back when during the bcstimes.com days....
 
Tungeacha sisi kwanza kulialia na ufisadi. Kama kurejea kupigania haki ni utoto basi na sie ni mitoto mikubwa tunaolilia na ufisadi. Hili unalosema wewe ni sawa na mkuki kwa nguruwe. Hebu tuache kuwabana ili tuone hawatakuwa? Sisi wenyew hatukuwi na kila siku tunatafutia dawa kero za Muungano tangu wakati wa Nyerere hadi huu wa JK. Tuwpe haki ili wasilalamike.

Mkuu Ngekewa nimejaribu kusoma hapo juu, nimeshindwa kuelewa. Nilidhani mada iliyopo hapa ni kwanini Hu Jintao hakwenda Zanzibar na Wazanzibar wanaona sio fair. Sasa hili la mafisadi linahusika vipi ndugu yangu?

Pengine ungeeleweshwa kuwa Zanzibar kama dola haijawahi kutowa mualiko kwa Rais yoyote uliesikia ameenda Zanzibar. Utaratibu wa Marais kwenda Zanzibar ulikuwa ni utaratibu wa kawaida kabla ya Zanzibar kudai kuwa ni nchi kamili. Kinachofanyika sasa ni kuondowa ile dhana ya kuonekana kuwa Rais anakwenda kule na kupokewa kama nchi nyengine. Iwapo kulikuwa na utaratibu basi si vizuri kuuondowa kwa nguvu ya upande mmoja tu kwani Muungano ni ridhaa ya sehemu mbili, sasa iwapo mmoja anajichukulia madaraka ya kila uamuzi ndiko kulikotupeleka tulipo kwenye Muungano wetu.

Sina uhakika kama Zanzibar ni DOLA. Una uhakika Zanzibar ni DOLA Mkuu? Nilidhani inaeleweka kuwa kila ziara ya kiongozi wa Taifa lolote anaekuja nchini ina malengo maalum. Na malengo hayo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara, viongozi hao hupelekwa kutembelea maeneo ambayo uhusiano huo unaweza kuthibitika. Sasa sijajua viongozi wanaolalamika Hu Jintao kutoitembelea Zanzibar, walitaka atembelee nini hasa ambacho ni muhimu kwake kukiona? Ama alitakiwa tu afike Ikulu ya Zanzibar na kupiga picha na Rais wa Zanzibar? Kama hilo ndilo hitaji, basi ingeweza kuangaliwa kama alikuwa na muda wa ziada wa kuchezea namna hiyo.

Jaribu kufikiria wewe ni Rais wa Tanzania uunataka kwenda China na pengine umealikwa kwenda huko, utajuwa wapi kwa kutembelea? ukishapata jawabu la suala hilo utakuwa umepata jawabu la uliyoyasema.

Mkuu Ngekewa, nadhani unafahamu kuwa Rais wa nchi anapokubali kutembelea nchi yoyote, anakuwa na ratiba iliyokamilika. Ratiba hiyo ambayo huwa anapelekewa na Ubalozi wake katika nchi anayotembelea, huwa ndio kigezo cha kuhalalisha matembezi yake hayo. Ni mabalozi mahiri ndio wanaoweza kuwatoa maRais wao nchini kwao au hata kuweka kwenye mipango yao ratiba za kutembelea nchi changa kama zetu. Hayo hufanyika pia kwa kushirikiana na serikali (kwa mfano wetu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Jee tushauri kuwa mara ijayo Ziara ya Rais ifanywe Zanzibar na Waziri Mkuu awepo kuiwakilisha Tanganyika. Kama mambo hayaendi nusu nusu penye wawili huwepo zamu.

Swali lako hapo juu ni la kiushindani zaidi kuliko hoja halisi. Rais wa nchi yoyote anapokuja nchini, mwenyeji wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hivyo ni lazima atafika Dar es Salaam ambapo ndio yalipo makazi wa Rais wetu. Hilo la kupokezana ili kuwa na uwiano halipo kwenye itifaki (protocol) za mapokezi ya maRais hasa hapa kwetu. Kinachoweza kufanya hilo liwezekane, ni kuhamisha makazi maalum ya Rais kuwa Zanzibar. Nahisi hilo lingekuwa jambo zuri kwa kudumisha Muungano.
 
Zanzibar ni dola na itabakia kuwa hivyo ,kwa vigezo vyote ambavyo ,mwenye ubavu anaweza kuviweka hapa basi aviweke ili tuone ! Haya manying'inya ya kuchomekea ni ukaliaji wa mabavu na kila anaekabidhiwa Ujemedari anajiona ana nguvu za kusema na kufanya atakalo ,wanasahau kuwa mambo kangaja ,Mkapa na ushupaliaji wake wote kufika hata kuuwa Wazanzibari kwa kasi hiyo hiyo ya kuulinda Muungano ,leo yupo wapi ,anasakwa kama ndezi ajibu tuhuma ,mbona hatuoni Ujemedari wake ,kama Jemedari kweli ajitokeze na kujibu shutuma kibao azipinge ,awe tayari kuitwa ili kuzabwa masuali ? Hawa wanaosema Zanzibar si Nchi ni dizaini za akina Mkapa ,wanajiona wao wapo top ,ndio wameshafika ,wanasahau msemo wa kiswahili usemao ..Mpanda ngazi hushuka. Basi Jemedari Mkapa akae akijua kizimba kinamzubiri.
 
Mwiba,

Kaazi kweli kweli!

Yaani posts zako hakuna Thanks hata moja!!! kwa nini?

Fanya reality check...kuna taabu mahali nadhani!

Maneno mengi!!! Substance kidogo!!!

Samahani ndugu na rafiki yangu!
 
Mwiba,

Kaazi kweli kweli!

Yaani posts zako hakuna Thanks hata moja!!! kwa nini?

Fanya reality check...kuna taabu mahali nadhani!

Maneno mengi!!! Substance kidogo!!!

Samahani ndugu na rafiki yangu!
Naenda kivyangu vyangu,mpaka nitaeleweka,si unajua kuna tatizo la wachangiaji ,wengi wetu mnaendeleza hisa za CCM ,hivyo sitegemei kupewa asante kwa kumsema Kikwete au Slaa au Zitto maana hawa wote ni kundi moja.Sio Chama kimoja nimesema kundi moja.
Kikwete anaibeba CCM kuwepo madarakani halikadhalika Slaa na Zitto ndio hivyo hivyo wanasaidia kwa kiasi kikubwa kuipa tamaa CCM.
Mimi ni tofauti na misimamo ya Slaa na wenzake ,Jamii ya akina Slaa imezama katika tuhuma kuituhumu CCM ,kuwa ni wala rushwa au mafisadi wakisaidiwa na nyaraka mbalimbali zinazowapa kuwa kifua mbele katika kunadi shutuma hizo ambazo kwa wanavyoona ni za kweli na ziwe za kweli kama zinavyoonyesha katika data zao.

Vipi CCM wananufaika na matangazo ya akina Slaa na kundi lake ,hapa ndipo msaada utakapouona ,CCM wanatumia mwisho wa kufurukuta kwa akina Slaa kwa kujiuzulu ,kubadilisha Mawaziri na kujinadi kwa wananchi kuwa CCM ni Chama ni imara kwa kuwa kinasikiliza matakwa ya wananchi na wakiona kiongozi mbovu wanamuondoa mara moja ,hivyo ndivyo wanavyojinadi.
Sasa zile purukushani za akina Slaa utaziona hazina faida kwa upande wa upinzani ,si mmeona DC kakumta walimu ,watu wakapiga makelele ,simple tu DC kaondoshwa au tuseme kafukuzwa ,hapo CCM wameshajijenga na walimu wametaka kuandaa maanandamano kumuunga mkono Kikwete au sio na uchaguzi ukifika walimu watakuwa na CCM bega kwa bega ? Hivyo nini faida ya makelele hapa ukumbini ? Je faida ni kufukuzwa kwa DC ,tazama kizungu nkuti hapa wananchi wanamlilia DC na kusema kuwa yeye ni bora kuliko waliokuwa wakipiga makelele ,ni nani hao wanaopiga makelele ,ni mimi na wewe na Slaa na jamii ya akina Zitto.

Sasa tatizo ni kuwa badala ya kuibana serikali jamii ya akina Slaa wanabana mtu mmojammoja na wanaondoka patupu maana CCM wanamuondosha mtu na kumuweka mwingine tayari ushapigwa bao na yule alieondoshwa hafikishwi kwenye sheria anatafutiwa kazi nyingine kama haitoshi hata kwenye Chama hafukuzwi ,sasa ni faida gani inapatikana upinzani gani upo hapo kama si kuisaidia CCM.
Siasa za CUF Zanzibar hazimsemi mtu mmoja mmoja zinawachanganya wote as a Government na hivyo wanamchukukua au wanamteka mwananchi kwa kumuondosha katika ufuwasi wa Serikali iliyopo madarakani na Chama cha serikali hiyo ,hivyo utaliona goli lilivyo . Ila jamii ya akina Slaa wanamfanya mwananchi amuone mtu kuwa ni adui yake na sio serikali na Chama kizima cha CCM ndipo pale CCM wanapozidi kupigilia msumari wakisema huu ufisadi unamhusu mtu peke yake na sio Chama wala serikali. Mpoo ?
Sasa kama upo hapa JF kwa kuhesabu asante , nani kapewa nyingi na nani kapewa kidogo na nani hana hata moja itakupata kazi ,yaani siku zote wewe unachunguza kama nimepewa asante au sijapewa ,jamani hii sasa ni hasara nyingine mpya.Halafu isitoshe kama kweli ulikuwa na ukonsultant au ushauri ungetumia private message lakini kuweka hapa peupe ni njia moja ya kunipiga vita na kunizalilisha ila ndio utakuwa umejitoga.Mwiba🙂 Najua kama ninachoma ndipo.
Kwa kukusaidia kuangalia data maana huna jingine la kujadili au kusaidia mawazo katika kujenga Nchi yako.Wale polisi waliovuka mpaka serikali yako ya CCM inafaa kuongoza nchi hii mpaka leo haijasema kitu ,zaidi sijui Mkuu wa Mkoa kaenda kasema hivi na vile na mambo sasa ni poa ?Mfano ambao unatakiwa kuibamiza serikali lakini akina Slaa wamelala.

Halafu mara ya pili jaribu kutafuta maana ya Thanks na Thanked na hapo ndipo ulipokwenda mchomo. Samahani ndugu yangu inabidi tufahamishane
Endelea na mahesabu hapa utuletee yako au tuwache watu wa mahesabu wakusaidie na wakupe salio lako

Mwiba
Join Date: Tue Oct 2007
Posts: 1,435
Rep Power: 24
Thanks: 8
Thanked 414 Times in 279 Posts
Credits: 164,426

Mzalendo Halisi
Join Date: Sun Jun 2007
Posts: 2,015
Rep Power: 26
Thanks: 1,305
Thanked 643 Times in 422 Posts
Credits: 47,244
 
Last edited:
Recta,
Swali lako hapo juu ni la kiushindani zaidi kuliko hoja halisi. Rais wa nchi yoyote anapokuja nchini, mwenyeji wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hivyo ni lazima atafika Dar es Salaam ambapo ndio yalipo makazi wa Rais wetu. Hilo la kupokezana ili kuwa na uwiano halipo kwenye itifaki (protocol) za mapokezi ya maRais hasa hapa kwetu. Kinachoweza kufanya hilo liwezekane, ni kuhamisha makazi maalum ya Rais kuwa Zanzibar. Nahisi hilo lingekuwa jambo zuri kwa kudumisha Muungano.
Mkuu maneno yako sawa kabisa lakini pia tukumbuke tuna Ma Rais wawili mkuu wangu.. Kwa mfumo wa uongozi unaotambua rais kuwa kiongozi wa nchi hapa tumechemsha! haiwezekani nchi (dola) moja kuwa na rais wawili pasipo kusema kuna dola mbili..Hivyo mgeni yoyote wa nje anapokuja Tanzania ni mgeni wa dola mbili zilizoungana kimiujiza..Pacha walioungana na ku share moyo mmoja..
Hakuna nchi duniani yenye marais wawili isipokuwa Tanzania hivyo tusichukue mifano ya nchi yenye rais mmoja tukaipachika kwetu.. Why tuna marais wawili ni swali la kuwauliza wale wanaosema Zanzibar sio nchi - imekuwaje kuwaje!
 
Mkuu Mkandara, hapo mi simo! KUmbe kidonda bado kibichi kabisa!
 
Hao CUF sasa naona wameishiwa, kilichobaki ni kuimba Mipasho. Ni bora waanzishe kikundi cha Taarab kabisaa (CUF Modern Taarab). Tamko lao na hotuba zilitolewa na Mahali Seif na Wapambe wake kwenye mkutano wao wa kukumbuka waanga wa machafuko ya Zenji (2001) pale Kibanda Maiti hazina tofauti na nyimbo maarufu za migasho huko zenjy (Mdebwedo).

Badala ya kutumia kipindi hiki cha kulelekea uchaguzi wa mwaka 2010 kujenga hoja na kuwaelimisha wapiga kura wao, wenyewe wanabaki kulalamika na kukoroma tu. What 4????

Hivi walijua sababu iliyomleta huyo rais wa China????????

Ndani ya Serikali ya Muungano wa Tanzania (United Republic of Tanzania) kuna mikoa 26.Kati ya hiyo, mikoa mitatu ni ya Tanzania Viziwani. Hivyo HAKUNA nchi ya Zanzibar. Waelezwe mara ngapi hadi waelewe??? Pia kuna Rais mmoja tu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Hakuna marais wawili).

Huyo Rais wa China kama angekuwa na sababu ya kwenda Zanziba ingekua ni sawa na kwenda kwenye mikoa mingine ya Tanzania eg. Kilimanjaro, Mbeya, Mkoa wa Magharibi, Pemba, Unguja, Kigoma n.k lakini si kwa sababu eti ni kuitembela kama "Nchi ya Zanzibar".

Nanukuu...."mahusiano kati ya Zanzibar na Marekani yanarudi nyuma tangu mwaka 1833 kwa kufunguliwa ubalozi rasmi wa Marekani mjini Zanzibar"

Jamani, hivi huyo aliyeandika taarifa hii alikusudia nini??? Mahusiano ya kibalozi kati ya Marekani na Zanzibar 1833, yalikuwa ni Kati ya Marekani na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Kati ya Marekani na Wakoloni (Waingereza/Waarab) waliokuwa wanafanya biashara ya watumwa kipindi hicho???

Tunahitaji viongozi wa vyama vya upinzania wenye kujenga hoja za msingi (e.g CHADEMA) dhidi ya chama tawala (CCM)..sio viongozi walalamishi tuuuuu.

Kutokana na ufinyu wa hoja za baadhi ya viongozi wa CUF, ninakosa imani iwapo wataweza kuingoza nchi yetu tulivu ya Tanzania iwapo nitawapa kura yangu muhimu. Kuna haja ya kuwachagua CUFUUUU??????? I wonder!!!!!!!!!!!
 
LOL Ngekewa sio makengeza, actually ndo context yenyewe hiyo, CUF wanalalamika nini huku waliwakilishwa na Mwenyekiti wao kwenye hafla? kwani huyu rais wa China lazima afike Zanzibar? na je mawazo ya CUF ni ya wazanzibari wote? Kipi ambacho Hu Jin Tao angefanya zenji ambacho hakingewezekana akiwa bara ukitilia maanani logistics nk?

NA sina mana Zanzibar ni CUF ila wanadai kuwa aende Zanzibar, kwa nini wasidai aende pia Arusha? AU Songea? Kwa nini CUF wadai aende tu sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano,, kwani watu wa Kigoma walimwona?

Bwana wa Arusha wana yao na husikia wakilalamika katika bunge la Tanganyika. Hawa Wazanzibari hawawakilishwi mambo yao kwenye Bunge la Tanganyika.
Jee unaonaje Ziara zikawa zinafanyika Zanzibar tu nanyi mkawa mnawakilisha na MH. Mbowe?
 
Mkuu Ngekewa nimejaribu kusoma hapo juu, nimeshindwa kuelewa. Nilidhani mada iliyopo hapa ni kwanini Hu Jintao hakwenda Zanzibar na Wazanzibar wanaona sio fair. Sasa hili la mafisadi linahusika vipi ndugu yangu?

Sina uhakika kama Zanzibar ni DOLA. Una uhakika Zanzibar ni DOLA Mkuu? Nilidhani inaeleweka kuwa kila ziara ya kiongozi wa Taifa lolote anaekuja nchini ina malengo maalum. Na malengo hayo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara, viongozi hao hupelekwa kutembelea maeneo ambayo uhusiano huo unaweza kuthibitika. Sasa sijajua viongozi wanaolalamika Hu Jintao kutoitembelea Zanzibar, walitaka atembelee nini hasa ambacho ni muhimu kwake kukiona? Ama alitakiwa tu afike Ikulu ya Zanzibar na kupiga picha na Rais wa Zanzibar? Kama hilo ndilo hitaji, basi ingeweza kuangaliwa kama alikuwa na muda wa ziada wa kuchezea namna hiyo.

Mkuu Ngekewa, nadhani unafahamu kuwa Rais wa nchi anapokubali kutembelea nchi yoyote, anakuwa na ratiba iliyokamilika. Ratiba hiyo ambayo huwa anapelekewa na Ubalozi wake katika nchi anayotembelea, huwa ndio kigezo cha kuhalalisha matembezi yake hayo. Ni mabalozi mahiri ndio wanaoweza kuwatoa maRais wao nchini kwao au hata kuweka kwenye mipango yao ratiba za kutembelea nchi changa kama zetu. Hayo hufanyika pia kwa kushirikiana na serikali (kwa mfano wetu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Swali lako hapo juu ni la kiushindani zaidi kuliko hoja halisi. Rais wa nchi yoyote anapokuja nchini, mwenyeji wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hivyo ni lazima atafika Dar es Salaam ambapo ndio yalipo makazi wa Rais wetu. Hilo la kupokezana ili kuwa na uwiano halipo kwenye itifaki (protocol) za mapokezi ya maRais hasa hapa kwetu. Kinachoweza kufanya hilo liwezekane, ni kuhamisha makazi maalum ya Rais kuwa Zanzibar. Nahisi hilo lingekuwa jambo zuri kwa kudumisha Muungano.

Naona yote unayoyaeleza ni nadharia sio application iliyokuwepo hapa Tanzania.
Marais karibu wote wanaokuja hapa Tanzania huwa wanakwenda Zanzibar, sasa hizo nadharia zako zina maana gani? Kama kule Zanzibar hakuna cha kufanya kama unavyohisi wewe basi wakubwa wako ndio wapungufu kuruhusu mtu aende pahala pasipo na maana.
Kuhusu suala langu si ushindani bali ni kukuonyesha vile ambavyo viatu walivyovaa Zanzibar mgekuwa mmevivaa nyie. Angalia ni Muungano gani wa mmoja kujiona Bora kuliko mwengine. Hata hivyo Bwana Mkubwa Kama JK ni Rais wa Tanzania na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kuna ubaya gani akampokea huyo mgeni wake kule Zanzibar na si lazima ahamishe makazi ndio akampokee kule Zanzibar.
Nafikiri kaha ipo haja ya kuimarisha Muungano basi utaratibu ule wa awali uuendelee kwani huku Bara tumewahi kupungukiwa na nini eti kwa Rais wa nchi nyengine kutembelea Zanzibar.
 
Back
Top Bottom