Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 666
- 1,277
UCHAGUZI WA MWAKA 2020: Chama cha Wananchi CUF chataka mazingira mazuri
Chama cha wananchi CUF kimetoa wito kwa Rais John Magufuli kukutana na viongozi wa Vyama vya Siasa ili kuweka mazingira mazuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Prof Ibrahim Lipumba katika mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam wakati akitoa salamu za mwaka mpya wa 2020
Katika hatua nyingine chama cha Wananchi CUF kimejipanga kuweka wagombea nchi nzima katika ngazi zote madiwani, wabunge na Rais hivyo tunawaomba watanzania wote kuwa imara katika kuhakikisha kuwa uchaguzi Mkuu 2020 unakuwa wa huru na wa haki.
Prof Lipumba amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kuamua mambo yanayogusa maisha yao ni suala muhimu la maendeleo endelevu na ujenzi wa demokrasia ni sehemu muhimu ya maendeleo na kuwanyima wananchi kuchagua viongozi wanaowataka ni kudumaza maendeleo ya kisiasa na kijamii. Sisi Chama cha wananchi CUF ndicho chama kitachoingia IKULU Mwaka 2020