CUF yaungana na CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wowote hadi ipatikane Tume Huru

CUF yaungana na CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wowote hadi ipatikane Tume Huru

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Chama cha CUF kimesema hakitashiriki uchaguzi wowote utakaoitishwa kwa sababu bado wanapima hali ya kisiasa nchini ikiwemo uhalali wa tume ya uchaguzi.

Mwenyekiti Prof Lipumba amesema maamuzi hayo yamefikiwa na kikao cha kamati kuu.

Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilishatoa msimamo ke huo wa kutoshiriki uchaguzi wowote hadi ipatikane Tume huru.

Chanzo: Star tv

Ramadhan Kareem!
 
Haya ni maamuzi bora sana. Hivi ndivyo inavyopaswa kuwa. Ni lazima kujitoa muhanga, kuumia, kukosa ruzuku, kukaa nje ya Bunge na kufeel pinch kama Taasisi sasa kwa manufaa makubwa ya baadae

Zitto na ACT Wazalendo yake ni wachumbia tumbo tu wasio na nia ya dhati ya kuona mabadiriko chanya. Ngoja wapigwe kipigo cha mbwa koko huko Muhambwe Kibondo ili akili zao zikae sawa
 
Nina uhakika CHADEMA watashiriki uchaguzi 2025 hata bila ya uwepo wa tume huru, Kauli nyengine ni kujitengenezea mazingira ya kuja kudharaulika tu mbeleni.
 
WASIPOSHIRIKI SAWA ILA SHIDA KUNA WAPINZANI WENGINE WATASHIRIKI NA UCHAGUZI UTAFANYIKA HAPO NDIPO WATAKAPOPIGWA BAO
 
Chama cha CUF kimesema hakitashiriki uchaguzi wowote utakaoitishwa kwa sababu bado wanapima hali ya kisiasa nchini ikiwemo uhalali wa tume ya uchaguzi.

Mwenyekiti Prof Lipumba amesema maamuzi hayo yamefikiwa na kikao cha kamati kuu.

Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilishatoa msimamo ke huo wa kutoshiriki uchaguzi wowote hadi ipatikane Tume huru.

Source Star tv

Ramadhan Kareem!

Kikao cha kamati kuu cha watu watatu? CUF ishakufa imebakia na watu watatu tu ,kambaya,sakaya na le profeseli.
 
Asije akaitwa ikulu huyo akabadilika, kila mmoja agome kushiriki kimpango wake.
 
Back
Top Bottom