IGP mteule Ernest Jumbe Mangu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Singida na alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Tumaini mwaka 1981.
By :
Alijiunga na Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) tarehe 17 mwezi Agosti mwaka 1982 na kuhitimu mwezi Juni mwaka 1983 ambapo alipata mafunzo ya awali ya Polisi.
Mwaka 1987 alipata mafunzo ya sheria kwa ngazi ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwezi Novemba mwaka 1992 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mwezi Juni mwaka 2010, alitunukiwa shahada ya udhamili katika masuala ya usalama katika Chuo Kikuu Cha Usalama cha Marekani.
Akiwa ndani ya Jeshi la Polisi amepandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Koplo wa Polisi (1988), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1992), Mkaguzi wa Polisi (1995), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (1997), Mrakibu wa Polisi (2002), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2004), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2006), Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (2010), Naibu Kamishna wa Polisi (2013) na Kamishna wa Polisi (2013).
Amewahi kufanya kazi kama Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza, Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Pwani na Mwanza na Kamishna wa Intelijensia ya Jinai.