Cwt kukata mishahara ya walimt

Cwt kukata mishahara ya walimt

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Matunda ya TTN/UMET yanaendelea kuonekana. Serikali imetoa Waraka kuwa Tarehe 30/6/2013 ni mwisho wa CWT kukata mishahara ya Walimu. Viongozi wa CWT wanazunguka kuwataka Walimu wajaze Fomu no:T.U.F.6 ili waendelee kukatwa mishahara yao,Ewe Mwalimu,kataa unyonyaji huu.TTN/UMET/CHAKEMWATA ni mkombozi wako.Tuma ujumbe huu kwa walimu wengi uwezavyo. KWA PAMOJA TUMESHINDA!

Ujumbe huo unaendelea kusambazwa na walimu. CWT inaelekea kufa.
 
Walimu linawahusu hili. Mleta mada hiki ulichopost sijui kama kitaeleweka kwa wengine jaribu kufafanua vizuri.
 
Ok vizuri mkubwa, ila TTN/UMET/CHAKAMWETA ni nini? naomba nifahamishe ndugu
 
Ttn nayo itakuja na matatzo yake so suala si kuivunja kwani inapelekea divide n rule,mnapaswa kuwa na umoja na kuifanyia mabadilko sio kufurahia tu na muangalie na hasara zake pia. Mmtambue adui yenu ambaye si cwt lazvyo mtaendelea kunyonywa tu.
 
hata hivyo makato ya cwa ni makubwa mno wakati msaada wao kwa walimu ni mdogo.
Naunga mkono hoja,makato yasitishwe.Walimu wakubaliane na vyama kwa hiari yao na si kukatwa bila ridhaa yao.
 
Afadhali waache kutuibia aisee. Hizo form ni zipi jamani isije kuwa ni zile walizosambaza miezi kadhaa ku update taarifa za wanachama na kuwapa kadi walimu wanachama. Kaa ndio hizo mbona majanga!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Tatizo cwt hawakusoma alama za nyakati na pia walishupaza shingo,wangeanza kwa kupunguza tozo ya 2% wanazowakata walimu kwani wameshajijenga vya kutosha. Umet watakata 0.2% ya mshahara,je unafikiri kuna mwalimu atakaekubali kuendelea kunyonywa na cwt? Hata hivyo kuliangalia vizuri hili swala ni lazima kwani twaweza gawanyika na serikali kupata nafasi ya kutukandamiza vizuri. Naamini cwt wataiangalia upya katiba yao,then tutafanya uchaguzi bora.
 
mleta uzi huu ni janga, umeleta taarf nzur, bila ufafanuzi,ufahamu kuwa unachochea kitu kizur kw walim kibaya kwao, ni wkt ambapo cwt wanafanya kila mbinu wawarubuni walimu.


my take Serikali inajua kwa mbinu hii zile asilimia mbili 2% kwa mfano mwalim anaechukua 720000/- atakua amepata 743400/= tayari kuna incriment kama 12,000 itakuwa 746400 bado kuna ongezeko mwaka huo mpya wa fedha chukua labda 20% YA 720,000 Unapata 864,000(mfano tu) jumla 890400

kwa hesabu hii serikali inajua hakuna mwalimu ataekubali kukatwa hii two percent ongeza na ile 1% iliyopunguzwa kwenye pay as you earn basic itasoma 897600 Waziri Willium Mgimwa anajua atendalo, huu ni mfano tu kwa mwalimu aliyekua anapata 720,000, kwa kawaida hawa ni masenior teachers, nimetoa mfano tu wakuu
 
Tatizo nadhani ni kubwa kuliko wengi tunavyofikiri. Mara nyingi vyama vinavyoibuka na kuja na makato madogo huwa ni mapandikizi ya watawala na havina lengo la kumtetea mfanyakazi kwa sababu utetezi ni gharama sana. Kuchangia asilimia 1 au chini ya hapo ni hadaa ya vyama vya kitapeli. Binafsi ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya vyama hivi nikiwa mimi ni mwanachama wa RAAWU, najua ili chama kitoe utetezi mwafaka lazima kiwe na waajiriwa ambao lazima walipwe maslahi yao kutokana na michango ya wanachama sasa huyo anayedai atakata 0.2% kimsingi hizo watakuwa wanatumia viongozi na kutofanya chochote.
Mfano kuna katika kupigania maslahi ya wafanyakazi kuna kamati ya utatu ambayo inajumuisha serikali, vyama vya wafanyakazi chini ya TUCTA na chama cha waajiri. Vyama vingi vinavyoibuka hivi sasa haviko TUCTA kwa hiyo havishiriki utetezi au kupigania maslahi, hayo wanapigania wengine vyenyewe vinanufaika na michango ya wafanyakazi wachache wasio na uelewa wa masuala haya.
Sasa inawezekana CWT wana makosa lakini mimi nadhani ni vema kutatua matatizo yaliyopo kuliko kuua CWT kumbuka atakayenufaika ni serkali na hapo tunakoleza suala la wagawe ili uwatawale (Divide and rule) na pia umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
 
Mleta mada bado huja fafanua hizo TTN/UMWET NA CHAKEMWATA ni vitu gani ati.
NAWAONYA WALIMU, MKIGAWANYIKA HATA KILE KIDOGO MNACHO DAI HAMTAKIPATA!!! period.
1. Jiulizen kwa nini serikali imeleta leo kufanya hivyo ( soma hivi... kudhoofisha umoja wa vyama vya wafanyakazi) jitahidini baada ya kazi ya kufundisha mjisomee na msome nyakati na katikati ya mistari!!!
2. Matatizo ya CWT yanaweza kutatuliwa na ni kipindi cha kureform vyama vya wafanyakazi kwa sasa, ila siyo muda mwafaka wa kuviua.
3. Wingi wa members hasa sector ya elimu na afya ni nguvu ya kutisha kwa mwajiri ikiwemo na serikali yenyewe.

Mwisho kabisa nikumbushe ni kwanini JK alimtaja sana Mgaya, akakataa kura za walimu, kisha akabadili maneno akaziomba?
Nguvu ya umma ni pamoja na vyama vya wafanyakazi vyenye nguvu.
kalagha baho!!
SP
 
Mleta mada bado huja fafanua hizo TTN/UMWET NA CHAKEMWATA ni vitu gani ati.
NAWAONYA WALIMU, MKIGAWANYIKA HATA KILE KIDOGO MNACHO DAI HAMTAKIPATA!!! period.
1. Jiulizen kwa nini serikali imeleta leo kufanya hivyo ( soma hivi... kudhoofisha umoja wa vyama vya wafanyakazi) jitahidini baada ya kazi ya kufundisha mjisomee na msome nyakati na katikati ya mistari!!!
2. Matatizo ya CWT yanaweza kutatuliwa na ni kipindi cha kureform vyama vya wafanyakazi kwa sasa, ila siyo muda mwafaka wa kuviua.
3. Wingi wa members hasa sector ya elimu na afya ni nguvu ya kutisha kwa mwajiri ikiwemo na serikali yenyewe.

Mwisho kabisa nikumbushe ni kwanini JK alimtaja sana Mgaya, akakataa kura za walimu, kisha akabadili maneno akaziomba?
Nguvu ya umma ni pamoja na vyama vya wafanyakazi vyenye nguvu.
kalagha baho!!
SP
ni kweli ndg,mm mwenyewe kila siku nawaambia lakini walimu wanajidai waelewa sana.Wanafurahia Cwt kfa badala ya kufanya mabadiliko wao wanayakimbia matatzo.hasira za mkizi............
 
Matatizo hayeshi hata hiyo UMET n.k itakuja na yake suala la msingi ni kuibana CWT ijirekebishe tuache uboya,tujiulize imekusanya shilingi ngapi kama michango kutoka kwa waalimu?na ikifa ina maana hizo fedha je?tusiufurahie huu mvurugano ambao utainufaisha serikali ya CCM na kuurudisha utumwa wa wafanyakazi!..
Hakuna kisichobadilika chini ya mbadiliko wa wakati na tafakuri za watu waalimu tunapaswa kuamua CWT iweje na tunaweza na siyo utenganoutengano wa kijinga tunaoletewa na sisi kuushangilia.
Mimi ni mwalimu na sijajaza form ya chama chochote ila upo umuhimu wa kujaza na nimeona nijaze mwezi huu wa sita wakisambaza form zao vituoni na nitajaza form ya CWT ila sitoukubali ujinga tena ndani ya CWT.
 
Wizi mtupu 02% ni pesa nyingi sana!

hawa viongozi ni matajiri sana na wamejenga majumba ya kufa mtu kwa jasho la waalimu!

Ni kwa nini kika mwalimu asikatwe tu shs 2,000 au 5,000 flat rate??
 
CWT huwa wanapiga kelele pale tu wanapokuwa na maslahi binafsi,jamaa wengi wa CWT naona ni wapiga deal tu.
 
Wizi mtupu 02% ni pesa nyingi sana!

hawa viongozi ni matajiri sana na wamejenga majumba ya kufa mtu kwa jasho la waalimu!

Ni kwa nini kika mwalimu asikatwe tu shs 2,000 au 5,000 flat rate??
Kama wewe ni mwl kweli jaza hivyo then kikaoni sema flta rate!! badilisha CWT kuwa bora, kuua CWT ni kuua SAUTI ya ya MWL

SP
 
Ivi toka Cwt ianzishwe imefanya nini kwa walimu zaidi ya kujenga majengo?matatizo kwenye ualimu yataisha pale mwalimu husika atakapobadilisha fani na kwenda sehemu nyingine.CWT ikifa or isife hamna la maana kwa walimu.ukomboz ni kubadili fani fullstop
 
Binafsi siutambui msaada wa cwt kwa walimu kwani ni shina la ccm kama kilivyo chama cha wanawake tanzania. hawa cwt huwawanatuzuga tu kwa kutangaza maandamano yaanze ijuma hafu j1 na j2 sio siku za kazi ili ifkapo j3 serikali iende mahakamani.
 
matapeli mara utackia tuna fungua bank uozo mtupu hakuna bank wala ------ wanakula tu pesa yetu hata wenyeviti wa matawi nao wanapo pata migao wanakula bila kushirikisha walimu magnila kinondoni mapinduzi tapeli hata uongozi unajua heri chama life
 
Back
Top Bottom