CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Tumesikitishwa sana na hawa vijana wenzetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioamua kuidhalilisha taasisi nyeti ya Urais Tanzania huenda kwa kujua au kutokujua,
Nikweli, Tunafahamu Rais hufanya UTEUZI kwa mtu yeyote anayedhani anaouwezo wa kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake ya siku kwa siku bila kumtaarifu.
Uteuzi ni ishara ya imani ya kiwango cha juu toka kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuja kwa mteuliwa ikiwa ni pamoja na Ukoo au familia yake.
Hebu fikiri hii, Nchi yenye watu takribani 62M Wewe unateuliwa kisha unamvimbia aliyekupatia hiyo heshima, hakika hili ni jambo baya huenda kuliko Ubaya wenyewe.
Hebu Vijana wa Tanzania bila kujali Itikadi zetu za Kisiasa & dini tujifunze kitu toka kwa aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi & Uenezi wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Mhe Shaka Hamdu Shaka.
Pamoja na kwamba Mhe Shaka Hamdu Shaka ambae Sasa ni mkuu wa Wilaya ya Kilosa alikuwa ni boss wa ma-RCs, ma-DCs, ma-RAS, Mawaziri wote akihudumu kama kiongozi wa ngazi ya juu wa Chama,
Leo sote tumashahidi baada tu ya kuondoshwa kwenye nafasi hiyo na kuteuliwa kuwa DC Kama ilivyo kwa viongozi hao waandamizi wa CWT Jamaa hakuhoji, hakususa Wala kukunja sura bali alikuwa ndio DC wakwanza kula kiapo miongoni mwa ma -DC wote walioteuliwa katika batch ile.
Tunahitaji kuwa na Taifa lenye vijana wenye nidhamu ya Uongozi na viongozi aina ya akina Shaka Hamdu hasa kwa kulinda Mila na Desturi zetu kama Watanzania kwani ni mbaya kutumwa na mkubwa hata kama hana cheo ukakataa.