CWT mnaomvimbia kichwa Rais jifunzeni unyenyekevu wa Shaka Hamdu Shaka mtafika mbali vyeo ni dhamana ya muda Tu

Kumbe CCM imeweka makada kwenye Chama cha Walimu....!?
 
Wewe unaoushahidi wa unayoyasema?
 
Hao wamekataa uteuzi kwasababu ya maslahi yao binafsi na wala si kwamba wanatetea taaluma yao!! Kama wangekuwa wanaipenda kweli taaluma yao ya uwalimu wasingekimbilia kugombania vyeo vya kiuongozi huko CWT, wangebaki kufundisha watoto darasani. Yaani kwa kifupi huo ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu kupangiwa kufanya kazi na boss wako mkuu na kumgomea, halafu bado unahitaji ufanye kazi nyingine ambayo boss ndo yuleyule. Mimi ndo ningekuwa boss nisingekubali hiyo dharau
 
Utaratibu sio huo
Utaratibu si hoja.

Hata Afrika Kusini utaratibu ulikuwa kuwabagua weusi, lakini ubaguzi huo kuwa utaratibu hakukufanya utaratibu huo kuwa wa sawa, wa haki wala wa mantiki.

Kumteua mtu bila kumuarifu asikie uteuzi redioni hakuna haki, hakuna mantiki.
 

Kwanini uteuzi unafanyika bila kuwasiliana na wateuliwa. Yaani wewe una familia yako, hujaomba kazi yeyote unafanya kazi nyingine kabisa ambayo haina uhamisho halafu unateuliwa kuwa mkuu wa wilaya! bila ya kuambiwa na huwezi kuukataa sasa hiyo siyo demokrasia. Kama mtu huwezi kazi ni bora ukatae kuliko kwenda kwenye kazi ambayo huipendi au familia yako haiko tayari. Hata mimi kama nina biashara zangu nisingekubali ukuu wa wilaya au ukuregenzi. Hizi kazi nilazima uwe na muda sana, uwe tayari kumbizana na hazina mishahara ya maana. Hizi ni nzuri kwa wale jobless
 
Wengi wakiarifiwa wameshindwa kutunza Siri Ndio sababu za kutowataarifu, wengine wanafanya na sherehe kabisa
 
Dawa ya pale CWT pelekeni CAG ili pawe mtafutano maana wale mbuzi wanatafuna sana fedha za walimu,na ndio maana kwa mfano pale Sumbawanga wamehonga Mkurugenzi na Afisa Utumishi ili waendeleze zengwe kwa walimu wanaojitoa CWT na kwanda CHAKUHAWATA.Serikali ya Samia inapenda kuchezewa kwa sababu imekumbatia wajinga wengi hilo ndio tatizo kubwa kuliko.
 
Wengi wakiarifiwa wameshindwa kutunza Siri Ndio sababu za kutowataarifu, wengine wanafanya na sherehe kabisa
Ukishakuwa na watu ambao wakiarifiwa hawatunzi siri, tatizo lako si taarifa tatizo lako ni hao watu.

Kama unatatua tatizo hilo kwa kubadili taarifa inavyotolewa, badala ya kubadili mzizi wa tatizo, ni kama unatibu mgonjwa wa kifua kikuu kwa kumpa Cofta ya kupunguza kikohozi.
 

Sio kila mtu ana shida kama huyo Shaka. Kwanza hii tabia ya wazanzibari kupata madaraka huku, wakati Wabara hawakubaliwi Zanzibar bado tunawacheck sana.
 
uchawa unakusumbua. Unadhani kila mtu ni chawa mbupavu sana nyinyi mi UVCCM
 

Mnataka rais asujudiwe, wakati raia akiona hataweza kutumikia cheo fulani akawa mkweli basi mna msakama wakati kuna raia watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18 wapatao milioni 23 ambao baadhi yao kwa makumi ya maelfu wangeweza kukubali wadhifa huo.

Tujenge kizazi cha kweli kinachoweza kusema asante umeona nafaa lakini nasikitika sijioni kuwa na wito iwe wakati wa kuteuliwa na hata kujiuzulu pale wanapoona hawajafikia malengo tarajiwa au wanapiashana maono na bosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…