Mpwayungu Village
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 14,540
- 30,875
Nimelia sana [emoji22]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimelia sana [emoji22]
Walimu wakatae kuchangampwayungu village una maoni gaNi
Chuki hii dhidi ya hawa mashujaa wetu wanaotuandalia kizazi kijacho huku wakidharauliwa na kutukanwa hivi inatokana na nini hasa?Kada ya kipumbavu dunia nzima n ualimu kwa Tanzania. M nainjoi kuwaona hivyo hao washenzi
Acha kujitia moyo. Mtaani kunahitaji watu wajanja na wapambanaji. Na siyo watu wa aina yako ambao mnalalamikia michango ambayo hamjalazimishwa kutoa. Mnatishiwa nyau, na nyinyi mnaogopa!Ndiyo maana nimeandika kwa Uchungu mkuu!.
Nafanya mpango aachane na hii kazi inayoitwa ya LAANA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah.Ukiwakuta na vishikwambi vyao sasa...mmoja akaropoka vinauzwa mil 3...nikabaki namtazama tu na kumuona mwehu...shida sio uwalimu ni walimu wa siku hiz...wanashindwa shtuka kuwa serikal inawaendesha...kwa technolojia ya miaka ya 80...na wenyewe wanauvaa mkenge...lazima utawaona wehu..
Hata mie naumia walimu wakisimangwaa, ila sina namna tyuuh, aaaahChuki hii dhidi ya hawa mashujaa wetu wanaotuandalia kizazi kijacho huku wakidharauliwa na kutukanwa hivi inatokana na nini hasa?
Sijawahi kuona ko kote kule duniani ambako nimewahi kufika walimu wakichukiwa na kudharaulika maana kimsingi wao ndiyo wameshikilia uhai wa taifa lo lote lile.
Kwa nini mnawachukia walimu kiasi hiki?
View attachment 2567378
Watagoma kulipa vip wakati hela inakatwa automatic kwenye mshaharaTatizo lenu amna umoja hivi mkiamua Tanzania nzima amlipi hyo pesa mnagoma hivi mtafutwa kazi nyote au mtahamishiwa vijijini nyote? amueni ninyi vitu vingine sio lazima mbaka rais aseme mnamchosha
Kama hvo kunashidah upande wa serikali hila wadau wengi nimewauliza wanasema ni mkononi inakusanywa hiyo pesaWatagoma kulipa vip wakati hela inakatwa automatic kwenye mshahara
Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Kwa ushahidi wa barua hii ndugu walimu wanampelekea mkuu wa shule hyo pesa yeye ndio anaratibu hlo zoezi then kwa pamoja baada ya makusanyo wataingiza hzo pesa kwa hzo account number walizopewa kwahiyo hapo awakatwi automatically kwenye mishahara yao bali wanapeleka manually kwa mkuu wao wa shule so hapo wanaweza kugoma tu Tanzania nzima waache uogaWatagoma kulipa vip wakati hela inakatwa automatic kwenye mshahara
Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Hii nchi ngumu sanaChuki hii dhidi ya hawa mashujaa wetu wanaotuandalia kizazi kijacho huku wakidharauliwa na kutukanwa hivi inatokana na nini hasa?
Sijawahi kuona ko kote kule duniani ambako nimewahi kufika walimu wakichukiwa na kudharaulika maana kimsingi wao ndiyo wameshikilia uhai wa taifa lo lote lile.
Kwa nini mnawachukia walimu kiasi hiki?
View attachment 2567378
Barua yenyewe sasa tungeiona Ina maneno gani piaNsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!
Kila mwaka kumekuwa na madai ya walimu kuchangia katika michango mbalimbali ya shughuli za kiserikali kwa ushurutishwaji hasa na wakurugenzi wa Halamashauri ama manaibu wakurugenzi.
Moja wapo ya kilio cha muda mrefu kwa walimu ni hii kero ya Michango ya mbio za Mwenge kila mwaka.
Sasa kuna barua ambayo inasambaa mitandaoni kutokea huko Halmashauri ya mji wa Ifakara ikionekana kuwataka walimu kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya mbio za mwenge wa mwaka huu 2023,ambapo imesema kila mwalimu mkuu atachangia elfu 50,000/= na walimu wa kawaida itawapasa kuchangia elfu 5000/=.
Kibaya zaidi ukigoma kuchangia michango hiyo unaambiwa hutapewa vipaumbele kama hutapewa fursa ya miradi ya serikali inayowahusu walimu n.k, na kama mkurugenzi hajaridhishwa na adhabu hizo utaambiwa uandike barua ya kujieleza kwanini umegoma kuchangia maendeleo na utawekwa kwenye list ya walimu wanaopaswa kukomolewa,ni eidha utimuliwe kwasababu lukuki au uhamishiwe vijijini huko ndani ndani ili ukaipate fresh.
Huu ni uonevu mkubwa ambao kila mwenye akili timamu anapaswa kuupigia kelele kwa nguvu zote.
Wakati ambao watu wenye akili timamu tunapinga huu uonevu kuna Shirikisho la Umoja wa Walimu Tanzania almaarufu kama CWT ambao wao ndiyo wenye mamlaka ya kulipigia kelele suala hili.
Miaka yote Chama hiki cha Walimu kimeendelea kukaa kimya pale ambapo walimu wamekuwa wakionewa na serikali,Chama hiki huwa kinaibuka wakati kikiwa na migogoro ya kimaslahi hasa kipindi cha Uchaguzi wa ndani wa Chama wa kuwachagua viongozi, lakini tofauti na hapo hakina msaada kwa walimu zaidi ya kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kuendelea kubaki madarakani.
Hivi Viongozi wa CWT mnaakili timamu kweli? Ni lini mtawapambania walimu waondokane na huu udharimu?,Hili suala halipo kisheria na ndiyo maana walimu wanalipigia kelele kila siku lakini nyie mmeendelea kupiga kimya huku mkipokea mafungu kutoka serikalini mkishibisha matumbo yenu na kujaza matako ili kila mpitapo basi watu wageuke kuwatazama mlivyoshiba pesa za dhulma!.
Walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu na bado mshahara ni mdogo lakini hapo hapo kwenye hako ka Mshahara na serikali pia bado inaendelea kuwakamua kila uchwao.
Hivi huo mwenge unafaida gani? Kama kitu kinaendelea kula pesa na Kodi za watanzania pasipo kuingiza pesa kina faida gani? Huo mwenge kwanini usiwekwe makumbusho uenda ukaliingizia taifa fedha kuliko hivi sasa kutumia fedha na gharama kubwa?
Hakuna mtu mwenye akili timamu leo ukamuuliza huo mwenge una faida gani akakujibu,labda awe mwendawazimu!
Nyie CHAMA CHA WALIMU ni MATAPELI mnaokula jasho la walimu na kuwanyonya!.
OMBI KWA WALIMU WENYE AKILI TIMAMU
Achaneni na CWT bali hamieni CHAKUWAHATA(Chama Cha Kulinda na Kutetea Haki za walimu Tanzania),Huko CWT mtanyonywa hadi mbaki na mafuvu!.
HIKI CHA MA CHA WALIMU HAKINA FAIDA KIFUTWE.
#Ukilala nayo hakikisha unaamka nayo!.
Ni hayo tu.
Chaka la serikali kivipi kama wewe ni mwalimu halafu huwezi kujenga hoja ni tatizo. Nataka uniambie namna gani cwt imekuwa chaka la upigaji.CWT ni Chaka la serikali kupigia walimu,
Haifai hata kidogo.
Siyo lazima ila kila mwalimu lazima awe mwanachama wa chama cha walimu. Elewa maelezo. Hata mkiwa 10 mnaweza kuanzisha chama cheni.Kwani waalimu ni lazima kuwemo kwenye hicho chama?