Ndugu mwandishi,
Bahati mbaya umetaja CWT peke yake, labda kwa sababu familia yako inaathirika na chama hicho. Na pia popularity ya hiki chama, kutokana kuwa walimu ni kada yenye watumishi wengi zaidi wa umma Tanzania hii.
Lakini mimi naomba nikuhakikishie kuwa, hili sio CWT peke yake. Ni vyama vyote vya Watumishi (Workers' Union) vinakata mishahara ya watumishi na hakuna kinachofanyika.
Imagine, kila mwezi watumishi wote wanakatwa 2% kutoka kwenye mishahara yao. Na hii ni sheria eti, imepitishwa na bunge letu tukufu.
Mbaya zaidi, kama mtumishi hataki kujiunga chama chochote, anakatwa bila kupenda. Hii inaitwa ada ya uwakala. Ni sheria pia imepitishwa na bunge letu tukufu. Hii ada ya uwakala pia wanakata 2% kama mwanachama.
So hivi vyama vyote, CWT, TALGWU, TUGHE hakuna kitu cha maana sana vinafanya. Ni mpango wa kula fedha za watumishi tu.