Daaah, bodaboda bodaboda...inauma sana


Sahihi mkuu, Serikali iwezeshe Vijana. Nguvu kazi kubwa la Taifa hili ni Vijana, Sasa vijana wakiwa tegemezi kwa wazee hiyo ni changamoto kubwa sana, vijana wanahitaji kuwa na Familia Bora, na kukiendeleza kizazi chao

Serikali yetu pendwa wekeni mazingira wezeshi ya Vijana kupata kazi Rasmi, na kuweka mazingira Rafiki pale kijana anapojiajiri haswa suala la Kodi kubwa za TRA.

Vijana wanapata msongo wa mawazo sababu ya Maisha Magumu. Vijana na sisi tuache Makundi, Starehe haswa pombe, wanawake. Ukiendekeza pombe, madawa ya kulevya na wanawake kutoboa ni ngumu sana.

Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya Juu, Eid imeisha, tuendelee kuijenga nchi yetu.
 
Kwa mujibu wa CCM hao ni maafisa usafirishaji.
Hiyo ni ajira rasmi kwa sera za chama tawala
 
Kwani gari za Rwanda huwa zinafuta mafuta wapi? Hapo ni TZ nadhani, angalia namba za pikipiki

HAPO NI TABORA MJINI,ENEO LA INALA,HIYO LORI NI LA RWANDA,HUWA YANAPITA HAPA TABORA MJINI YAKIENDA BANDARINI KUCHUKUWA MIZIGO.HUYO SIO BODA BODA,NI MTUMISHI WA SERIKALI KAKA.
 
Kwahiyo hitimishi huyo ni bodaboda, hawezi kuwa mwendesha pikipiki wa kawaida? Mbona hapo chini kuna kabegi, labda alikuwa ni mwanachuo, au kijana mjasiriamali anakimbizana na muda!
Namba za pikipiki ni za kibiashara
 
Ni aibu nchi yenye hekari za mamilioni ya ardhi inayofaa kwa kilimo kuiacha na kusema bodaboda ni ajira. Bodaboda imefanya vijana waingie kwenye unywaji wa pombe kali na mihadarati mingine. Serikali ya mama Samia itafanya jambo jema kama ikitangaza kuwa bodaboda ni janga la kitaifa. Lakini sababu wananufaika kisiasa sidhani kama hilo litakaa lifikiwe. Bodaboda siyo kazi. Nasema na mimi ili mninange
 
Mhh hii picha ya mchongo ukiangalia vizuri. Kwanza hakuna hata damu wala nyama nyama zimetapakaa, pili hakuna hata mashuhuda pembeni wakishangaa, tatu mtu kanasaje hapo maana analingana na gari unene.
Ukiwa ni mtu wa barabarani huwezi sema haya maneno.
 
Naona afisa msafirishaji, aliamua kupark kwa kuweka kwanza stand ya pikipiki kisha akaning'inia.
 
Mhh hii picha ya mchongo ukiangalia vizuri. Kwanza hakuna hata damu wala nyama nyama zimetapakaa, pili hakuna hata mashuhuda pembeni wakishangaa, tatu mtu kanasaje hapo maana analingana na gari unene.
Hiyo picha ni ya kweli na huyo sio boda bali ni mwalimu mmoja wa shule ya msingi huko Tabora. Amezikwa last week huko Same Kilimanjaro
 
Wadudu hao wa Chuga tayari...Ngoja wakazikane kweny migomba
 

Attachments

  • BODA ARUSHA.jpeg
    124.7 KB · Views: 2
  • tTcgvEd7PsuLLtBo.mp4
    1.1 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…