Mwalimu wa Jamii
Senior Member
- Mar 9, 2023
- 162
- 373
Mh. Lema aliposema bodaboda siyo kazi watu walimdhihaki sana. Lakini kiukweli hii siyo kazi. Kwanza inatakiwa ibuniwe Kodi kubwa ambayo itazifanya bodaboda ziadimike barabarani. Nenda kwenye mahospitali yote makubwa na madogo idadi ya waathirika ni kubwa na wafanyakazi wa sekta ya afya ni wachache kuwahudumia waathirika.
Pia serikali yetu tukufu haioni jinsi uchumi wa nchi unavyoathirika na hizi ajali...
Sahihi mkuu, Serikali iwezeshe Vijana. Nguvu kazi kubwa la Taifa hili ni Vijana, Sasa vijana wakiwa tegemezi kwa wazee hiyo ni changamoto kubwa sana, vijana wanahitaji kuwa na Familia Bora, na kukiendeleza kizazi chao
Serikali yetu pendwa wekeni mazingira wezeshi ya Vijana kupata kazi Rasmi, na kuweka mazingira Rafiki pale kijana anapojiajiri haswa suala la Kodi kubwa za TRA.
Vijana wanapata msongo wa mawazo sababu ya Maisha Magumu. Vijana na sisi tuache Makundi, Starehe haswa pombe, wanawake. Ukiendekeza pombe, madawa ya kulevya na wanawake kutoboa ni ngumu sana.
Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya Juu, Eid imeisha, tuendelee kuijenga nchi yetu.