Habari waungwana poleni sana na kazi..
Leo nilimechoropoka ofisin nimekuja hospitali flani ya macho mjini hapa NHC HOUSE kurepair lens za miwani maana macho yangu yanamwaga machozi mfululizo afu yananiwasha.
Sasa wakati nasubiri kuingia kwa doctor nikawa nakagua frem za miwani najaribu hii na ile na nini.
Kiukweli sikuwahi kuingia hospitali hiyo ila ushauri wa washikaji kua jamaa wako vizuri pia wanafremu kali za miwani nikaona nijisogeze nione huduma zao kingine si mbali sana na ofisini na nini sio mbaya.
Zamu yangu ilipofika nikaingia nipate tija ya tatizo langu, Namkuta Dr kakaa yupo, "karibu" huku akiwa busy kukagua vipimo vyangu. Nikakaa,sasa wakati namuangalia vizuri tukagongana ile tunaangaliana, heee!!! Nikawa nimepigwa butwaa naangalia vizuri Dr mwenyewe ni class mate wangu wa primary enzi ziile za mchumba, mchumba wote tukabaki tunaangaliana... Yuko do I know you?
Nikawa Like yah Im Joseph n ur schola right? Aisee aliluka kunihug tukachekaa chit chat finally akaniambia kua tatizo ni lens ya miwani yangu imekua weak so nibadilishiwe.
Sasa wakati ushauri wa ki dr umeisha tukiwa tunaendelea na chit chat akauliza umeoa? nikamwambia ni long story ila to make it short bado life is full of shit, akawa tu excited n yuko aisee umekua mkaka sana with how you look unapaswa kua mume wa mtu... Nikacheka tuu ila kimoyo moyo niko once a gentleman always a gentleman tukapeana mawasiliano n kuplan kumeet again.
Kiukweli amekua mkali haswa yani those ladies of that kind,self made af kastaarabika na nimemuelewa saaana nahisi nikikaa hapa moyo wangu utapoa na ntafika mbali.
Muda huu hapa nachati nae namchombeza kama haniamini amini hivi ila dizaini amenielewa pia maana ana vijimaswali flani hivi vinanifanya natabasamu kila text ya whassap ikitua kwenye simu yangu.[emoji56] [emoji56].
Vipi waungwana Yawezekana hii ndio karata yangu chanya, maana ni muda mfupi ila nimetokea kumuelewa vibaya sana huyu dada af kilichoniua zaidi amekua mzuri haswa,
Nishaurini wadau nichangamkie fursa maana daaah si kwa uzuri ule na ustaarabu ule yani niko salama mpaka rohoni[emoji56] [emoji56].