Daah! Wahuni siyo watu

Daah! Wahuni siyo watu

Toto Zembe

Member
Joined
Jul 15, 2019
Posts
74
Reaction score
99
Jamani wana JamiiForums habari zenu?

Kuna mkasa ulinikuta nikikumbuka nacheka sana[emoji2][emoji2].

Jumamosi moja niliamka ikiwa siku njema sana, ila ilipofika jioni mambo ayakuwa sawa, ishu yenyewe ilikuwa hivi: Si unajua mishe za mjini hapa katika michakato ya kusaka tonge.

Basi nilitoka zangu home nikiwa na elfu tatu kwa jili ya nauli kwenda kazini na kurudi pamoja na kula, basi uko bajeti ilivurugika nikajikuta nimetumia hadi pesa ya nauli ya kurudia. Basi jioni ilipofika si nikagongea nauli kwa mwana; basi mwana akanambia nimsubiri kidogo basi jamaa alipokuja akanifinyia noto lakini hela yenyewe alivonipa alinipa kwa style ya kama tuna shake hands. Basi alivonipa nikaitia mfukoni kwa furaha tele nikijua mambo ni [emoji106]sawa.

Basi nilivyo fika kwenye daladala nikakaa siti karibu na mrembo fulani hivi. Ilivyofika muda wa kutoa nauli si nikatoa ile noti bwana; bwana kumbe noti yenyewe kipande yaani ilikuwa imechanika imebaki kipande nilijuta kuzaliwa basi kama mnavyo wajua makonda na tabia zao alinikazia hadi ikawa noma mwisho wa siku mrembo akani save, tokea pale nilikaa kimya kama nimenyeshewa mvua.

Kwaiyo jamani tukipewa pesa na mhuni tuwe tunachunguza[emoji113][emoji113][emoji113]
 
Na huyo mwana ulimwambiaje mlivyoonana? Kwa wanaume inaweza isiwe ishu kubwa ila kwa sie wa kikeni hiyo vita atakuja kuamua Yesu mwenyewe
Hapo wanaweza kuwa walicheka kinoma

Yaani huo uboya wanaume kufanyiana ni kawaida sana

Hafu uskute mshikaji ndo tabia yake kwenda mjini kula nauli na kumshtua mshikaji Kumsave

Sa jmaa ametumia mbinu ya kijasusi kupeleka ujumbe [emoji41][emoji28]
 
Hapo wanaweza kuwa walicheka kinoma

Yaani huo uboya wanaume kufanyiana ni kawaida sana

Hafu uskute mshikaji ndo tabia yake kwenda mjini kula nauli na kumshtua mshikaji Kumsave

Sa jmaa ametumia mbinu ya kijasusi kupeleka ujumbe [emoji41][emoji28]
[emoji3][emoji3][emoji3] hatari sana
 
Back
Top Bottom